mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
- Unakosoa agizo la Mungu. Msiache kukusanyika pamoja kama ilivyodesturi ya watakatifu. Unakosa Baraka maana kukaa peke yako wakati huna sababu ni laana.
- Rahisi kutekwa na Televangelists wengi ambao ni wajasiliainjili. Kuna watu wameteka mitego kunasa watu wasiojitambua mitandaoni kwa mgonjobwa injili. Utajiweka hatarini maana sio chochote unachokiona ni halisi. Mfano Nabii kijana tajiri wa SA aliwahi kudanganya malaika wameshuka. Kumbe ile video ilikuwa edited na green screen effects za mifano ya malaika.
- Unaanzisha utaratibu mpya ambao Yesu hakuwa nao. Hivyo humfanyi Yesu kuwa kielelezo chako. Yesu alipokuwa duniani kanisa lilikuwa chafu na asi kiliko sasa. Ila hakuacha kwenda kwenye sinagogi au hekaluni kila sabato kama lilivyo agizo.
- Utakuwa umepiga hatua ya tatu ama ya pili kuelekea kwenye kuasi. Hatua ya kwanza ya uasi wa kiibada ya mwanadamu ilikuwa ni Kugeuza siku maalumu ya kukutana ibadani Jumamosi ikamishiwa Jumapili na Ijumaa. Kuacha kukutana na wenzako ni hatua advanced ya uasi ukiacha tu kwamba hatua ya kukutana kinyume na agizo ni uasi.
Note:
Uzi huu hauwahusu wale ambao wako katika mazingira magumu ya kiibada. Ni wagonjwa, hakuna MTU au kanisa wa kukutana nae.