Hasara 4 za Kuabudu kwenye TV badala ya kuhudhuria pamoja na wenzako

Hasara 4 za Kuabudu kwenye TV badala ya kuhudhuria pamoja na wenzako

Thibitisha Mungu yupo kwa njia yoyote unayoijua wewe.
Kama nyumba za ibada zipo na watu mamilioni wanamuabudu na kuthibitisha uwepo wake wewe ni nani.
Mungu ni roho, mambo ya kiroho uthibitishwa kiroho, na sio kisayansi.
 
Kama nyumba za ibada zipo na watu mamilioni wanamuabudu na kuthibitisha uwepo wake wewe ni nani.
Mungu ni roho, mambo ya kiroho uthibitishwa kiroho, na sio kisayansi.
Nyumba za ibada kuwepo na watu mamilioni kumuabudu hakuthibitishi Mungu yupo.

Kwa sababu, hata hao mamilioni hawamuabudu Mungu mmoja.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Nyumba za ibada kuwepo na watu mamilioni kumuabudu hakuthibitishi Mungu yupo.

Kwa sababu, hata hao mamilioni hawamuabudu Mungu mmoja.

Thibitisha Mungu yupo.
Mungu yupo kwasababu hakuna mwenye Kujua chanzo cha Uhai zaidi yake..
 
Kwanza sadaka inapaswa ifike rasmi madhabauhuni na kuombewa pale sio itumwe kwa njia ya MPESA, TIGOPESA au kwa Account namba za Benki.

Wajinga ndio waliwao.
 
Unakosoa agizo la Mungu. Msiache kukusanyika pamoja kama ilivyodesturi ya watakatifu.

Kuna watakatifu makanisa ya leo!? Fanya jaribio dondosha noti kanisani sehemu tofauti tofauti uone kama itatangazwa kuwa aliyepoteza fedha ajitokeze🤣🤣
 
  1. Unakosoa agizo la Mungu. Msiache kukusanyika pamoja kama ilivyodesturi ya watakatifu. Unakosa Baraka maana kukaa peke yako wakati huna sababu ni laana.
  2. Rahisi kutekwa na Televangelists wengi ambao ni wajasiliainjili. Kuna watu wameteka mitego kunasa watu wasiojitambua mitandaoni kwa mgonjobwa injili. Utajiweka hatarini maana sio chochote unachokiona ni halisi. Mfano Nabii kijana tajiri wa SA aliwahi kudanganya malaika wameshuka. Kumbe ile video ilikuwa edited na green screen effects za mifano ya malaika.
  3. Unaanzisha utaratibu mpya ambao Yesu hakuwa nao. Hivyo humfanyi Yesu kuwa kielelezo chako. Yesu alipokuwa duniani kanisa lilikuwa chafu na asi kiliko sasa. Ila hakuacha kwenda kwenye sinagogi au hekaluni kila sabato kama lilivyo agizo.
  4. Utakuwa umepiga hatua ya tatu ama ya pili kuelekea kwenye kuasi. Hatua ya kwanza ya uasi wa kiibada ya mwanadamu ilikuwa ni Kugeuza siku maalumu ya kukutana ibadani Jumamosi ikamishiwa Jumapili na Ijumaa. Kuacha kukutana na wenzako ni hatua advanced ya uasi ukiacha tu kwamba hatua ya kukutana kinyume na agizo ni uasi.
Kumbuka, ni rahisi sana kuacha kusali lakini inagharama kubwa kurudi kusali.

Note:
Uzi huu hauwahusu wale ambao wako katika mazingira magumu ya kiibada. Ni wagonjwa, hakuna MTU au kanisa wa kukutana nae.

Ibada zenu ziwe inclussive, msibague wenye nacho na wasiokuwa nacho, hii ndiyo sababu kuu watu wameanza kushitukia makanisa ya sasa
 
Sababu za kuporomoka mahudhurio ya waumini kwenye nyumba za ibada yamesababishwa - yametokana na nini?

Je, mdondoko huo unaashiria nini?
 
Mungu yupo kwasababu hakuna mwenye Kujua chanzo cha Uhai zaidi yake..

Hapa umechanganya logical non sequitur na circular reasoning.

Kutojua chanzo chabuhai ni kutojua chanzo cha uhai. Kutojua chanzo cha uhai si ushahidi kwamba Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Kwanza sadaka inapaswa ifike rasmi madhabauhuni na kuombewa pale sio itumwe kwa njia ya MPESA, TIGOPESA au kwa Account namba za Benki.

Wajinga ndio waliwao.
Kuna dhehebu/kanisa ambalo SADAKA hazitumwi kwa hizo huduma za PESA?
 
Kuna dhehebu/kanisa ambalo SADAKA hazitumwi kwa hizo huduma za PESA?
Wanatuma dhabihu, malimbuko na michango mbalimbali labda ya jengo au kuwezesha huduma lakini kwa zaka haipaswi kutumwa hivyo.
 
Back
Top Bottom