safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Tabia ya kupenda kukaa peke yangu bila kuwa na mazoea sana na washakaji ama majirani, kuna siku niliumwa wakuu nikakaa ndani siku nzima nakunywa maji tu hakuna anayejua kama naumwa.
Homa ilinikamata vibaya nje sionekani washakaji na majirani wakajua ndio kawaida yangu kuwa ndani kumbe mwenzao maji ya shingo, niko mbali na familia, wife hayupo.
Nikapiga simu kwa wife, wife akasema huyu jamaa atakufa kwa sababu ananijua sina kampani, wife akasafiri kesho yake akaja ndio ikawa afadhali yangu maana ugonjwa ukiwa peke yako unazidi.
Nikasema nikipona mimi jamani ntatafuta washkaji wa kutembeleana ili nikipata matatizo nisaidiwe, baada ya wiki kupona ndio kwanza nikazidi kujichimbia ndani na vitabu vyangu uchwara😀😀😀
Nashauri wakuu tujitahidini kuwa na watu wa karibu washkaji ama majirani, mimi imenishinda kidogo.