Hasara zipi unazipitia kwa kuwa na tabia za introvert?

Hasara zipi unazipitia kwa kuwa na tabia za introvert?

Dah nimejifunza kitu, mimi nikiwa sina hela nahisi ndiyo nakuwa Introvert, nikiwa nazo sijui ndiyo nakuwa Exrovert.
nikiwa na hela kila mtu atajua na hela 😀 navyojipenda acha tu kila mahali nitaenda ata kwa ndugu ambao hata cjawahi kuongea nao.
 
Yaani mimi na vile sina usafiri basi kupita njia za mtaani kwangu inanipa shida sana
Nakuwa free zaidi maeneo ambayo sijulikani
Nikijaribu kuwa extrovert nakereka nalazimika kurudia hali yangu, sizungumzi na mtu nisiyemfahamu, ukinikuta na watu niliozeana nao utakataa ukiambiwa huwa sizungumzi

Tabia zingine za kiduanzi sana

Wewe ni mimi mtupu
 
Tukiwa club hiki ndio tunachokiona
FB_IMG_16194400072995369.jpg
 
Introvertism is a curse,yani hapa nilikua na mipango ya kuoa,nimepeleka barua last monday ila ninavyoandika muda huu nawaza sana sioni sababu za kuoa,ni mambo mengi tu huwa naghairi ghafla
 
Tabia ya kupenda kukaa peke yangu bila kuwa na mazoea sana na washakaji ama majirani, kuna siku niliumwa wakuu nikakaa ndani siku nzima nakunywa maji tu hakuna anayejua kama naumwa.

Homa ilinikamata vibaya nje sionekani washakaji na majirani wakajua ndio kawaida yangu kuwa ndani kumbe mwenzao maji ya shingo, niko mbali na familia, wife hayupo.

Nikapiga simu kwa wife, wife akasema huyu jamaa atakufa kwa sababu ananijua sina kampani, wife akasafiri kesho yake akaja ndio ikawa afadhali yangu maana ugonjwa ukiwa peke yako unazidi.

Nikasema nikipona mimi jamani ntatafuta washkaji wa kutembeleana ili nikipata matatizo nisaidiwe, baada ya wiki kupona ndio kwanza nikazidi kujichimbia ndani na vitabu vyangu uchwara[emoji3][emoji3][emoji3]

Nashauri wakuu tujitahidini kuwa na watu wa karibu washkaji ama majirani, mimi imenishinda kidogo.

Kuwa introvert inadaidia pia. Kwa mfano mtu umeingia Bar umeagiza kuku mzima tena wa kienyeji au mbavu za mbuzi, kumbe wakati unaagiza bar maid alikuwa anapiga chabo! Ukifika unaketi kwenye kiti na kuagiza kinywaji mara unakuta bar maid anakuletea kinywaji na kuanza kuketi hapo hapo huku akiuliza ‘ mbona umepotea siku nyingi’ mara nini na nini! Kumbe alishakuona unaagiza nyama sasa anatengeneza mazingira ili ale pia ile nyama! Hapo mimi huwa naanua kuwa introvert na kumtimua haraka sana!
 
Me majirani zangu ndio hua spendi shobo ila washkaji na wawili watatu ila spendagi kuwatembelea labda kama kuna ulazima sana
 
Kuchoka kuwa introvert ni Sawa na kuuchoka uasilia wako,unaweza jaribu kujibadili ila mwisho wa siku unajikuta peke yako pasipo kupenda
Me mpaka Leo zaidi ya mika 24 cjawai kuwa na mpenzi/demu nikijaribu kutafuta mpenzi kunamaswali huwa najiuliza na kujijibu mwisho Siku zinaenda hvhv
Vipi kusex umewahi?
 
Washikaji wanaopenda jifungia ndani mara nyinhi wanakuaga wachafuuuu...

Ukiingia ghetto yake ndio wale unapata sahani zipo kwa bed, soksi na vinasa vimeanikwa kwa dirisha n.k
Huo umama kujadili mambo ya wanaume wenzio, tena kwenye mageto yao. Acha hizo bhana.
 
Ni Maisha mazuri sana! Unatumia Akili yako 100%..
 
Back
Top Bottom