Hasheem Thabeet afanya kufuru Bilicanas

Hasheem Thabeet afanya kufuru Bilicanas

Huko nyuma waliowahi chezea pesa uwa wanaishia pabaya. Kuna mchezaji mmoja wa mpira wa miguu wa Brazil (miaka ya 80) yeye alikuwa anachukua kiberiti anawasha moto halafu ndo anachukua noti na kuiwasha baadaye anawashia ile noti sigara tena hadharani. Mwisho wake ulikuwa mbaya sana.

Huyu jamaa mimi sina uhakika kama kafanya vile kwani haya magazeti ya Tsh. 100 ni hatari kubwa waweza kukusingizia kitu chochote wapate cha kuandika OVYO kabisa! Yawezekana alimtunza mwanamuziki Dola 50 ( 70,000/=) na kumtunza jamaa mwingine aliyekuwa anacheza vizuri kiasi kama hicho wao wakadai kuwa ametupa pesa.

Lakini kama alifanya hivyo ni vizuri mnaomfahamu mmsaidie siyo kumwombea mabaya
maombi ya kuku hayampati mwewe. tamaa tu na wivu umetuzidi
 
Hashim anahitaji watu wa kumshauri. Hata kina Pipen walifilisika kwa design za maisha kama hizi...
 
inawezekana ana akili. Fujo anafanyia home kwa malofa. Dully kapewa laki, kamwaga laki tatu ukumbini, hazijafika hata dola mia tatu. Kwa mastaa wa kipato chake hela iyo hata chupa ya wine hupati us. Angefanya fujo kwenye klub kubwa us ningemshangaa. Wacha awagawie kidogo wabongo wenzake japo approach yake si nzuri sana
 
jamaa anijifanya anawaiga akina rick ross!!! afu nasikia anachemka tu nba.. smh @ this n*gga!!

@manzese, kwa mfuga mbwa
 
Si ajifunze kwa kuiga kama kina bilgates wanachofanya . achngatie yatima, Ajenge basketball ball court ya nguvu.

Hivi huyo jamaa anaye PR advisor kweli Au ndo wale sasa ana pesa unaweza kukuta anapokea hata shikamoo ya mama yake.
 
nina uhakika hasheem hajatumia zaidi ya 2,000$ sasa hii si pesa kwani hata mimi naweza kufanya matumizi ya pesa kama hii kwa siku mbili tu au siku moja,
kwanza ninavyoona hasheem hajafanya kufuru bado ...inabidi sku moja afunge hi o bilcanas watu wote mrudishiwe pesa yenu(marambili ya mliyolipa) halafu ale bata na wapambe wake hapo ndio kidoogo nitasema kafanya madude yanayotakiwa
 
Hela zake na haki kufanya nazo fujo ya haina yoyote kutoka na akili yake. Kama zikija kuisha namuomba asije akasema kwamba watu wamemroga kama alivyo sema karogwa ndio maana perfomance yake mbovu kwenye NBA.

Kingine pia namshauri kama kweli kafanya hivyo ni kwamba si vizuri kutupa hela kwenye mkusanyiko wa watu kama huo unaweza kusababisha watu waumizane au maafa zaidi. Kuna njia nyingi tu za amani za kugawa pesa.

Kila la kheri Thabeet urudi na nguvu zaidi season inayokuja.
 
Inabid achangie chadema ela ya mana ndo tumuheshimu zaid ya sabodo
 
Mchezo wenyewe umemshinda Marekani anaishia kupigwa benchi na visingizio vya kuwa yeye ni long time project..

Ajiangalie sana isijefikia wakati akaanza kuwa omba omba hao wanaomtia kiburi cha kurusha noti kwa watu watakuwa wameshamkimbia. Ushauri wangu kwa mdogo wangu Hasheem, peleka hela zako kwa charity angalau utakuwa unakumbukwa lakini hiyo style ya kuchezea hela wakati kuna watu wanaitafuta na hawaipati ndugu yangu ni kujitafutia laana.
 
Kila mtu ana style yake ya kula maisha. Sasa sielewi nyie kinawauma nini mazee.? Hamjamsaidia kuosha viatu vyake wala kufanya laundry sasa iweje leo mjifanye mna-care sana. Toeni upuuzi wenu huu.

...with thoughts like these, no wonder Bongoland and Bongomites are where they are, my brother! In the Proverbial Bottomless Pit.
 
Kiukweli huwa nasikia vibaya ninaposikia huyu dogo anachemsha kwenye gem. Ana maisha ya kutosha ndani ya gem. Atumie muda huo vizuri
 
wote hamna hela ndo mana mnasikitika na imani mkizipata mtafanya kama ya hasheem
 
Akili za kibongobongo, mbona wengine wanapata zaidi ya huo mshahara wake lakini hawafanyi mambo kama hayo, ajitahidi kuwekeza nyumbani kabla hajazeeka.
 
Yo Yo keep on doin u! achana nao hawa, ma d*ck riders.
 
Ni hela zake mwenyewe, kazisotea mwenyewe so ana haki ya kuzitumia kadri atakavyo. None of our business!!
 
Back
Top Bottom