Hasheem Thabit, kumbuka nyumbani ule mema ya nchi

Nimeona video Moja jamaa alishawahi fanyaga Clinic ya Basketball hapa Bongo miaka ya nyuma na alikuwa yeye pamoja na Steph Curry ..It seems like walikuwa washikaji enzi hizo ndo wanaingia NBA .
Ile video ilinisikitisha mno nikicheki level ambayo Hasheem yupo compare na Curry .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dekembe Mutombo wa Congo ni Legendary na mpaka sasa ni Balozi wa NBA Africa.. The guy is rich, very rich na ulichosema ni sahihi kabisa, Lebron James, Steph Curry pamoja na vipaji vyao vikubwa walivyokuwa navyo ila season ikiisha wanajipa likizo ya wiki mbili tu wanarudi gym kutrain kwa ajili ya msimu ujao.

Hasheem yeye season imeisha kaja kupiga watu mitama club, kubadilisha club kila uchao na kubadilisha wanawake.. Kuna siku alimtukana mtoto wa Dr. Charles Kimei pale Maisha Club alafu anawaambiwa waiters watoe champagne zote za gharama pale na akawaambia watu wanywe atazilipia..

Fujo zote hizo sasahivi akirudi bongo anajificha Sinza..
 
Hapa ni mungine. Mutombo namjua. Mutombo mafanikio yake yalifungua njia kwa wakongo wenzake kupata nafasi kwenye nba
Hakeem olujuwan alifungua mlango kwa wanigeria wenzake
Kama sio Mutombo basi ni Serge Ibaka ambaye mpaka sasa anakipiga Toronto Raptors. Ni mchumba wa msanii Keli Hilson
 
JoJo jokate nae alikuwa na ndoto za kuwa NBA wife hahahah huwezi jua angekuwa anachill party na akina ayesha curry hahahah

Baadae ya jamaa kuzingua NBA akamtema jamaa saivi DC kisarawe na somebody mistress

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JoJo jokate nae alikuwa na ndoto za kuwa NBA wife hahahah huwezi jua angekuwa anachill party na akina ayesha curry hahahah

Baadae ya jamaa kuzingua NBA akamtema jamaa saivi DC kisarawe na somebody mistress

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua kama jamaa angemuoa au hata kumchumbia JoJo angekuwa still labda yupo NBA bado.. JoJo ana akili sio kama akina Wema..

Na ukichunguza kwa makini mastaa wengi wa NBA wanaoa mapema sana, angalia Lebron, Steph, Kobe walioa mapema sana na hawana scandal za kujinga jinga kabisa za Wanamake..

Hii inaniaminisha mwanamke mwenye akili ana msaada mkubwaa sana kwenye mafanikio ya mwanaume..

Hahahaha eti angekuwa ana chill na kina Ayesha Curry, nimecheka sana kaka..
 
Curry aliendaga hadi kigoma makambi ya wakimbizi kutoa net

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea big point. Watu wanaweza kuchukulia utani.
 
Yes TID alilambwa mitama ya kufa mtu mpaka akazima hahahahaha
Duh angalia sasa ameacha legacy mbaya badala ya kukumbukwa kwa mazuri. Unajua dogo alitakiwa awe mfano wa kuigwa kwa mazuri. Sasa kama kuna madogo walimwona na mitama yake wataenda ku practice mitaani na mitaa itazidi fujo
 
Huyu huyu ambaye kiswahili amesahau siku hizi?
 
Naona hatuelewani, umesema kachezea shilingi, mimi nasema hapana kwasababu kile ndio kiwango chake.
Hivi unajua unachoongea au ni ushabiki. Hivi unajua mpaka uingie NBA unatakiwa uwe umepitia nini na nini? Au unafikiri alichukuliwa tu eti sababu ni mrefu? Huo urefu wake kule US sio big deal labda hapa kwetu walikojaa maandunje..
 
Yes ni kweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…