Hashim Rungwe ahoji: Mtauzaje Bandari zetu?

Hashim Rungwe ahoji: Mtauzaje Bandari zetu?

Akihojiwa na mwandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha CHAUMA ameshangazwa sana na namna DP World walivyopewa bandari zetu.

Mzee Rungwe amesema bandari zetu zilishauzwa tangu day one rais Samia alipokwenda huko Uarabuni mwaka jana.

Rungwe anasema hili jambo la uuzwaji bandari siyo zuri hata kidogo. Akasema kuwa viongozi wote waliopita walifanyw yao lakini hawakuthubutu kuuza bandari.

Mzee Rungwe akasema kuwa suala la bandarini ilikuwa ni issue ya management tu, ni bora hata ingekodishwa management nzuri iendeshe bandari badala ya kuiuza kwa mwarabu. Anasema kitendo cha kusema eti sisi hatuwezi kuendesha bandari ila mwarabu ndo anaweza ni matusi kwetu, maana atakachofanya mwarabu ni kuleta management tu na si kitu kingine kikubwa chochote. Akasema kuwa hata sisi tungeweza pia.

Unaweza kumsikiliza hapa:


Wazalendo wootw hawajaridhika na hili swala
 
Kama kuna jema katika hili la mkataba wa dpw,mbona serikali haizungumzii vipengele vya mkataba badala yake inazungumzia uwezo wa dpw na faida ya uwekezaje au ndio zilezile story za gasi na bomba la mafuta,acheni kuwaona watanzania wajinga kwa kuwa mmeshakula hela ya waarabu.
 
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Huyu Mzee ameshazeeka apumzike sasa alee wajukuu,hafahamu ya kuwa biashara za sasa zinaendana na influence ya muwekezaji, (chain types of tradings) unaweza weka managent hapo na ukapiga mihayo na mizigo ukapata kiducho,due to lack of influence!

Intelegent point ni tunataka Ku trade high au tunataka Ku trade low! We have to choose a way, mtanzania akishapata ugali kibanda Kagari ,haoni mbele tena !

-RAIS WANGU SAMIAH,SONGA MBELE LETS MOVES FORWARD NO TIME TO WASTE!
-Bandari ikiwekezwa vizuri ikaleta tija tarajiwa,waelewa tunafahamu ya kuwa makodi kodi ya hovyo yatapungua huku mitaani,au kufutwa,kodi za Magari zitashuka na mengi tu,kwa sababu SEREKALI itakuwa na vyanzo ambavyo havisababishi mtanzania kuminywa!/kukamuliwa hali ya watoto kupata bulga itarudi madaftari bure mashuleni itarudi na mengi tu.

Ndio mnadanganyana na Bi Samia?
 
Back
Top Bottom