Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, amewataka wananchi wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza kwa wingi kutoa ushahidi mbele ya Tume ya Jaji Lila, ambayo kwa sasa inapokea maoni kutoka kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa muda wa wiki moja.
Rungwe amesema wananchi wanapaswa kuwa na imani na tume hiyo, akieleza kuwa ina uwezo wa kutenda haki kwa kuwa inaundwa na mawakili wabobezi kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia fursa hiyo kutoa maoni na ushahidi wao kwa lengo la kuiwezesha tume kupata maoni ya wananchi wa Kinondoni.
Chanzo: Habari Leo