Naam, Allah mwenyewe, Muumba, ndio kashuhudia hilo kuwa Uislam ndio ukweli. Kupitia Maneno yake aliyoyateremsha (Qur-an).
Ushahidi kuwa ni Maneno yake?
Miongoni mwa ushahidi ni challenge tu aliyoitoa (katika hiyo Qur-an) ya kuleta/kutunga maneno sawa na Qur-an, challenge ambayo haijajibiwa kwa miaka zaidi ya 1400 sasa na kamwe haitojibiwa. Kama Qur-an ingelikuwa sio Maneno ya Allah, basi yangekuwa ni maneno yaliyotungwa tu na viumbe, na kama ingekuwa ni hivyo basi, wangeweza kutunga na mfano wake. Viumbe kushindwa kuleta maneno sawa na Qur-an, ni ushahidi wa kiakili tu kuwa Maneno hayo hayajatoka kwa kiumbe yoyote, bali kwa Muumba mwenyewe.
Aliyeteremshiwa, Mtume Muhammad, hakuwa akijua kusoma wala kuandika wala hakuwa na historia ya uanazuoni au usomi hapo kabla na watu wake walioishi nae miaka yote walimjua kuwa hakujishughulisha na mambo ya kusoma na kuandika kabisa. Alipoteremshiwa na kuanza kuzisoma aya za Qur-an, kwa watu, zilizo katika ufasaha wa hali ya juu mno uliowashangaza hata Maquraish wenyewe wabobezi wa lugha na fasihi, zenye habari za watu waliopita na za mambo yaliyokuja baadae pia, umekuwa ni ushahidi mwengine kuwa Maneno hayo sio yake (Qur-an 29:48). Watu walipoanza kusema kuwa amefundishwa au kutungiwa na mwengine ( imejibiwa katika Qur-an 16: 103), mara waseme ameitunga, mara waseme ni maneno ya mashetani, hoja zao zikakataliwa katika Qur-an kwa hoja zenye nguvu na ikatolewa challenge ya kuleta mfano wake Qur-an. Hakuna aliyeweza sio binadamu wala majini/mapepo. Challenge hiyo utaipata Qur-an 2:23, 10:38-39, 17:88 na 52:33-34 kwa uchache tu.
Ushahidi mwengine ni namna Qur-an ilivyohifadhiwa. Maneno hayo (Qur-an) yamehifadhiwa kama yalivyo tokea Mtume Muhammad alipoteremshiwa mpaka Leo kwa zaidi ya miaka 1400. Visomo vyote vya Qur-an vina chain ya wapokezi inayorudi mpaka kwa Mtume Muhammad tena vile vile. Hili huwezi kulikuta kwa vitabu vyote vya dini zengine ikiwemo Biblia ambayo sehemu kubwa hata waandishi wake hawajulikani. Na hata wale wanaotajwa ni waandishi hakuna uthibitisho kuwa ndio wenyewe kwa sababu ya kukosekana sanad (chain) inayotia nguvu. Tunaweza kuirudisha Qur-an mpaka kwa Mtume Muhammad. Ila hatuwezi kuirudisha Biblia mpaka kwa waandishi wake ambao sio tu hawajulikani, bali maelezo yao yanajichanganya.
Na Qur-an hiyo imehifadhiwa yote na mamilioni ya watu vifuani mwao kiasi kwamba lau kurasa za Qur-an zitapotea zote leo, itaweza kurudishwa yote katika maandishi bila kupotea hata herufi. Kinyume na vitabu vyengine. Na hii ni ahadi imo ndani ya Qur-an kwamba itahifadhiwa na yule aliyekiteremsha bila kupotea (15:9), ahadi hii na kutekelezeka kwake kunaonesha ukweli wa maneno hayo.
Qur-an yenyewe kujitolea ushahidi...
Kwa kutaja kwa uchache tu.
Ushahidi huko juu na hoja nyengine nyingi zinaonesha kuwa Qur-an ni Maneno ya Muumba wa kila kitu. Sasa Allah katika hiyo Qur-an anasema kuwa Dini kwake ni Uislam rejea Qur-an 3:19, ndio dini aliyoiridhia kwetu rejea Qur-an 5:3 na hatokubaliwa anayetaka dini isiyokuwa Uislam rejea Qur-an 3: 83. Hivyo, Ndio, Allah ameshasema Uislam ndio Dini ya kweli.
Mwisho, Uislam ndio Dini inayoendana na maumbile ya kibinadamu. Na mafundisho yake yanakubaliana na uhalisia wa maumbile. Kinyume na Ukristo.
Niishie hapo.
Kisai
Allah ni Mjuzi zaidi