Hasira ni hasara, tujifunze kwa hii story

Hasira ni hasara, tujifunze kwa hii story

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
2,170
Reaction score
3,107
Ni Mkasa Wa Kutengenezwa Lakini Unamafunzo Kwa Watu Walio Kwenye Ndoa.

Mama🙁akimwita Mtoto Wake) Chukua Simu Mpigie Baba Yako Mwambie Aje Malamoja

Mtoto🙁anachukua Simu Na Kupiga) Mama Nimepiga Lakini Kuna Mdada Kapokea Wala Sijaongea Na Baba

Mama🙁anaonekana Kukasilishwa Na Kitu Hicho) Acha Mwanangu We Nenda Kalale Tu, Akiludi Atanikoma

Baada Ya Muda Mfupi Baba Mtu Anaingia, Anapokelewa Na Mangumi, Pigwa Na Pasi, Pigwa Na Jiko, Pigwa Na Dvd Player, Baba Kaumia Damu Chapachapa Mpaka Kapiga Kelele, Majirani Wakafika.

Majirani:kuna Nini Kwani?

Mama:mwanaume Malaya Sana Huyu, Aniambie Alikuwa Na Mwanamke Gani Aliyempa Simu

Baba:jamani Mi Sielewi Kabisa Hakuna Kitu Kama Hicho

Ikabidi Aitwe Mtoto Na Kuulizwa Kilichotokea

Mtoto:nilimpigia Baba Simu Akapokea Mdada Mmoja Hivi Akasema "mteja Unayempigia Hapatikani Kwa Sasa"

Watu Wakashangaa!
 
Ofcz Nililifikilia Hilo Bt Naona Kuna Kitu Ambacho Watu Wanaweza Kujifunza Kutokana Na Maamuzi, Xo Sio Lazima Nifanye Unachotaka, Ushauli Wako Sitaufanyia Kazi, Sory!

hivi ndio vinini!!!!!!!!!!huwezi kuandika kwa ufasaha had uweke xoxo.
Ofcz
Bt
Xo
 
Mimi mtu akiandika coz xaxa ... Ninahisi kichefuchefu picha ninayopata haraka naona ni mtu kavaa kisruali kichafu kifupi kiko china ya magoti hakina risani kimeshikizwa na pini ili kisidonduke nguo ya ndani inaonekana sipendi nasema sipendi kuandika xaxa
 
hivi ndio vinini!!!!!!!!!!huwezi kuandika kwa ufasaha had uweke xoxo.
Ofcz
Bt
Xo

Kuna watu nilikuwa nachart nao wats up,wakawa wanaleta hayo madoido niliandika status flani,mpaka leo bado sijaona wamerudia.

Inakera sana,sijui ndo wana akili sana kuliko walioanzisha hizi herufi! Hata sielewi.
 
ujumbe mzuri, tujifunze kuwa na subira na kutofanya maamuzi wakati ukiwa na hasira
 
Ha ha haaaaa, jamaa naona hayupo tena xaxa.

Mtoa mada ludi bana japo malamoja baxi
 
Mimi mtu akiandika coz xaxa ... Ninahisi kichefuchefu picha ninayopata haraka naona ni mtu kavaa kisruali kichafu kifupi kiko china ya magoti hakina risani kimeshikizwa na pini ili kisidonduke nguo ya ndani inaonekana sipendi nasema sipendi kuandika xaxa
'kisruali'?....'kisidonduke?!.....kireno hicho mkuu au?
 
Back
Top Bottom