Huyu bwana ni mweledi na anajiamini sana anaingia popote na kusema lolote bila woga na pia ana network ya kutosha! Kasoro zake kubwa ni muongo anaweza kukutia maneno ambayo hukuyasema kwa kujiamini kabisa na watu wakamsikiliza. Ana jaziba hapendi kukosolewa, ukijaribu tu atakutotelea lugha chafu. Hawezi tunza siri za mwajiri ukikorofishana nae tu anamwaga upupu hadharani. Ananunulika huyu jamaa kukiwa na cash aaah kweshney. Anakejeli, gubu na visasi visivyoisha. Just imagine stori aliyotengeneza eti walikutana na Karia kwenye shughuli mojawapo, alimuomba msamaha, eti Karia akamwambia aende nyumbani wakaongee huko, alipoenda eti Karia alitoa sharti kwamba lazima wapige picha, halafu aposti kwenye mitandao, baada ya hapo aite wanahabari kuelezea kuomba msamaha huo. Anadai alilazimishwa kufanya hivyo!. Kweli? hii hainingii akilini, na anaongea kwa kujiamini mkavu kabisa.