Napenda kuzungumzia mpira wa Yanga na Simba ndani ya uwanja. Mm Simba damu tena top fan ila huwa siizungumzii Yanga nje ya uwanja kwani sio msingi wa UTANI WA JADI, Hicho unachofanya Gent ni kuvuka mipaka vinginevyo usifanye haya kwa mgongo wa simba na ufanye wewe kama wewe na Yanga yako.
Simba ni familia ya soka na soka linamiiko yake na taratibu zake, kwa akili hizo ndugu yangu basi hata maji hatunyweana mtaani na visa vingi vitarekodiwa vya mashabiki,.
HATUTAKI KUFIKA HUKO.
NB: Point Of Soccer ndipo msingi wa soka ulipo hana mambo mengi dogo na namkubali sana kwani hachezi na jukwaa bali jukwaa linacheza na yeye. Yanga tumewaletea mfano wa kumwiga mazoezini huyu ndiye P.O.S Msingi wa Soka hao wengine wanaiga tu.