Hassan Dilunga wapi Unakwama Brother....

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
6,816
Reaction score
8,809
Wakuu habari zenu....

Leo imenibidi niongee na Hassani Dilunga (HD), Kiungo machachari, Una sifa zoote brother, nilianza kukuona wa tofauti kwanzia mechi ya Nkana, pressing yako sikutofautishi na Oscar aliekua Chelsea.

Sijawahi kukuona umeflop kwenye mechi yoyote kama alivyoflop Firmino jana(mfano halisi) ila unaleta uhai kwenye timu kila unapoingia au unapoanza, nikirudi nyuma kwenye mechi za Simba ulizoanza, washambuliaji wa Simba walikua wanasumbua sana safu ya ulinzi na uhai wa Kiungo unaonekana.

Brother Unakwama wapi?? Sijui tu, macho ya wanadamu yanatofautiana sanaa, Wewe sio wa Simba pale japo basi tu naona kama umesharidhika mzee baba.

Ongeza Jitihada Man, Ongeza Maombi kwa Mungu, nakuaminia sana HD, Unaweza Brooo, Unaweza sannaaaa.

Umri bado unakuruhusu kufanya makubwa zaidi, ila usije ikawa uneridhika kuwa Simba, nakutegemea nikuone hata Championship pale England kwa kua unajua sana kuliko wengi wanaocheza ligi hiyo

Ni mimi Mshabiki wako No.1

 
Tatizo maisha yake ya nje ya uwanja yana muathiri sana na hii ipo sana kwa wachezaji wanaotokea temeke

Ndio maana ukuangalia Temeke kuna vipaji vingi sana lakini hakuna wanaotoboa kufikia hayo mafanikio

Meneja wake ni Cambiaso ambaye anauwezo wa kumpeleka mchezaji timu yoyote Africa

kunajifanya wajuaji wakati bado hawajafika kokote
 
Wakati ligi inaanza huyo feitoto wenu mlikuwa mnamlinganisha na chama baadae mkahamia kwa Mkude Sasa mpo kwa HD yanga mtateseka Sana mwaka huu

Fei toto mimi namuona mlaini sanaaaaaaaa, mechi za nguvu hawezi yule atakua anapumulia oxygen
 

Hapo ndio changamoto inapoanza sasa, Wachezaji wetu sijui wanakwama wapi asee, hajui mpira ndio kazi unayostaaafu mapema sana kuliko zingine
 
Wakati ligi inaanza huyo feitoto wenu mlikuwa mnamlinganisha na chama baadae mkahamia kwa Mkude Sasa mpo kwa HD yanga mtateseka Sana mwaka huu

Feitoto anahitaji muda ule Uzenji umtoke, kiungo mlaini vile hapana
 
Leo Samakiba uliona touch moja mbaya sana alifanya uwanja mzima ulilipuka shangwe. .
Hapo ndio tunakuwa wachezaji wetu wana fail, wakisikia jukwaa basi wanajuwa wamemaliza. Ili kuweza kwenda kucheza huko majuu sio hizo touch ni uwezo wako wakuelewa tactic za kimpira. Ni kama engine ya gari kila part lazima ifanye kazi ili kusukuma gari na ukiwa mchezaji na zaidi wakati hakuna room ya kufanya makosa. nataka nikumbushie tu mechi moja ya Tanzania na Ivory coast, sure boy wakati huo yuko vizuri tu akawa na chenga zake kugeuka mara na watu wanashangilia sana sababu tu kulikuwa na mtu kama Yaya Toure lakini Yaya hakuwa anapiga chenga wala kukimbia hovyo unaona sehemu ya pass anapiga, sehemu ya shoot anapiga na kuna wakati ana jiposition kubana nafasi katika kulinda defenders huwezi kumuona yuko out of position maana itacost team. mfano mdogo wa kwetu huwezi kumuona Samatha anafanya mbwembwe ndio maana anakubalika huko.
 
Uyo fei toto kiukweli hamna kitu pale, yule dogo akizidiwa basi atakuchezea rafu tena yakijinga sana au atakushika, sijawahi ona mpira mzuri kwake wakumlinganisha na mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…