Mabibi na mabwana, usiku wa leo kwa masaa ya Afrika Mashariki, Bondia mtanzania, Hassan Mwakinyo atakuwa anapambana na bondia Liam Smith katika dimba la M&S Bank Arena huko jijini Liverpool.
Liam Smith ana umri wa miaka 33 huku Mwakinyo akiwa na miaka 27.
Pambano hilo limekuja muda muafaka mara baada ya Mwakinyo kuwa nje ya ulingo kwa muda mrefu.
Liam Smith amepoteza mapambano matatu tu katika career yake ya masumbwi.
Yote kwa yote, tunamtakia heri Mtanzania mwezetu Mwakinyo aibuke na ushindi na kuendelea kuitangaza vema nchi yetu.
Tukutane hapahapa jukwaani kwanzia saa 3:00 usiku kwa live updates
Pambano litakuwa mbashara Azam Sports 1HD
====
BONDIA MWAKINYO APIGWA TKO
Bondia Hassan Mwakinyo amepoteza pambano dhidi ya Liam Smith baada ya kupigwa kwa TKO
Pambano hilo lililokuwa na mizunguko 12 limeishia mzunguko wa 4 baada ya Mwakinyo kupiga goti wakati pambano likiendelea
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
MWAKINYO: WALINIPA VIATU VILIVYOKUWA VINANIUMIZA KIFUNDO CHA MGUU
Baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith, Bondia Hassan Mwakinyo ameelezea kilichotokea huku akisema yupo tayari kurudiana na mpinzani wake
Amesema alipoteza begi lake alipokuwa Uwanja wa Ndege, hivyo ilibidi Wenyeji wake wampatie viatu vingine ambavyo vilikuwa vinamfinya na kumuumiza Kifundo cha Mguu
Amesema wakati wa pambano alipokuwa anakabiliana na hali hiyo ilibidi ateme 'MouthGuard' maana Sheria za Boxing zinasema Refa anatakiwa amsimamishe mpinzani na kuliuza nini kinaendelea
Ameongeza "Aliniuliza kama naweza kuendelea, nilimjibu naweza kuendelea lakini viatu vilizidi kuniumiza Kifundo cha Mguu nikaa chini lakini mpinzani akaendelea kunipiga na pamabano likaisha hapo"
Kila la heri ila inatakiwa awe makini yule bondia ni mzoefu halafu ni sugu katika hayo mapambano aliyopigwa lipo na lile alilopigana na Canelo sasa fikiria mtu mpaka kapambana na Canelo c mchezo
Kocha ya uzalendo, lakini mimi ni shabiki lia lia wa mwakinyo.
Sema ana ile style ya kutenga mpinzani napiga tumbo weeee yeye ametenga tu, siikubali aisee
Kila la heri ila inatakiwa awe makini yule bondia ni mzoefu halafu ni sugu katika hayo mapambano aliyopigwa lipo na lile alilopigana na Canelo sasa fikiria mtu mpaka kapambana na Canelo c mchezo