Hassan Mwakinyo ataingia ulingoni Septemba 3, akizichapa na bondia mkali wa Uingireza mwenye mikanda ya WBO

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Baada ya kimya cha muda mrefu kilichomfanya bondia wa Tanzania ambaye kwa sasa anaishi Marekani, Hassan Mwakinyo kupoteza baadhi ya mikanda, bondia huyo atarejea ulingoni Septemba 3, 2022.

Hassan Mwakinyo anatarajia kupigana na Liam Smith bingwa wa zamani wa WBO ambaye amecheza mapambano 35 na alipoteza mapambano matatu tu.

Tofauti ya Liam na Mwakinyo ni umri na idadi ya mapambano waliyocheza. Liam ana miaka 34, Mwakinyo ana miaka 27 na amecheza mapambano 22 ambapo alipoteza mapambano mawili.
 
Mwankinyo ana miaka 27 na kuzeeka koote huko?.
Namtakia ushindi
 
Mwakinyo hajawahi kushinda mkanda wowote wa maana. Labda iwe hii mikanda ya ''kimachinga'' waliokuwa wanashinda kina Matumla. Lile pambano la utanguzi lililoonyeshwa kwenye Sky Sports ndiyo lilitakiwa limtangaze na apate mapambano ya maana lakini naona pengine hana uwezo.
 
Kama ni hivyo bado anayo nafasi kubwa kufanya makubwa.

Mkuu Kidimbwi linj tena?🤣
Dah😅😅..tudiscuss ya mwakinyo mkuu

Kidimbwi wacha tutafute pesa Kwanza maana ili uenjoy kule haupaswi kuwa na hela ya kuuunga unga km Mimi😄,tutarudi Tu MUNGU akijaalia insha'Allah
 
Kila la Kheri Mwakinyo..! Mandonga mtu KAZI ngumi jiwe alijitamba akapigwa, wewe usifanye hivyo

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Nimecheki mapambano ya Liam smith,mwamba ni mbishi na hatari sana round za mwisho,
Natandika mkeka wangu nampa mwakinyo japo najua atoboi.
You're very against mwakinyo..unajua nyingi kila comment zako...unajua nini..wewe mungu...toka zako hapa
 
Mimi mdigo mmojawapo.Team Mwakinyo!!

Hassan Mwakinyo ni bondia mzuri na bado ni mdogo sana ila kafikia ndoto za alieanzisha boxing mtaani Makorora jamaa anaitwa Issa ni marehemu , Issa akawa anahamasisha vijana wote wa Makorora twende nae Tangamano mazoezi community centre hall!! watu tunajificha tukimuona Issa maana masumbwi si kitoto, siku moja moja tulikuwa tunaenda nae just for fun ila mtu ukipigwa ngumi jiwe moja ikajaa vizuri usoni unaona nyota nyota!!kesho wakikuita unalala mbele!!

Marehemu Issa ni ndugu yake na Barua na Tajiri!! Mwakinyo akisoma hii comment atajua hiyo stori!
Vijana wa Makorora na ndoto zetu za kufika majuu!!

All the best Hassan huko uzunguni
 
You're very against mwakinyo..unajua nyingi kila comment zako...unajua nini..wewe mungu...toka zako hapa
Huyu mtoto Mwakinyo ana laana ya kuwatukana viongozi wa ngumi Tanzania.

Refer kauli iliyowahi kutolewa na Raisi wa tasnia hiyo wakati huo marehemu Yassin akimtaka aombe radhi akakataa,mafanikio kwake yatakuwa finyu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…