Hassan Mwakinyo kwa kutua kwako bungeni umejitafutia laana ya bure kabisa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nimekudharau sana bwana mdogo kwa kurubuniwa kizembe sana na kukubali kuingia mkenge wa kutua ndani ya bunge la Tanzania, umebugi sana!

Bunge la Tanzania halijawahi kusaidia mwanamichezo yeyote yule mahali popote nchini Tanzania, Matumla, Cheka walipigwa laana baada ya kukubali kuingia kwenye bunge lisilopenda michezo, labda nikunong'oneze hata huyu mkimbiaji Simbu kwa kuingia kwake bungeni kishajitia mkosi ambao hatakuja tena kunyakua medali hata ya kifuu cha nazi, jaribu kutafakari kabla ya kuamua, hivi ni nani aliyewahi kukujua kutoka ndani ya bunge la Tanzania, kwani ngumi umeanza jana? hivi mnakuwa mmepofushwa vipi hadi kujipendekeza kwa watu wasiowajali hata chembe?

Majuto ni mjukuu.
 
Alialikwa na Spika wa Bunge, kwa mapendekezo ya Wabunge wa JMT.
Kukataa mwaliko kama huo sio jambo la kiungwana kwa Mtanzania yeyote.
unaweza kukubali mwaliko wa kifo kwa vile mwaliko huo umetoka bungeni ?
 
unaweza kukubali mwaliko wa kifo kwa vile mwaliko huo umetoka bungeni ?
Bunge ni Muhimili wa Dola, wenye viongozi wa vyama vyote pendwa vya kisiasa waliochaguliwa na wananchi. Bunge haliwezi kumwalika mtu mwenye kuiletea sifa njema Nchi ili kumdhuru.
Bunge Linaheshimiwa na Kila Mwananchi Mwenye Akili Timamu.
 
Ameshajitia nuksi kwa kitendo cha kuji-attach na Usisiem, anaweza asifanikiwe kwenye mapambano mengine.
 
Amepata miliono 7.7 ,ukijumlisha na zile alizopewa kwenye pambano 6.6 jumla milioni 14.3.
 
Bunge siyo chombo cha kikashifu hata kama yanayoendelea bungeni,siyo hayaridhishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…