Hassan Mwakinyo kwa kutua kwako bungeni umejitafutia laana ya bure kabisa

Hassan Mwakinyo kwa kutua kwako bungeni umejitafutia laana ya bure kabisa

Nimekudharau sana bwana mdogo kwa kurubuniwa kizembe sana na kukubali kuingia mkenge wa kutua ndani ya bunge la Tanzania, umebugi sana!

Bunge la Tanzania halijawahi kusaidia mwanamichezo yeyote yule mahali popote nchini Tanzania, Matumla, Cheka walipigwa laana baada ya kukubali kuingia kwenye bunge lisilopenda michezo, labda nikunong'oneze hata huyu mkimbiaji Simbu kwa kuingia kwake bungeni kishajitia mkosi ambao hatakuja tena kunyakua medali hata ya kifuu cha nazi, jaribu kutafakari kabla ya kuamua, hivi ni nani aliyewahi kukujua kutoka ndani ya bunge la Tanzania, kwani ngumi umeanza jana? hivi mnakuwa mmepofushwa vipi hadi kujipendekeza kwa watu wasiowajali hata chembe?

Majuto ni mjukuu.
Duuh, we jamaa
 
Bado hamjaelewa tu jamani ?
Scientific evidence ya uhusiano baina ya kupigwa kwa Mwakinyo na kuingia bungeni haipo. Anthony Joshua alipigwa mwezi jana, kaingia bunge lipi?
Tuseme na mabondia wengine wanaopigwa huwa wamepitia bungeni. Kila kitu mnalazimisha kiwe CCM vs Chadema
 
Kinachowapeleka Bungeni ni kaurubuniwa ionekane CCM Inasaidia wanamichezo. Ndo maana utasikia "tunamshukuru sana Mama" kwa ushindi. Tumeona na kusikia Mkuu wa mkoa wa Tanga akijinasibu hadharani kisiasa kumsapoti Mwakinyo na kusema ndo Ilani inavyotaka.
 
Mwakinyo sijui kala sh ngapi kwa kuuza pambano ili kumpandisha Liam smith, ilo halipingiki
 
Back
Top Bottom