TANZIA Hassy Kitine, Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama afariki dunia

- Alipotakiwa kumpendekeza mtu mwafaka, Kitine alimtaja Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu . Nyerere alikubali haraka na kumtuma Kitine amuite Mkapa, ambaye baadaye alipata uteuzi wa CCM na kisha kuchaguliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
R.I.P Dr Hassy Kitine.
===
Tuunganishe dots ama tuache?
 
UMRI wa Miaka 35 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa
Mkuu vijana wa sikuhizi sijui tunafeli wapi tumebakia kuwa machawa tu baada tuchangamkie fursa ya Uongozi tumebakia kupiga debe wangombea Wazee.ilitakiwa tuwapumzishe wazee wameshapitwa na wakati, inatakiwa mawaziri na makatibu wakuu wawe na umri chini ya miaka 45 ndiyo tutapata maendeleo.
 
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi, Amina. Pumzika mzee Kitine, huenda Taifa halikudai kitu, ulilitumikia vema
 
Rais na watia nia wa 2015 wanaendelea kutoweka katika uso wa dunia.
 
Rest in peace Dr Hassy Kitine—the former Director General of Tanzania Intelligence and Security Service (1978-1980).

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mbunge wa Makete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayesimamia Usalama wa Taifa, Dr. Hassy (Hassan) Kitine amefariki dunia.

Aliwahi pia kutia nia kugombea Urais wa Tanzania

Pichani ni Dr. Hassy Kitine, PhD aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS (1978 - 1980) akiwa na fomu ya kugombea Urais ndani ya CCM.

View attachment 3418136

=========

Maisha ya Awali na Jeshi:

Kuzaliwa:
Alizaliwa mwaka 1943 Kijiji cha Kisinga, Kata ya Lupalilo, Tarafa ya Lupalilo, Wilaya ya Makete.

Elimu na Mafunzo: Dkt. Hassy Kitine alipata shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kisha alirudi kufundisha hapo baada ya kuhitimu masomo ya juu nje ya nchi, hasa nchini Canada ambako alipata shahada ya uzamili na uzamivu.

Huduma Jeshini: Aliingia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kupanda vyeo kwa kasi. Kufikia mwaka 1971, akiwa Luteni, alihusika katika kuanzisha shule ya maofisa wa kijeshi Monduli (OCS) na alihudumu kama kamanda wa kikosi na afisa wa elimu ya siasa kabla ya kurejea Dar es Salaam kama mhadhiri.

Ujasusi – Mkurugenzi Mkuu wa TISS (1978–1980):

Mnamo mwaka 1978, akiwa na umri wa takribani miaka 35, Dkt. Kitine aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) – akiwa mmoja wa viongozi wachanga zaidi kushika nafasi hiyo. Wakati huo, alikuwa tayari amepanda hadi cheo cha Kanali katika JWTZ.

Alimrithi Dkt. Lawrence Gama, na baada yake walikuja wakuu wengine kama Augustine Mahiga na Imran Kombe. Kipindi chake kilijiri wakati nyeti wa mabadiliko ya kiusalama na kisiasa nchini.

Mahusiano na Mwalimu Nyerere:

- Kitine alijulikana kuwa mshauri wa karibu wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania. Mwaka 1995, siku chache kabla ya uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM, alikwenda nyumbani kwa Nyerere Msasani na kumweleza kuwa hakuna mgombea aliyestahili kutokana na migawanyiko ya makundi.

- Alipotakiwa kumpendekeza mtu mwafaka, Kitine alimtaja Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu . Nyerere alikubali haraka na kumtuma Kitine amuite Mkapa, ambaye baadaye alipata uteuzi wa CCM na kisha kuchaguliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyadhifa Serikalini chini ya Rais Mkapa:

- Mbunge wa Makete: Baada ya Mkapa kuchaguliwa, Kitine aliingia kwenye siasa za kuchaguliwa na kuwa Mbunge wa Makete, akichukua nafasi ya Tuntemeke Sanga.

- Pia aliteuliwa kuwa Waziri wa Afya, na baadaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayesimamia Usalama wa Taifa, nafasi muhimu katika ulinzi na usalama wa nchi.

Kashfa na Kujiuzulu:

- Sakata la Shilingi Milioni 60: Mwishoni mwa miaka ya 1990, Kitine alihusishwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali kiasi cha shilingi milioni 60, zilizodaiwa kuwa kwa ajili ya matibabu ya mke wake nchini Kanada.

- Tukio hilo liliibua mjadala mkubwa na kumlazimu kujiuzulu. Hata hivyo, Kitine alieleza kuwa kashfa hiyo ilikuwa njama ya kisiasa kuzuia azma yake ya kugombea urais.

Msimamo dhidi ya Rushwa:

- Kama mbunge, Kitine alijipambanua kwa kutoa kauli kali dhidi ya rushwa, akilalamikia uharibifu wa maadili ndani ya CCM na serikali. Kauli zake zilichochea mjadala mkubwa nchini na kuvunja ukimya kuhusu rushwa serikalini.

- Alisisitiza kuwa Tanzania ilikuwa inaporomoka kimaadili, ikilinganishwa na enzi za Nyerere. Kauli hizi zilimpatia wafuasi waliotaka mabadiliko ya kweli katika utawala bora.

Azma ya Urais na Maono:

- Mwaka 2015, Kitine alitangaza rasmi nia ya kugombea urais kupitia tiketi ya CCM, akiahidi kurudisha maadili ya enzi za Mwalimu Nyerere.

Alisema: “Nipe miaka mitano tu, nitairejesha Tanzania ya Mwalimu.”

Alionya kuwa Ikulu si mahali pa kuficha udhaifu wala si biashara, bali ni uwanja wa wajibu na sadaka ya uongozi. Alisisitiza sifa muhimu kwa kiongozi ni uadilifu, uzalendo, na heshima kwa katiba.

Urithi:

Ubobezi katika Ujasusi na Uongozi wa Kitaifa: Uteuzi wake kama kijana katika TISS ulionyesha imani kubwa kwake na mchango wake katika katika usalama wa nchi. Ushauri wake kuhusu urais wa Mkapa ulikuwa na maana kubwa katika siasa za CCM.

Uwajibikaji: Kauli zake za hadharani kuhusu rushwa ziliamsha ari mpya ya wananchi na vyombo vya habari kuhoji viongozi, na zilionekana kuwa mwanzo wa mabadiliko ya kisiasa.

Maadili: Licha ya changamoto na kashfa, Kitine alibaki kuwa sauti ya kuhimiza uongozi wa maadili, uwazi, na uzalendo. Wito wake wa kurudi kwenye misingi ya Nyerere umeendelea kupewa uzito mkubwa hasa katika mijadala ya uongozi nchini.
RIP Hassy Kitine.
Ulikuwa gentleman!
 
Tumeshapoa na msiba🙏

Anyway Leo katika pitapita zangu kwenye nyuzi kadhaa zinazoelezea taratibu za kufungua makampuni na usajiri wa biashara, nimekuona ukiwa active sana huko!!
Nipe go on nije pm mkuu.... nipate ABC nisijenaswa na matapeli
 
Kiranga huwezi kosa mchango wako hapa.

Kwa kusoma hapa najiuliza kwanini mzee Kitine alisoma uchumi, ila akapelekwa jeshini kufundisha siasa na akapanda vyeo haraka. Kwanini asingeenda chuo kufundisha uchumi, suala alilosomea. Au baadae uko Canada alisomea siasa.
Canada kulikuwa na kitu hatujakijua vizuri bado.

Ukiangalia wazee wa kitengo wengi kina Kitine, Membe, Mahiga na wengine wa level za chini wengi wamepitia Canada ama ubalozini ama kusoma. Labda Nyerwre alikuwa hataki kupeleka sana watu wake wa intwlligence Uingereza na Marekani.

Wale walikuwa ni vijana wa Nyerere waliochaguliwa na kufanyiwa fast tracking, wengi wao walisoma kwa kipindi kifupi sana wakapata PhD kama Dr. Kitine na Dr. Mahiga, wengine wakaingia vyuoni kufundisha na jeshini kuwa military intelligence. Lengo lilikuwa ni kuingilia kila sehemu, kuichunguza, kui report na kuhakikisha usalama.

Mzee Kitine nilikuwa naonana naye sana kuna wakati kampuni yetu ilitumia nyumba yake moja kama ofisi.

Mengine bado yapo classified 😂😂😂
 
Rest in peace Dr Hassy Kitine—the former Director General of Tanzania Intelligence and Security Service (1978-1980).

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mbunge wa Makete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayesimamia Usalama wa Taifa, Dr. Hassy (Hassan) Kitine amefariki dunia.

Aliwahi pia kutia nia kugombea Urais wa Tanzania

Pichani ni Dr. Hassy Kitine, PhD aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS (1978 - 1980) akiwa na fomu ya kugombea Urais ndani ya CCM.

View attachment 3418136

=========

Maisha ya Awali na Jeshi:

Kuzaliwa:
Alizaliwa mwaka 1943 Kijiji cha Kisinga, Kata ya Lupalilo, Tarafa ya Lupalilo, Wilaya ya Makete.

Elimu na Mafunzo: Dkt. Hassy Kitine alipata shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kisha alirudi kufundisha hapo baada ya kuhitimu masomo ya juu nje ya nchi, hasa nchini Canada ambako alipata shahada ya uzamili na uzamivu.

Huduma Jeshini: Aliingia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kupanda vyeo kwa kasi. Kufikia mwaka 1971, akiwa Luteni, alihusika katika kuanzisha shule ya maofisa wa kijeshi Monduli (OCS) na alihudumu kama kamanda wa kikosi na afisa wa elimu ya siasa kabla ya kurejea Dar es Salaam kama mhadhiri.

Ujasusi – Mkurugenzi Mkuu wa TISS (1978–1980):

Mnamo mwaka 1978, akiwa na umri wa takribani miaka 35, Dkt. Kitine aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) – akiwa mmoja wa viongozi wachanga zaidi kushika nafasi hiyo. Wakati huo, alikuwa tayari amepanda hadi cheo cha Kanali katika JWTZ.

Alimrithi Dkt. Lawrence Gama, na baada yake walikuja wakuu wengine kama Augustine Mahiga na Imran Kombe. Kipindi chake kilijiri wakati nyeti wa mabadiliko ya kiusalama na kisiasa nchini.

Mahusiano na Mwalimu Nyerere:

- Kitine alijulikana kuwa mshauri wa karibu wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania. Mwaka 1995, siku chache kabla ya uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM, alikwenda nyumbani kwa Nyerere Msasani na kumweleza kuwa hakuna mgombea aliyestahili kutokana na migawanyiko ya makundi.

- Alipotakiwa kumpendekeza mtu mwafaka, Kitine alimtaja Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu . Nyerere alikubali haraka na kumtuma Kitine amuite Mkapa, ambaye baadaye alipata uteuzi wa CCM na kisha kuchaguliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyadhifa Serikalini chini ya Rais Mkapa:

- Mbunge wa Makete: Baada ya Mkapa kuchaguliwa, Kitine aliingia kwenye siasa za kuchaguliwa na kuwa Mbunge wa Makete, akichukua nafasi ya Tuntemeke Sanga.

- Pia aliteuliwa kuwa Waziri wa Afya, na baadaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayesimamia Usalama wa Taifa, nafasi muhimu katika ulinzi na usalama wa nchi.

Kashfa na Kujiuzulu:

- Sakata la Shilingi Milioni 60: Mwishoni mwa miaka ya 1990, Kitine alihusishwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali kiasi cha shilingi milioni 60, zilizodaiwa kuwa kwa ajili ya matibabu ya mke wake nchini Kanada.

- Tukio hilo liliibua mjadala mkubwa na kumlazimu kujiuzulu. Hata hivyo, Kitine alieleza kuwa kashfa hiyo ilikuwa njama ya kisiasa kuzuia azma yake ya kugombea urais.

Msimamo dhidi ya Rushwa:

- Kama mbunge, Kitine alijipambanua kwa kutoa kauli kali dhidi ya rushwa, akilalamikia uharibifu wa maadili ndani ya CCM na serikali. Kauli zake zilichochea mjadala mkubwa nchini na kuvunja ukimya kuhusu rushwa serikalini.

- Alisisitiza kuwa Tanzania ilikuwa inaporomoka kimaadili, ikilinganishwa na enzi za Nyerere. Kauli hizi zilimpatia wafuasi waliotaka mabadiliko ya kweli katika utawala bora.

Azma ya Urais na Maono:

- Mwaka 2015, Kitine alitangaza rasmi nia ya kugombea urais kupitia tiketi ya CCM, akiahidi kurudisha maadili ya enzi za Mwalimu Nyerere.

Alisema: “Nipe miaka mitano tu, nitairejesha Tanzania ya Mwalimu.”

Alionya kuwa Ikulu si mahali pa kuficha udhaifu wala si biashara, bali ni uwanja wa wajibu na sadaka ya uongozi. Alisisitiza sifa muhimu kwa kiongozi ni uadilifu, uzalendo, na heshima kwa katiba.

Urithi:

Ubobezi katika Ujasusi na Uongozi wa Kitaifa: Uteuzi wake kama kijana katika TISS ulionyesha imani kubwa kwake na mchango wake katika katika usalama wa nchi. Ushauri wake kuhusu urais wa Mkapa ulikuwa na maana kubwa katika siasa za CCM.

Uwajibikaji: Kauli zake za hadharani kuhusu rushwa ziliamsha ari mpya ya wananchi na vyombo vya habari kuhoji viongozi, na zilionekana kuwa mwanzo wa mabadiliko ya kisiasa.

Maadili: Licha ya changamoto na kashfa, Kitine alibaki kuwa sauti ya kuhimiza uongozi wa maadili, uwazi, na uzalendo. Wito wake wa kurudi kwenye misingi ya Nyerere umeendelea kupewa uzito mkubwa hasa katika mijadala ya uongozi nchini.
Taifa limepoteza mtu na nusu!
 
Pumzika Kwa Amani Mzee Kitine! Taifa litakukumbuka Kwa mengi. Wewe ndiye uliyekuwa Mkuu wa idara nyeti ya nchi yetu wakati nchi ikipitia madhila ya Vita ya Kagera dhidi ya Nduli Idd Amini Dadah. Pengine unao mchango mkubwa katika ushindi tulioupata dhidi ya fashisti Amini.

PUMZIKA KWA AMANI...
 
Huyu ndio kisa kikubwa cha Big Ben kugombana na mshikaji wake Jenerali Ulimwengu
 
UMRI wa Miaka 35 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

..miaka hiyo vijana walikuwa wanapewa shavu ktk vitengo nyeti.

..kwa mfano, kuna jamaa aliteuliwa kuwa Mkuu wa Utawala / Chief of Staff Jwtz akiwa na miaka 33.
 
Back
Top Bottom