TANZIA Hassy Kitine, Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama afariki dunia

R.I.P Dr Hassy Kitine.
===
Tuunganishe dots ama tuache?
 
UMRI wa Miaka 35 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa
Mkuu vijana wa sikuhizi sijui tunafeli wapi tumebakia kuwa machawa tu baada tuchangamkie fursa ya Uongozi tumebakia kupiga debe wangombea Wazee.ilitakiwa tuwapumzishe wazee wameshapitwa na wakati, inatakiwa mawaziri na makatibu wakuu wawe na umri chini ya miaka 45 ndiyo tutapata maendeleo.
 
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi, Amina. Pumzika mzee Kitine, huenda Taifa halikudai kitu, ulilitumikia vema
 
Rais na watia nia wa 2015 wanaendelea kutoweka katika uso wa dunia.
 
RIP Hassy Kitine.
Ulikuwa gentleman!
 
Tumeshapoa na msiba🙏

Anyway Leo katika pitapita zangu kwenye nyuzi kadhaa zinazoelezea taratibu za kufungua makampuni na usajiri wa biashara, nimekuona ukiwa active sana huko!!
Nipe go on nije pm mkuu.... nipate ABC nisijenaswa na matapeli
 
Canada kulikuwa na kitu hatujakijua vizuri bado.

Ukiangalia wazee wa kitengo wengi kina Kitine, Membe, Mahiga na wengine wa level za chini wengi wamepitia Canada ama ubalozini ama kusoma. Labda Nyerwre alikuwa hataki kupeleka sana watu wake wa intwlligence Uingereza na Marekani.

Wale walikuwa ni vijana wa Nyerere waliochaguliwa na kufanyiwa fast tracking, wengi wao walisoma kwa kipindi kifupi sana wakapata PhD kama Dr. Kitine na Dr. Mahiga, wengine wakaingia vyuoni kufundisha na jeshini kuwa military intelligence. Lengo lilikuwa ni kuingilia kila sehemu, kuichunguza, kui report na kuhakikisha usalama.

Mzee Kitine nilikuwa naonana naye sana kuna wakati kampuni yetu ilitumia nyumba yake moja kama ofisi.

Mengine bado yapo classified 😂😂😂
 
Taifa limepoteza mtu na nusu!
 
Pumzika Kwa Amani Mzee Kitine! Taifa litakukumbuka Kwa mengi. Wewe ndiye uliyekuwa Mkuu wa idara nyeti ya nchi yetu wakati nchi ikipitia madhila ya Vita ya Kagera dhidi ya Nduli Idd Amini Dadah. Pengine unao mchango mkubwa katika ushindi tulioupata dhidi ya fashisti Amini.

PUMZIKA KWA AMANI...
 
Huyu ndio kisa kikubwa cha Big Ben kugombana na mshikaji wake Jenerali Ulimwengu
 
UMRI wa Miaka 35 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

..miaka hiyo vijana walikuwa wanapewa shavu ktk vitengo nyeti.

..kwa mfano, kuna jamaa aliteuliwa kuwa Mkuu wa Utawala / Chief of Staff Jwtz akiwa na miaka 33.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…