ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Kisaikolojia Simba huu mchezo walishaupoteza almost wiki sasa maana baada tu kuisha mchezo wa kwanza hapa kwa mkapa...washabiki wa simba asilimia 90.
Pamoja na uongozi wao wakakata tamaa ya kuvuka raundi hii kila walipowafikiria Orlando.
Barbara amezunguka huku na huko hadi serikalini kulalamika akilialia kuwa watafanyiwa fujo...yaani woga tu
Hii nadhani imepelekea kuwaumiza sana kisaikolojia wachezaji wakajiona tu wacha waende tu kukamilisha ratiba!
Lakini kwangu mimi japo mimi ni "mwananchi^ nina imani simba wangejiaminisha kuwa wanaenda kupambana waongeze ushindi wapigane jihadi hakika wangeweza vuka.....bahati mbaya wachezaji wakakosa moral.
Kocha kaweka kikosi cha kujilinda badala ya kushambulia kawaida....matokeo yake wakaelemewa kadi ikatoka wakawa pungufu ati mwalimu ndio anaingiza washambuliaji!
Niseme tu hesabu za benchi la ufundi hazikua sawa kwa vyovyote hii game ilijulikana kuwa ingekua ngumu wao walipaswa kucheza kawaida tu kwa style ya liwalo na liwe.
Wangecheza washambuliaji wanne mbele nina imani huenda orlando wangepigika tu lakini nasikitika ndugu zetu Simba ni kama walisha ingia woga kuwa hawawezi shinda mchezo hivyo kuingia kinyonge.
Poleni sana watani ila mnastahili pongezi kwa japo hapo mlipofikia.si haba.
In Shaa Allah next time mtajipanga na kurekebisha mapungufu.