Hata Hivyo Simba Mliingia Kinyonge Mno

Hata Hivyo Simba Mliingia Kinyonge Mno

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kisaikolojia Simba huu mchezo walishaupoteza almost wiki sasa maana baada tu kuisha mchezo wa kwanza hapa kwa mkapa...washabiki wa simba asilimia 90.

Pamoja na uongozi wao wakakata tamaa ya kuvuka raundi hii kila walipowafikiria Orlando.

Barbara amezunguka huku na huko hadi serikalini kulalamika akilialia kuwa watafanyiwa fujo...yaani woga tu

Hii nadhani imepelekea kuwaumiza sana kisaikolojia wachezaji wakajiona tu wacha waende tu kukamilisha ratiba!

Lakini kwangu mimi japo mimi ni "mwananchi^ nina imani simba wangejiaminisha kuwa wanaenda kupambana waongeze ushindi wapigane jihadi hakika wangeweza vuka.....bahati mbaya wachezaji wakakosa moral.

Kocha kaweka kikosi cha kujilinda badala ya kushambulia kawaida....matokeo yake wakaelemewa kadi ikatoka wakawa pungufu ati mwalimu ndio anaingiza washambuliaji!

Niseme tu hesabu za benchi la ufundi hazikua sawa kwa vyovyote hii game ilijulikana kuwa ingekua ngumu wao walipaswa kucheza kawaida tu kwa style ya liwalo na liwe.

Wangecheza washambuliaji wanne mbele nina imani huenda orlando wangepigika tu lakini nasikitika ndugu zetu Simba ni kama walisha ingia woga kuwa hawawezi shinda mchezo hivyo kuingia kinyonge.

Poleni sana watani ila mnastahili pongezi kwa japo hapo mlipofikia.si haba.

In Shaa Allah next time mtajipanga na kurekebisha mapungufu.
 
Hebu ona hizi konokono za kijani! Tumeridhika wachezaji wamepambana! Penalt hazna mwenyewe! Tukutane jumamos
 
Kocha katuangusha kwa kutomfanyia sub Mugalu. Hakuwa na mchango wwt ndani na ni kawaida yake kufanya mirafu ya hovyo. Stricker anatolewa kwa kucheza rafu ni kichekesho kikubwa. Mshituko wa kadi nyekundu uliwatoa mchezoni na baada ya muda mfupi tu Orlando waliwea kupata goli.
Mkude kuanza kupiga penalty ilikuwa ni kosa kubwa. Alivyoipiga hata mimi hunifungi. Unamuona kabisa anapiga kushoto kwa golikipa.
Wakati mechi inakaribia kwisha angewaingiza kina Bwalya na Nyoni kwa kwa ajili hiyo. Kuwakosa matokeo yake ndio hayo.
Manula penalty ya kwanza hakuwa making. Alikuwa kama yule kipa wa Simba Quines pale kwa kwa Mkapa.
Safu ya ushambuliaji ni butu kweli kweli na mimi simlaumu kocha kwa kujaribu kulinda goli moja. Mugalu awe ni mchezaji wa kwanza kuachwa msimu ujao kwani hana tija yyt kwenye club.
Kocha tatizo lake ni hilo tu la kuchelewa kufanya sub.
 
Halafu kuna uwezekano wa kukumbana na adhabu kutoka CAF kutokana na kile kitendo chao cha kuchoma ile karatasi pale uwanjani.

Na bado wakaishia tu kufungwa! 🤔
 
Jamani kweli binadamu hawana jema, Yaani watu tumepambana hadi matuta,wewe Unasema tuliingia kinyonge kweli?!!. Mbona ninyi Yanga hamjafika popote Mlipigwa nje ndani lkn watu hatukusema lolote?.
 
Tuwe wakweli Simba haina wachezaji
Huwezi mtegemea Mugalu, Kagere, Wawa, Onyango, Sadio, Banda, Mzamiru, Nyoni eti hawa wakupe kombe Afrika
 
Jamani kweli binadamu hawana jema, Yaani watu tumepambana hadi matuta,wewe Unasema tuliingia kinyonge kweli?!!. Mbona ninyi Yanga hamjafika popote Mlipigwa nje ndani lkn watu hatukusema lolote?.
Makolo kila mwaka mnaishia hapo hapo ...si muache kupambana tu sasa
 
Jamani kweli binadamu hawana jema, Yaani watu tumepambana hadi matuta,wewe Unasema tuliingia kinyonge kweli?!!. Mbona ninyi Yanga hamjafika popote Mlipigwa nje ndani lkn watu hatukusema lolote?.
Yanga ile ilikua bado haijakamilika...ilikua baaado subiri jmamosi kwanza
 
Kisaikolojia Simba huu mchezo walishaupoteza almost wiki sasa maana baada tu kuisha mchezo wa kwanza hapa kwa mkapa...washabiki wa simba asilimia 90.

Pamoja na uongozi wao wakakata tamaa ya kuvuka raundi hii kila walipowafikiria Orlando.

Barbara amezunguka huku na huko hadi serikalini kulalamika akilialia kuwa watafanyiwa fujo...yaani woga tu

Hii nadhani imepelekea kuwaumiza sana kisaikolojia wachezaji wakajiona tu wacha waende tu kukamilisha ratiba!

Lakini kwangu mimi japo mimi ni "mwananchi^ nina imani simba wangejiaminisha kuwa wanaenda kupambana waongeze ushindi wapigane jihadi hakika wangeweza vuka.....bahati mbaya wachezaji wakakosa moral.

Kocha kaweka kikosi cha kujilinda badala ya kushambulia kawaida....matokeo yake wakaelemewa kadi ikatoka wakawa pungufu ati mwalimu ndio anaingiza washambuliaji!

Niseme tu hesabu za benchi la ufundi hazikua sawa kwa vyovyote hii game ilijulikana kuwa ingekua ngumu wao walipaswa kucheza kawaida tu kwa style ya liwalo na liwe.

Wangecheza washambuliaji wanne mbele nina imani huenda orlando wangepigika tu lakini nasikitika ndugu zetu Simba ni kama walisha ingia woga kuwa hawawezi shinda mchezo hivyo kuingia kinyonge.

Poleni sana watani ila mnastahili pongezi kwa japo hapo mlipofikia.si haba.

In Shaa Allah next time mtajipanga na kurekebisha mapungufu.
Tunaongea kishabiki zaidi uhalisia tunauacha pembeni. Hivi tukiondoa hiyo mikwaju ya penalty ambayo huwa haina mwenyewe GA ilikuwa ngapi? Timu kama simba kwa uwekezaji wa Orlando kutoana kwa matuta ni jambo la kuwapongeza simba.

Mategemeo ya wengi ilikuwa ni simba atapigwa 5+ huko ugenini. Simba kafungwa goli Moja ugenini mnaibua tena hoja nyingine.

Wakati tunaikosoa simba , tuweke na mifano ya timu ambazo simba anapaswa kujifunza kutoka kwao hapa Tz , timu ambazo zimewahi kupata mafanikio zaidi ya hapo simba alipofika.
 
Back
Top Bottom