GE2025 Hata kama maandamano ya 29/10 hayatafanikiwa, message itakuwa "sent"

GE2025 Hata kama maandamano ya 29/10 hayatafanikiwa, message itakuwa "sent"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hakuna kitu kama hiko , maandamano yasipofanikiwa kitu mbacho ni 1% najua kuna njia nyingine zitatumika.

Message itafika vipi? hivi unawaelewa hao watu au unawasikia?

Pasipo kuwafurusha hakuna lolote litakalobadilika..

Usijipe moyo eti message itafika, ufisadi utaendelea tena mara kadhaa zaidi ya sasa.. mauaji yataendelea..

Nasemaje!! maandamano yatafanikiwa 100% na Tanzania mpya inakuja.
Anyway, tarehe 29/10 baada ya saa 12 turudi hapa tena tuone nani alikuwa mkweli
 
Unafanana na Nape aliyesema madaraka na kushika dola ndio muhimu zaidi kwa CCM mengine baadaye.
Hakuna kitu chochote cha maana cha kubadilisha nchi katika hali channya kitakachofanywa na viongozi watokanao na uchaguzi haramu wa maonyesho kwani hao watawala wanajua hawajachaguliwa na raia na hivyo hawana haja ya kuwajibika kwao.
Kila mahali lazima kuwa na starting point. Hatuwezi kuwa desperate kiasi hicho.

Mwaka 2019 Aala Salah, mdada wa mwaka wa 2 Sudan University aliongoza maandamano yaliyomtoa Omar Bashir. Then Majenerali wakuu wawili wa Bashir: Abdel Fattah Al Burhani wa Sudanese Armed Forces na Mohamed Hamdan Dagalo wa Rapid Support Forces wameigawana Sudan. Ni mauaji na kwenda mbele.

Kufanya maandamano kwa ajili ya kuitoa Serikali kwa kadamnasi bila strategy ni kuleta instability ndani ya nchi
 
Hakuna cha akili kurudi, bali hizo ni facts. Viongozi wote wa ndani ya chama na upinzani walikuwa wanagombea fursa ya kutaka kuiongoza Tanzania. Hivyo anayeshinda lazima azingatie masilahi ya taifa kwanza. Hiyo ndiyo maudhui ya uzi wangu

??!!

G4GVvkJWkAAHLu3.jpeg
 
Hakuna cha akili kurudi, bali hizo ni facts. Viongozi wote wa ndani ya chama na upinzani walikuwa wanagombea fursa ya kutaka kuiongoza Tanzania. Hivyo anayeshinda lazima azingatie masilahi ya taifa kwanza. Hiyo ndiyo maudhui ya uzi wangu
You hooligans your time is up. We have given you so many chances to make it right. Enough is enough, we want our country back. No turning back.
 
Naomba hesabu ya pesa zote zilizotumika katika mchakato wa mwanzo. Pia nipe gharama za pesa za mchakato unaotarajiwa. Na hizi pesa za mchakato tarajiwa zitatoka wapi na ni miradi ipi itasimamishwa hili gharama za mchakato zitimie.
Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia
 
Kwani aliyekwambia time line, mwisho wa ukombozi ni 18:00, 29/10/25 nani?
Rule of nature.

The "Rule of Nature" in philosophy refers to the ordered patterns of occurrences observed in the natural world, characterized by their universality, constancy, and observability
 
Uwezekano wa maandamno kufanyika ni 1% au 0.01 kwa mujibu wa historia, hali ya kijamii na hali ya kisiasa ya Tanzania. Yote kwa yote CCM na Serikali yake wana hoja za kufanyia kazi bila kupuuza:-

1. Kuchunguza matukio ya utekaji, upotezaji, mateso na mauaji ya raia kutoka 2016 hadi 2025, ili kubaini wahusika na kurejesha imani kwa taasisi.

2. Kuundwa kwa Tume Mpya ya Katiba huru yenye uwakilishi wa jamii nzima, ili kukusanya maoni na kujadili masuala kama haki za Tanganyika na utambulisho wa kikatiba.

3. Kuchunguzwa kwa viongozi waliotenda dhulma na kuundwa upya kwa jeshi lenye msingi wa maadili na uwajibikaji, ili liwe chombo cha ulinzi badala ya hofu.

4. Kuachiliwa mara moja kwa Tundu Antipas Mughway Lissu na wengine kama waliotekwa au kufichwa, pamoja na kufutwa mashtaka ya kisiasa.

5. Kuanzisha Sheria itakayohakikisha uwazi na usalama kwa wahanga wa kisiasa, ili warudi nchini bila hofu au kulipiziwa kisasi.

6. Kuhakikisha kuna uwajibikaji kwa utekaji na ufisadi unaoongezeka, ikiwemo upotezaji wa watu na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

7. Kurejesha amani ya kweli kupitia haki, uadilifu wa taasisi na ulinzi wa raia dhidi ya vurugu za serikali.
Niamini mimi Comrade! Ikitokea vijana wakajitokeza kweli na baadhi yao kukubali kujitoa muhanga; aisee jeshi litachukua nchi. Na sababu ni moja tu;

Watu wengi (wakiwemo wale wa kwenye chama na vyombo vya ulinzi) wamekosa imani na kiongozi mkuu wa nchi kutokana na mapungufu yake mengi ya kiutawala anayo yaonesha mpaka sasa.

Naungana na wewe kwenye hizo hoja zako ulizo zitaja. Zote ni za msingi, zina ukweli na zimebakia kuwa kero kwa wananchi walio wengi.

Ila mwisho wa siku changamoto iko kwa wahafidhina na wahuni wachache ndani ya chama, wasiopenda kutanguliza maslahi ya Taifa mbele! Na badala yake wamekuwa mara zote wakitanguliza kwanza maslahi ya ccm mbele, halafu yanafuatia maslahi yao na familia zao; na maslahi ya Taifa yanawekwa mwisho kabisa!!

Hivyo bila ccm kuondolewa madarakani, kamwe nchi haiwezi kupata katiba mpya na bora! Nchi haiwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi! Nchi haiwezi kuwa na vyombo huru vya dola, mahakama, bunge, nk.

Sababu siku zote ccm hutanguliza maslahi yao kwanza na yale maslahi msingi ya Taifa, huwekwa mwishoni.
 
Baada ya Uchaguzi utakao tawala ni Mkono wa Chuma, Wenye Chama wasipojiongeza 2030 mgombea wa Kiti Kikuu atapata shida sana pengine anaweza kuwa defeated kabisa
 
Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia
Naam hilo nalijua. Leo nahitaji kujua gharama halisi (Tanzanian Shillings) ya hii demokrasia ya kutunga katiba mpya kwa wakati uliopita na tunaoendea . Ni miradi ipi itasimamishwa ili tupate rasilimali fedha za kutunga hii katiba.

Natanguliza Shukrani kwa majibu.
 
Baada ya Uchaguzi utakao tawala ni Mkono wa Chuma, Wenye Chama wasipojiongeza 2030 mgombea wa Kiti Kikuu atapata shida sana pengine anaweza kuwa defeated kabisa
Siamini kwenye mkono wa chuma, naamini kwenye maridhiano
 
Naam hilo nalijua. Leo nahitaji kujua gharama halisi (Tanzanian Shillings) ya hii demokrasia ya kutunga katiba mpya kwa wakati uliopita na tunaoendea . Ni miradi ipi itasimamishwa ili tupate rasilimali fedha za kutunga hii katiba.

Natanguliza Shukrani kwa majibu.
Mwaka 2014 bajeti ya Katiba mpya ilikuwa Tsh 450 Bilioni. Kuhusu miradi ipi itasimama ni suala la mipango tu
 
Hayo yote uliyoyafanya bi Samia alikuwa ana nafasi ya kuyafanya tangu March 2021 hadi July 2025 miaka 4 ni mingi tu.

Mtangulizi wake alivuruga vitu vingi tu na yeye alitakiwa kufukia mashimo na kutibu makovu mengi aliyoyakuta alijitahidi walau miezi 3 ya mwanzo ila baada ya hapo alirudi kule kule na sasa ameshika njia ile ile ya mtangulizi wake na akajiita kabisa chura kiziwi.

Hicho anachofanya Samia sasa hakina tofauti na upumbavu aliofanya Magufuli 2020 hivyo wote wanaingia kapu moja na japo Samia anaonekana kavuka maouvu ya yule mtangulizi wake.

Mimi nilikua miongoni mwa watu wa kwanza kupinga habari za maridhiano na niliona ni kiinimacho katika maridhiano yale yasiyokua na afya kulingana na gravity ya wahanga wa matukio ya mtangulizi wake niliona Samia kachukua pande fulani tu kujipatia turufu ya kisiasa na sio kuponya makovu na kuirudisha nchi katika umoja.

Najua mnaweza kubisha ila niseme tu wazi naliona giza na ombwe kubwa la mgawanyiko katika kiti anacholazimisha Samia aendelee kukikalia.

Nakupa mfano tu mwepesi umeona siku cpt Tesha kaongea, je ulifanya utafiti wa haraka kuona mapokeo ya cpt Tesha na kauli zake toka kwa wananchi?

Jibu unalo pengine kama hamkujifunza pale mkaona Tesha ndio kikwazo akawa "neutralized" basi watanzania watatafuta njia nyingine ya kupeleka vilio vyao na pengine njia hiyo haitopendwa na watawala ambao ni kikundi kidogo kinachoogelea kwenye bwawa la ufisadi kutokana na kodi za wananchi.

Niseme tu , Samia kachelewa sio kidogo bali sana.

Adíos.
 
Uwezekano wa maandamno kufanyika ni 1% au 0.01 kwa mujibu wa historia, hali ya kijamii na hali ya kisiasa ya Tanzania. Yote kwa yote CCM na Serikali yake wana hoja za kufanyia kazi bila kupuuza:-

1. Kuchunguza matukio ya utekaji, upotezaji, mateso na mauaji ya raia kutoka 2016 hadi 2025, ili kubaini wahusika na kurejesha imani kwa taasisi.

2. Kuundwa kwa Tume Mpya ya Katiba huru yenye uwakilishi wa jamii nzima, ili kukusanya maoni na kujadili masuala kama haki za Tanganyika na utambulisho wa kikatiba.

3. Kuchunguzwa kwa viongozi waliotenda dhulma na kuundwa upya kwa jeshi lenye msingi wa maadili na uwajibikaji, ili liwe chombo cha ulinzi badala ya hofu.

4. Kuachiliwa mara moja kwa Tundu Antipas Mughway Lissu na wengine kama waliotekwa au kufichwa, pamoja na kufutwa mashtaka ya kisiasa.

5. Kuanzisha Sheria itakayohakikisha uwazi na usalama kwa wahanga wa kisiasa, ili warudi nchini bila hofu au kulipiziwa kisasi.

6. Kuhakikisha kuna uwajibikaji kwa utekaji na ufisadi unaoongezeka, ikiwemo upotezaji wa watu na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

7. Kurejesha amani ya kweli kupitia haki, uadilifu wa taasisi na ulinzi wa raia dhidi ya vurugu za serikali.
Mawazo mazuri sana, lakini mawazo yako yanapingana na uchafu wa Demokrasia. Hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali baada ya uchaguzi bado itabagazwa na kuchafuliwa kuwa si lolote Wala chichote. Hii ndiyo Demokrasia. DEMOKRASIA haitaki utulivu ktk jamii ndiyo maana hata Kikwete alipoamua kuanziaha mchakato wa Katiba mpya baada ya kilio Cha muda mrefu, bado haikupatikana sababu ya DEMOKRASIA. DEMOKRASIA ulitaka kukwamisha ujenzi wa Miradi ya maendekeo kuanzia barabara, ununuzi wa ndege, ujenzi wa viwanja vya ndege, bwawa la Umeme, Reli ya SGR n.k. Tushukuru Kuna Rais aliamua kuziba masikio. DEMOKRASIA ni kuchafuana na maadamu wako wakubwa wanaotoa pesa na kufadhili kuchafuana huko hayatakoma. Ni mpaka mtakapopiganishwa mkachoma moto nchi, Akili ikiwarudi ndipo mtajua kumbe tulikuwa tunagombashwa.
 
Nakupa mfano tu mwepesi umeona siku cpt Tesha kaongea, je ulifanya utafiti wa haraka kuona mapokeo ya cpt Tesha na kauli zake toka kwa wananchi?

Jibu unalo pengine kama hamkujifunza pale mkaona Tesha ndio kikwazo akawa "neutralized" basi watanzania watatafuta njia nyingine ya kupeleka vilio vyao na pengine njia hiyo haitopendwa na watawala ambao ni kikundi kidogo kinachoogelea kwenye bwawa la ufisadi kutokana na kodi za wananchi.

Niseme tu , Samia kachelewa sio kidogo bali sana.

Adíos.
Kwa taarifa yako, Kepten Tesha ni project ya waliomteka Polepole. Angalia zile picha za chumba ambacho Polepole alikuwa anatumia kuongelea, then linganisha na ile meza na background ya Kepteni Tesha. Zina ufanano. Pili kumbuka script aliyokuwa anaisoma Tesha, halafu linganisha na maudhui ya Polepole aliyokuwa anaongea. Ni mwandiko wa Polepole.

Kepteni Tesha aliongea tarehe 4/10 na Polepole alinyakuliwa tarehe 6/10, na hatujamsikia Kepteni Tesha tena. Watekaji walimtengenezea mtego Polepole kupitia Kepteni Tesha kama panya anavyotegwa kwa mfupa wa samaki, kisha Polepole akaingia mazima
 
Wewe ulikuwa mtu wa kwanza humu kusema cpt Tesha sio mwanajeshi ni AI tu ile kweli si kweli?.

Ok sasa nakuuliza tena Cpt Tesha ni mwanajeshi au sio mwanajeshi,?
Kepteni Tesha aliongea tarehe 4/10 na Polepole alinyakuliwa tarehe 6/10, na hatujamsikia Kepteni Tesha tena. Watekaji walimtengenezea mtego Polepole kupitia Kepteni Tesha kama panya anavyotegwa kwa mfupa wa samaki, kisha Polepole akaingia mazima
Hao watekaji wa Polepole walitoka wapi??

Na wewe unajuaje huo mtego au sio mtego?

Je kosa la Polepole lilikuwa ni lipi?

Je kosa la Polepole halikuweza kusikilizwa kisheria?

Mwisho tena nakuachia swali je baada ya cpt Tesha na Polepole kupotea ndio suluhu ya mwisho kumaliza ukosoaji na jw ukosoaji umeisha kabisa kwamba watu wote sasa ni mstari mmoja kusema MAMA HANA DENI??

NB: Matatizo ya miaka 6 yangeweza kutatulika tu kwa miaka 4 ila sasa ni 10 huwezi yatatua kwa kujidanganya usiku mmoja tu nikuhakikishie muda haudanganyi.

Mimi nimefungia mjadala hapa.
 
Mawazo mazuri sana, lakini mawazo yako yanapingana na uchafu wa Demokrasia. Hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali baada ya uchaguzi bado itabagazwa na kuchafuliwa kuwa si lolote Wala chichote. Hii ndiyo Demokrasia. DEMOKRASIA haitaki utulivu ktk jamii ndiyo maana hata Kikwete alipoamua kuanziaha mchakato wa Katiba mpya baada ya kilio Cha muda mrefu, bado haikupatikana sababu ya DEMOKRASIA. DEMOKRASIA ulitaka kukwamisha ujenzi wa Miradi ya maendekeo kuanzia barabara, ununuzi wa ndege, ujenzi wa viwanja vya ndege, bwawa la Umeme, Reli ya SGR n.k. Tushukuru Kuna Rais aliamua kuziba masikio. DEMOKRASIA ni kuchafuana na maadamu wako wakubwa wanaotoa pesa na kufadhili kuchafuana huko hayatakoma. Ni mpaka mtakapopiganishwa mkachoma moto nchi, Akili ikiwarudi ndipo mtajua kumbe tulikuwa tunagombashwa.

Hakuziba masikio ila yeye ni chura kiziwi. Maajabu ni pale chura akisikia achilia mbali akiwa kiziwi!
 
Back
Top Bottom