Hata kama majigambo ni asili yao ila hii imezidi sasa, ni kabila gani hili wemeanza sifa za kuzika kwa kutumia crane?

Hata kama majigambo ni asili yao ila hii imezidi sasa, ni kabila gani hili wemeanza sifa za kuzika kwa kutumia crane?

Mapembelo.....!
Tuweke ukabila pembeni lakini kwa mtazamo wa akili ya kawaida msiba ni sehemu ya kuomboleza, watu wana uchungu kumpoteza marehemu lakini kwenye hio video naona majigambo yametawala zaidi
 
Tuweke ukabila pembeni lakini kwa mtazamo wa akili ya kawaida msiba ni sehemu ya kuomboleza, watu wana uchungu kumpoteza marehemu lakini kwenye hio video naona majigambo yametawala zaidi
Nimeishi na watu wa makabila mbalimbali lakini makabila ya watu wa kanda ya ziwa kiukweli wana kaushamba fulani hasa kwa hawa wahaya yaani wana ushamba fulani ambao kwa watu waliozoea wanaona ni ulimbukeni fulani umewajaa!

Msiba ni maomboleza, huzuni inafaa ichukuliwe hvy na zaidi ni kuwafariji wahusika wa moja kwa moja, kuleta mbwembwe na kusababisha taharuki km hy ya kuanguka kwa jeneza ni kuzidi kuleta simanzi kwa wafiwa!
 
Kwa hiyo nshomile ndo wamefikia kuwa na sifa za kijinga namna hii? basi nimewashindwa hawa watani zangu natangaza rasmi kuwagawa....
 
jeuri ya pesa
Muleba hapo, kijiji Kahumlo
Kwanini mnakuwaga waongo? Apo ni Uganda Kabale unasikia ata lugha ni kiganda unasemaje ni Muleba? Usilijua kaa kimya. Achaga misifa sifa ya kijinga. Hakuna Muhaya wa akili hizi.
 
Kwanini mnakuwaga waongo? Apo ni Uganda Kabale unasikia ata lugha ni kiganda unasemaje ni Muleba? Usilijua kaa kimya. Achaga misifa sifa ya kijinga. Hakuna Muhaya wa akili hizi.
duh, punguza hasira, tafuta pesa komredi
 
Ukisikia sifa zinaua ndio huku, Hapa kwa mporomoko huu wa jeneza sijui kama waliodondokewa na jeneza walipona?

Humo kwenye jeneza mwili wa marehemu ushavunjika vunjika kwajili ya hizi sifa.

Utasikia kisingizio ni jeuri ya pesa lakini ukifatilia unakuta pesa zenyewe ni mshahara wa kuajiriwa, hapo inabidi ushangae tu maana kuna makabila yana wafanyabiashara wakubwa ambao wanaingiza faida maradufu ya huo mshahara kila siku lakini kwenye misiba huwezi kuta hivi vitu.

Msiba ni maomboleza, huzuni, inafaa ichukuliwe hivyo na zaidi ni kuwafariji wahusika wa moja kwa moja, kuleta hizi mbwembwe na kusababisha taharuki kama hii ya kuanguka kwa jeneza ni kuzidi kuleta simanzi kwa wafiwa, kumkosea heshima marehemu, kuongeza gharama za msiba na hata kusababisha vifo vya ziada.

View attachment 2444067
Duh!!
 
Back
Top Bottom