Hata kama mkeo na watoto unawapenda usisafiri nao kwenye gari moja; wahenga waliishi muda mrefu kwa kukwepa haya

Kumuomba Mungu atuepushe na mabaya yote alivyopanga kutuchukua atatuchukua tu haijalishi mkiwa pamoja au tofauti. Humu kwenye safari za magari binafsi kuna uzembe mwingi sana unafanyika. Mfano siku moja nilikua natoka dar kwenda klm njiani nikapita petrol station moja nikapaki nikaingia chooni nikakutana na jamaa yuko vyombo japo sio dereva nikamtania tukacheka kila mtu akatoka wakati naondoka wakaniuliza hapa na wapi nikawaambia naingia kilimanjaro. Basi nikatoka wakanipita kibati sana na ndani mziki mkubwa na totoz zinafurahi nilipofika maeneo ya chekereni nakuta ajali na ndio wao wamebamiza gari kwenye kalavati dereva hajaumia sana ila wale wala bata alooo hawatamaniki, hivyo uzembe na kujiachia safarini kuna mchango mkubwa sana kwenye kupoteza maisha. Napenda sana kusafiri na familia yangu ila nakua na utulivu wa hali ya juu mixer maombi ya wife na maji ya baraka lazima yahusike kabla ya safari kuanza unaweza ona jambo la kawaida ila kwenye imani nakua nimekata minyororo mingi ya mabaya
 
Nimeiona hiyo habari. Mungu awatangulie wana familia akawe mfariji wao. Back to the topic mtoa mada uko sahihi kabisa ni vyema kujigawa kama mko wanne basi walau wawili mpande usafiri tofauti kwa kiasi inaweza saidia.
 
Ajali ni ajali tu, Kikubwa uwe umempa Yesu maisha yako, ukifa uende mbinguni, duniani tunapita.
 
Hizi ni juhudi zetu wanadamu hasa tunapofikwa na mambo magumu na yenye kuumiza mioyo yetu....

Lakini kiimani kila mja ataondoka kwa wakati wake.....na wakati wake ukifika haijalishi mko pamoja au mpo mbali mbali bali ataondoka......kila mja ataishi na kurudhukiwa kwa kadri alivyokadiriwa.......kuanzia uhai mpaka ridhiki.......

Hekima na busara sio kuogopa kifo bali ni kujiandaa na maisha baada ya kifo kwa kuyazingatia maarisho yake na kukaa mbali na aliyoyakataza.....

Mungu atujaalie mwisho mwema kwenye maisha yetu.......


IJUMAA KAREEM......
 
Kanuni yangu ni kutokutumia chombo kimoja Cha usafiri na mke wangu kipenzi..........hata likitokea watoto wetu wasikose wa kuwasimamia

Japo Naamini kifo hakiepukiki na Siku yako au zenu zikiwa zimefika mtaunganishwa na mauti bila kujali umbali mliopo
 
Uaishi Mtwara, kwenu Bukoba, mmechukua likizo na mnapaswa kusafiri mwezi wa 12, una ki VANGUARD chako cha mkopo, hapo mtafanyaje?
 
Haya maisha pamoja na kwamba hatujuchagua kuzaliwa, bado tuna nafasi kubwa sana ya kuya shape. Yatupasa tuishi kimachale sana, siyo mbaya kujifanya Komando kipensi au machale mengi kama vile Bruce Lee.
Trust in God, yes, but close your doors.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…