Kanuni Huwa haibadiliki.....ni eidha Yeye aende hiyo likizo na baadhi ya watoto na Si na watoto woote na Sisi Wengine tutasubiri Next likizo
Mkuu Mtongwe,
Tahadhari ni lazima kuchukua....lakini kifo hakikimbiliki ukifika wakati wake Mkuu....Labda wazazi wangu waliniathiri, nimesafiri mno na familia yangu, nikiwa na maana mke na watoto wangu, lakini hata nikiwa mtu mzima tumesafiri sana na ndugu zangu wa kuzaliwa, misiba, harusi na hata kusamilia ndugu....na hata kuvinjari tu! Labda niseme tu, licha ya tahadhari, ulinzi wa Mwenyezi Mungu umekuwa juu yangu.
Na kwa upande wangu binafsi, kuendesha gari ni kama hobby, miaka ya nyuma tukiboreka na mke wangu, ni kuchukua watoto siku ya Weekend, Mnatoka Mbezi ya barabara ya Bagamoyo, mnaenda hadi Pungu Kajiungeni, mnapinda kulia na kuendelea hadi kuja kutokea Kigamboni, vuka pantoni kurudi Mbezi, au Mbezi, unaelekea Bagamoyo, Msata, Chalinze na kurudi Dar...just for fun. Njiani mnanunua maembe, mananasi, mihogo kutokana na msimu.....imeacha kumbukumbu kwa wanangu. Safari za Dar hadi Morogoro nimezifanya mara nyingi, ni streach ambayo inabidi uwe mwangalifu mno mno. Nimepoteza rafiki yangu katika kipande cha Dar/Moro....lakini haikuzuia njaa yangu ya kuendesha.
Sijawahi ogopa kuwa barabarani na familia! Ikifika siku kuondoka Imefika....ukiogopa sana unaweza shindwa furahia maisha! Ni mafupi sana anyway!.