Hata kama ni MC wa kukodi, kwanini akodiwe mtu aliyefungiwa?

Hata kama ni MC wa kukodi, kwanini akodiwe mtu aliyefungiwa?

Kesi ya mpira haiendi mahakama za kiraia, labda iwe rushwa
Haya mambo kisiasa pia yapo . FIFA Wanakataza serikali kuingilia mpira lakini umeona serikali ya uingeleza ilichofanga kwa Chelsea ? Haya niambie nini kimetokea ?
 
Bado sijaelewa hili jambo , ilidaiwa Manara kafungiwa asishiriki shughuli za Soka za ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili , sasa leo kaonekana kwenye tamasha la Yanga , KWA KISINGIZIO CHA MC WA KUKODIWA , na baada ya kumaliza kuwatambulisha wachezaji wa Yanga , Manara amedai kwamba hajihusishi na soka na anaondoka kwenda huko Kigogo kufanya shughuli zake za UMC kwenye harusi .

Hili jambo limekaaje jamani ?
Siku zote watu hukodi MC wanayemfahamu na vizuri zaidi kama anawafahamu nyie pia.
 
Mbona hujibu swali, ule u "MC" wake leo pale uwanjani, haukuwa kwenye shughuli ya mpira?

Hapa usilete huruma ya kipato, suala la kipato kama vipi akauze magodoro ya GSM, ila sio kwenye shughuli ya mpira.
Kwani TFF walipomwambia anaruhusiwa kuingia uwanjani kutizama mpira anakuwa hajajihusisha na mpira?. Hizo conditions walizompa ndo zimepelekea hayo yote . wao wangesema HARUHUSIWI KUJIHUSISHA NA MPIRA KWA NAMNA YOYOTE full stop . lakini kuanza kusema Mara unaruhusiwa kupost hiki. Mara unaruhusiwa kuingia uwanjani ......... Hapo ndo walipojikologa
NB. Manara amepewa nakala ya hukumu?
 
hii ni wiki ya mwananchi ina mambo mengi sana na mpira n sehmu ndogo tu ya shughuli ya nzima
 
Yanga ni mwanachama wa TFF
Mimi nadhani Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa ndiyo maana tuna shirikisho la soka nchini(TFF). Yaani Yanga anawajibika kwa DRFA kwa mambo madogo kama ya Yanga day lakini suala la Ligi msimamizi ni TFF mwenyewe (Nawaza)
 
Unajua ulichokiandika au ? Ina maana TFF haina taarifa ya tukio Hilo.?.elewa pia imelikwa timu ya nchi jirani unadhani wamekuja tu kama wanakuja kumsalimia mjomba wao...unajua criteria za FIFA kwa friendly mechi ...YANGA ni mwanachama wa TFF either anafanya jambo Lililo kwenye kalenda au laa, msimamizi wake ni TFF
Ndiyomaana nikaandika ni mwendo wa kuvurugana , mwenyewe sielewi!
===
The Tanzania Football Federation (TFF), previously Football Association of Tanzania (FAT), is the governing body of football in Tanzania and oversees the Tanzania national football teams. It was founded in 1930 and is affiliated to FIFA since 1964.
===
Wanasema Wana shughulika na timu za Taifa.
Sasa nimeelewa baada ya kuguugo!! Nimesoma article 12 Membership ya katiba ya TFF.Kweli TFF wameshikiria mpini, Yanga tuna Makali. Manara ni wakuadhibiwa! Ikiwezekana na Yanga iadhibiwe kwa kuleta mchafuzi wa michezo nchini!
 
Ni dhahiri Yanga inaendeshwa kihuni Sana .ni Kama wamemwambia wewe kuwa MC hakuna mtu wakukufanya kitu.Lakini watu professional na wenye hekima wangeona hili jambo kwa mapana.
Yanga mwenye akili alikua Senzo, wengine wahuni tu. Huyu keshaambiwa hata siku ya Mwananchi ipo under TFF as Yanga ni mwanachama sasa kaamua kudharau. Halafu akiadhibiwa anaanza kuharisha mdomoni...
 
IMG-20220806-WA0013.jpg
 
Mpeni jamaa nakala ya hukumu hayo yote yataisha . Nakala ya hukumu hamtaki kumpa mnahofia atakata rufaa . huku kanuni zenu zinasema adhabu itaanza kuhesabika Mara tu mtuhumiwa anapopewa nakala ya hukumu. Mnajikaanga kwa mafuta yenu.
Alishapewa mbna, labda hufuatilii habari.
 
Kosa kubwa sana yanga wamefanya.wakiadhibiwa watasema wameonewa.Ngoja mtaniambia
 
Ila mnajua kurukaruka, adhabu inaanza baada ya kupewa nakala, je nakala ameshapata ili adhabu ianze mbona mnarukaruka hapa!! Porojo nyingi, adhabu inaanza vipi wakati nakala hajapata! Je nauliza tena nakala yake ameshapewa!!!
 
Back
Top Bottom