Hata katika lugha ya Kiswahili, Kenya wametudhibiti kimataifa

Hata katika lugha ya Kiswahili, Kenya wametudhibiti kimataifa

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Na Elius Ndabila
0768239284

Ni kweli kuwa lugha ya Kiswahili pamoja na historia yake kubwa, lakini ni ukweli kuwa inazungumzwa sana pwani ya Afrika Mashariki. Na Tanzania ndiyo nchi ambayo ni Mama wa Kiswahili.

Tulimushuhudia Rais wa awamu ya Tano akitumia kila jitihada za kukuza na kueneza Kiswahili. Ni waazi kuwa ndoto yake ilikuwa ni kuona siku moja Afrika yote inafundishwa na kuzungumza Kiswahili.

Tanzania tu kuwa chimbuko la lugha ya kiswahili ingetumika kama fursa ya kutengeneza ajira kwenye nchi zinazotaka kufundishwa kiswahili.

Sina uhakika kama Watu wanajua kuwa Kenya ndiyo inajulikana kama nchi ya Waswahili. Kenya inajulikana kuliko Tanzania. Hivyo nchi yoyote ikitaka kutafuta Mwalimu wa Kiswahili inaenda kutafuta Kenya na si Tanzania. Fursa za ajira ambazo zingetengenezwa Tanzania zinaenda Kenya.

Ukisoma hata kwenye mitandao ikiwepo App ya language Translate wanakuletea Kenya Swahili na si Tanzania Swahili.

Hii inadhihilisha wazi kuwa bado kwenye diplomasia ya uchumi Kenya wametumia vizuri fursa kuliko Tanzania. Kitendo tu cha App kutokuonyesha Tanzania Swahili na kuonyesha Kenya Swahili huu ni ushahidi tosha kuwa Kenya wanafanya vizuri.
 
Kenya pia ni chimbuko la lugha, sema pwani lote la A. Mashariki.
 
Watu kwenda kutafuta walimu Kenya hakumaanishi kenya inazungumza Kiswahili kuliko Tanzania.

Kuna kitu extra hapo ambacho limeangaliwa.

Watu wanaenda kutafuta walimu kenya kwakua wanajua kenya ina idadi kubwa ya watu wanaojua kuongea Kiingereza.

Hivyo huwezi kumfundisha mtu kiswahili ambaye anajua kiingereza endapo utakua hujui lugha ya Kiingereza ambayo inayokuunganisha na mwanafunzi.

Ni sawa na mchina ambaye hajui kiingereza aseme akufundishe kichina wewe unayejua kiswahili pekee, itawezekana vipi?
 
Tatizo watanzania bado washamba kwenye nchi za watu.

Wanaowakilisha kiswahili kwenye mataifa ya kigeni ni nchi ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Wasomalia walioishi Kenya na Kenya maana hawa wako wengi kwenye mataifa ya nje.

Marekani kuna mitaa au viwanda wafanyakazi wanaongea Kiswahili, watu hao ni kutoka nchi nilizotaja.

Wabongo si wengi nchi za watu ni ngumu kuwakilisha kiswahili
 
Watanzania ni werevu wa unafiki na uzandiki tu.

Labda tuanzishe chuo cha unafiki Cha kimataifa
 
Back
Top Bottom