Hata mkoloni hakuondolewa kwa mtutu, bali Gen Z, Mbegu ya Ujasiri: Last Man Standing Kati ya Nyota za Mashahidi

Hata mkoloni hakuondolewa kwa mtutu, bali Gen Z, Mbegu ya Ujasiri: Last Man Standing Kati ya Nyota za Mashahidi

FlyingDutchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2022
Posts
459
Reaction score
862
Tulikua vitani, tukipigania uhuru kwa amani.
Rafiki zangu waliuawa kikatili na askari.
Mikononi mwao hawakubeba hata jiwe la kupigania,
lakini walipigwa risasi viunoni, vifuani, na hata kichwani,
ili kututisha, ili kutunyamazisha, ili kutuvunja moyo.

Walio tangulia nawaombea mbele ya MUNGU,
awafanye kuwa nyota angani.
Na mimi niliyesalia, ndiye last man standing.
Nimevaa ujasiri wao kama nguo isiyochakaa.

Hata mlio wa risasi ukipiga,
kwangu ni kama ngurumo ya radi yenye mvua nene,
ijazayo ardhi harufu ya udongo ulionywa uhai.
Haunitishi tena, bali hunikumbusha lengo,
nikae tayari nife kifo kilicho na heshima.

Nikiondoka kwenda vitani,
mkumbusheni mwanangu kuwa sikumtenga kwa hiari,
ila naenda kupigania kesho yake,
ili asije kukatwa kama kuku na kutupwa gizani bila majina.

Na mkianza mazishi yangu, msiseme ni msiba.
Mimi ni mbegu mnayopanda ardhini.
Na ikijalia Maulana, nitaota na kuchipua,
kuwa msimbo wa kuwakumbusha
kuwa kila Mtanzania anastahili haki,
si kutekwa na wasiojulikana.

Na tutashinda.
Kwa sababu manabii wapo upande wetu,
walimu wa dini na rabi wanatuombea,
na sauti zao zinapanda juu kama moshi mwororo wa uvumba.
Hapa siyo jambo la kibinadamu tu,
jambo hili MUNGU yupo upande wetu.
Kwa hivyo uhalali wetu ni wa angani na ardhini,
na ushindi wetu utaandikwa katika pumzi za vizazi.

Pichani ni picha ya shujaa anaeshitakiwa kwa kosa la uhaini
Screenshot_20251108-174039_1.jpg
 
Tulikua vitani, tukipigania uhuru kwa amani.
Rafiki zangu waliuawa kikatili na askari.
Mikononi mwao hawakubeba hata jiwe la kupigania,
lakini walipigwa risasi viunoni, vifuani, na hata kichwani,
ili kututisha, ili kutunyamazisha, ili kutuvunja moyo.
Tutaisha mtoa mada ushairi unahamasisha ila tupange mikakati inayoeleweka sio ya mikono mitupu, tutaisha.
 
Tutaisha mtoa mada ushairi unahamasisha ila tupange mikakati inayoeleweka sio ya mikono mitupu, tutaisha.
Itoshe kusema historia mpya imeandikwa nami nitawaenzi ndugu zangu kwa kuandika kitabu chenye hisia na mwanga kuwakumbuka toka moyoni.

Amini tunaye MUNGU na kizazi chenye akili sana kuliko waliowaua ndugu zetu kama Hitler.

Hatuta isha Bali tutaishi.
 
Kijana utafaa uwaziri wa hekima katika nchi ya ahadi, ujumbe ni mzuri sana zaidi ya dhahabu.
 
Kijana utafaa uwaziri wa hekima katika nchi ya ahadi, ujumbe ni mzuri sana zaidi ya dhahabu.
Baraka zako napokea🙏, japo moyoni Bado nina majonzi mazito! Nyama za moyo wangu Bado zatetema na kutoka jasho la damu.

Nilizoea kuyasikia haya Mogadishu lakini Leo nimeyaona Tanzania Tena kwa kiini Cha macho yangu

Nawakumbusha ndugu zangu "A lion can be born mighty, with fangs like promises and a roar that shakes miles. But if he stays where the grass is soft and the meals come easy, his power dulls. Not in one moment, but slowly. The world forgets him. And worse, he forgets himself.".

We are lions who has spent a long time in confort zone"
 
Back
Top Bottom