Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hizi kauli za kumuangalia mtu na kusema hata muonekano wake tu unaonyesha yule ni kahaba, mdangaji, mwizi shoga, muuaji, ana roho mbaya n.k ni kauli za hovyo sana. Yani mtu anaweza kumuangalia tu mwanamke amevaa mini skirt, ana tatoo mkononi au shingoni, kichwani ana bleach na mguuni ana kikuku akajiamulia tu huyu ni kahaba, anajiuza, malaya au malaya mzoefu.
Mtu anaweza kumuangalia tu mwanaume jinsi anavyotembea, kuongea au amevaa kinjuga kimebana unasikia anasema "huyu kasha left group", "lile papai" au ni shoga
Mtu anaweza kukamatwa na polisi na kwa sababu polisi wamejijengea utamaduni wa ku parade kila aina ya watuhumiwa mbele ya vyombo vya habari unasikia mtu anasema "kwa kumuangalia tu sura" yake yule atakuwa kweli muuaji, kahaba, ana roho mbaya n.k
Mtu anaangalia tu kichwa cha mtu anasema kwa kuangalia tu kichwa chake atakuwa hana akili! Hivi kuweli muundo wa kichwa cha mtu unaweza kukujulisha kama anazo au hana akili??
Hizi na kauli nyingine za aina hii ni kauli za hovyo sana zinazotumiwa na watu wapumbavu zaidi.