Hata sijamtongoza

Hata sijamtongoza

Mr mgeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,222
Reaction score
805
Habarini wana JF,

Nina rafiki yangu wa kike tulisoma nae elimu ya sekondari tulipendana kama marafiki na alikuwa akinipenda sana ila mimi sikumpenda kimapenzi japo ni mzuri,miaka minne imepita sikuwa na mawasiliano nae kwa sababu nilikuwa mbali nikiendelea na masomo ya juu, yeye yupo Arusha na mimi nilirejea Dar,akapata mawasiliano yangu tukawa tunawasiliana alilalamika sana sababu sikutaka kumtafuta,akaanza kuniomba vocha,pesa vyote nilimsaidia kibinadamu.

Nimekuja kushtuka jana baada ya kuniambia baby naomba hela nikanunue kuna nguo nimeipenda halafu wiki ijayo nakuja.

Msaada jaman na mimi nina mpenzi wangu.
 
Mmmmmhh!!hizi njaa njaa na tamaa ya vitu itampelekea kuitwa wa VIBOMU!
 
kaona humtongozi kaamua kujitongoza na week ijayo anakuja unatakiwa uelewe hivyo na ujiandae kwa ujio wake.
 
Umeshamfahamisha kuwa wewe una mtu wako? Maana haya mambo mengine huwa tunayatengeneza wenyewe halafu mwishoni tunalalamika, kwa mfano ulichukua hatua gani alivyokuita Baby wakati wewe upo kwenye mahusiano mengine ambayo unayaheshimu?
 
Kama unajijua una mpenzi inatakiwa kuwe na mipaka kwa hao marafiki zako,
ushalikoroga mpe tu hizo hela
mi ningekuwa huyo dem nakuomba tu, yani naomba tu
eti una mpenzi hata sisimizi nae ana mpenzi wake
mmmmmm...!!
 
kama umesoma nae ana kigezo cha kukupiga vibomu na kuhusu nanilihii muonjeshee kama hutaki nipe namba yake huku atakusimulia magoli
 
Kama unajijua una mpenzi inatakiwa kuwe na mipaka kwa hao marafiki zako,
ushalikoroga mpe tu hizo hela
mi ningekuwa huyo dem nakuomba tu, yani naomba tu
eti una mpenzi hata sisimizi nae ana mpenzi wake
kwi kwi kwi bingwa la kuharibu !!sasa si amesoma nae?sema anataka amuonjeshe na mgegedo wake !!haki ya nani mimi nisingemuacha hata ningekua na nyumba ndogo zingine 10(INAONGEZA HADHI YA KIUME)
 
Nina rafiki yangu wa kike tulisoma nae elimu ya sekondari tulipendana kama marafiki na alikuwa akinipenda sana ila mimi sikumpenda kimapenzi japo ni mzuri

Je hapo awali alijua kuwa hauna mapenzi naye?

Tatizo ni dogo sana, mnaishi dunia moja lakini nchi tofauti...

Anyway siku atakayofika mjini nenda kampokee ukiwa wewe na mchumba/mpenzi wako halisi na hakikisha zoezi la utambulisho linafanyika vyema...

Baada ya hapo nin uhakika hutapata tena usumbufu...
 
Umeshamfahamisha kuwa wewe una mtu wako? Maana haya mambo mengine huwa tunayatengeneza wenyewe halafu mwishoni tunalalamika, kwa mfano ulichukua hatua gani alivyokuita Baby wakati wewe upo kwenye mahusiano mengine ambayo unayaheshimu?
sasa mkuu mambo yangu mimi hayamuhusu,hakuna ulazima wa yeye kujua mimi nipo kwenye uhusiano,ishtoshe kipindi tunasoma nilikuwa na mpenzi sikujua kama alijua au hakujua kutokana na tabia zangu za upole na kuwa serious sana.
 
kwi kwi kwi bingwa la kuharibu !!sasa si amesoma nae?sema anataka amuonjeshe na mgegedo wake !!haki ya nani mimi nisingemuacha hata ningekua na nyumba ndogo zingine 10(INAONGEZA HADHI YA KIUME)
mkuu ni binti mzuri kaumbika sana tatizo simtamani kimapenzi hata kidogo.Kuhusu suala la namba nisamehe bure itakuwa si ungwana
 
Back
Top Bottom