SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
AFCON inatarajiwa kuanza huko Ivory Coast chini ya miezi 4 kutoka sasa. Unaenda kutafuta mechi ya ushindi lakini mategemeo yako ni kina Boko ambao hawajacheza mechi ya ushindani kitambo sana maana tayari wameonekana ni liability katika timu pamoja na kwamba kuna viongozi pale Simba wanamkingia kifua. Una Mbwana Samatta ambaye naye wote hata wasiojua mpira wanaona ni mzigo pale uwanjani. Kuna Msuva ambaye pamoja na kwamba amekuwa na bahati ya kuipatia magoli Stars ila naye ni machachari ila siyo hatari. Hawa ndiyo tunategemea kuwapeleka huko Ivory Coast maana usitegemee waachwe wakati ndiyo wanaonekana walioivusha timu. Wengine ndiyo kina Mzize, yaani ni masikitiko makubwa.
Halafu kuna ahadi ya yale mamilioni kama watafuzu. Unajiuliza hizo pesa zitagawanywaje kama wachezaji wanabadilishwa kila siku. Kuna waliopambana katika mechi za nyuma ili hata timu leo iwe na matumaini ila leo hii hawapo kwenye kikosi, kuna wengine wameitwa kwa mechi ya leo ila kwenye mapambano ya nyuma hawakuwepo wala kuonekana kama wana faida. Cameroon waliahidiwa nyumba walipofanya vizuri kombe la dunia 1990 ila imechukua miaka 30 kupewa hizo nyumba na sababu moja ya kuchelewa ilikuwa chama cha soka cha kule walipeleka majina ya wachezaji 44 wanaotakiwa kupewa nyumba badala ya wachezaji 22 ambao hasa ndiyo walikuwepo kwenye kombe la dunia. Toka 1990 wamekuja kupewa hizo nyumba 2020. Ngoja tuone.
Tukifungwa, tena tufungwe goli nyingi itatupunguzia visirani, rushwa na mengineyo. Itatusaidia pia kujenga utaratibu wa uwajibikaji katoka football siyo huu ujinga.