Hata tukifuzu kwa mazingaombwe hatuna timu ya kupeleka AFCON 2023

Tumefuzu,Ili ndo la msingi
 
Kuna taaluma na ushabiki, nyinyi mashabiki kuna wakati mpuuzwe tu kwakuwa hamna msaada wowote ndani ya uwanja. Hata hayo mliyojifunza kwenye maisha bado hamjafikia mafanikio makubwa ya kujitapa,Sasa huku kwenye soka kocha anajua fika kuna mashabiki wasiojua kitu ila watajifanya wanajua dawa yao ni kuwazimia fegi tu ndio kocha alichofanya.
 
Hao Niger walipomuweka nje huyo Adebayor wakashinda ngapi? Mpira sio kukimbiza kuku kuwa mwenye mbio ndio akimbize. Kocha amekaa na wachezaji anajua nani ana fitness na utayari wa kukabiliana na adui kutokana na mbinu za mchezo, Sasa wewe upo huko hujui hata wachezaji wamejifunza nini na mwalimu kaona nini eti unakuja unadai kocha kakosea.. Wale wachezaji sio maroboti ya kuendeshwa na rimoti, kuna saikolojia inazingatiwa kabla hata mtu hujampa jukumu la kupigana. Kama unaona ile kazi ni rahisi jaribu siku uone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…