Asante mkuu nilikuwa nahitaji kitabu cha kaliba hii na umekileta kwa wakati.
Mkuu kitabu kinatisha sana.
Mfn, kijana anasimulia kwamba..
Kuna siku waasi walivamia kiji jirani, wakati kijiji hicho kinavamiwa, wao (kijana anaesimulia na wenzake 5) walikuwa wanaelekea uelekeo huo huo. Sasa, walikutana na watu wengi sana wanakimbia vita na wengi wao walikuwa wanavuja damu sana.
Wengine walikuwa wanakimbia bila kujua kama wamejeruhiwa na wanatoka damu, hadi walioofika mahali wakakaa wenzao ndo wanawaambia kuwa wanatoka damu.
Wengine walikuwa wanakimbia wamebeba watoto mikononi amabo tayari wameshakufa ila wao wanajua watoto bado wako hai, hadi pale walipofika sehemu wakitulia ndo wanagundua mtoto alishakufa zamani.
Kwa mfano, kuna mama alikuwa amebeba mtoto mgongoni, katika kukimbia, mtoto alipigwa risasi akiwa mgingoni akafa, ila mama yake aliendelea kukimbia akijua mtoto wake yuko salama, hadi alipofika sehemu walipo watu wengine, akakaa chini, akawa anamshusha mwanae amnyonyeshe, kumshusha mtoto, macho yako wazi lakini alishakufa zamani.
Oya kitabu kinatisha hatari.
ππππ