Hata Wamarekani hawaamini tena katika elimu ya shule zao

Sisi tunasoma mambo mengi sana hadi tunachanganyikiwa..unashindwa kujua hata wewni bora kwenye nini kwasababu kila kitu unagusagusa tu ufaulu
 
Sidhani kama huyo mtu mmoja uliyemtaja anaweza kuwakilisha Merekani, huyo amekuja na mtizamo wake kutokana na mahitaji yake ya wakati husika. Kama ilivowahi kutokea TZ aliyekuwa waziri wa elimu TZ Hayati Joseph Mungai alivofuta masomo ya biashara, kilimo na ufundi na kuunganisha Fizikia na Kemia kuwa somo moja. Hiyo ilikuwa hoja yake na si ya watanzania
 
Kidari komeo la chuma yuko sahihi sana, suala la mtu binafsi kuamua kufanya kitu kwa ajili ya familia yake huwezi ukalifanya kuwa suala la wamerekani hata kidogo, Kwa hiyo wewe ukimpeleka mtoto wako akasoma mchepuo wa Cambridge tayari linaitwa suala la wa Tanzania? Lakini kwa kuwa umekariri utopolo umeshindwa kuona hoja ya komeo la CHUMA
 
Huyu bwana Elon huwa ana maamuzi ya ajabu sana kwahiyo anawaandaa vijana wake kwenda kwenye mradi wake wa Mars colonisation
 
Chuo ca Havard kilifanya research kwa watoto 1200, toka wakiwa na umri mdogo kabla ya kuanza shule. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
wakati ni wadogo, zaidi ya 90% ya watoto hao walikuwa ni wabunifu na walikuwa na kila criteria ya kuitwa ma genius
Wakaja fanyiwa tathimini wakiwa wmefikisha tena miaka 9 na wakiwa washaanza shule, wakagundua namba imesuka mpaka 30%. Wengi wamepoteza ubunifu kabisa.
Wakaja fanyiwa tena wakila elementary school wakaundua only 12% ndiyo wamebaki.
Wakaja fanyiwa tena baada ya miaka kibao, ikagundulika imebaki only 2%.


Elon Musk lenog lake kubwa lilikuwa ni kuwaepusha watoto wake na hili jambo. Kwakuwa elimu ina tutrain katika uelekeo flani inatuondoa katika ubunifu. Shule yake ya Astra Nova inalenga kuwafanya watoto waendelee kuwa wabunifu.

Halafu pia title yangu ilikuwa ni kuwavutia watu wasome habari yangu...
 
Kaamua kufungua shule yake baada ya kuona elimu anayotaka kumpa mtoto wake haiwezi kupatikana kwenye shule za serekali au nyingine binafsi...
 
Ilikua ni ya Tanzania maana alitekeleza kwenye shuke za serekali sio shule zake binafsi...hilo halikwepeki
 
Huyu bwana Elon huwa ana maamuzi ya ajabu sana kwahiyo anawaandaa vijana wake kwenda kwenye mradi wake wa Mars colonisation
Ana miradi mingi na ni CEO wa kampuni kibao ikiwemo Tesla Motors, Space X, HHyperloop, Solarcity, OpenIA

Sasa hii OpenAi ni habari nyingine. Mpaka sasa imeweza tengeneza system ambayo unaweza chat nayo kam mtu, unaweza ipa kicha cha habari ikaandika habari ukiisoma ukahisi imeandikwa na mtu. Unaweza kuipa poem ikaandika poem kama hizo hata mia.
Unaweza ipa story ikaandika story yenye kueleweka yenye niche ya story uliyoipa isome. Inaweza kufanya mengi sana
 
Hapa sasa nimekuelewa.maana kuna watu walikuwa wanatetea ujinga ulioandika utadhani we mume wao... Nimekusamehe.

Duh. Umenikata maini kabisa.sikuwa nimefikilia vizuri.ila ndo najifunza toka kwenu wasomi.sema umetumia lugha kali sana.ndo na sisi pia muwa mnatufikilia tunapojifunza kuandika
 
nimekuelewa sana, masomo mengi hayana faida wala hayaji kumsaidia mtoto baadae anapokuja kwenye uhalisia wa maisha,alivyovisoma shule hawezi kuja kuvitumia baadae, masomo ya practical ndio yanahitajika kuliko ya theory
 
Sikujua kama unamtetea sababu ni bwana ako. Nlidhani unatetea ana points.kumbe unaangalia maslahi yako?mmeoana rasmi ando ndo hivyo tu?
Hii coment umequote umeitoa wapi? Mbona sijaandika upuuzi kama huo
 
Sisi hata kuamini matokeo ya uchaguzi ni shughuli.
Katika nchi yetu hakuna lolote la kuamini, labda uhai wetu kwa muda wa sasa hivi, maana lolote laweza kutokea. Walinda usalama hawaaminiki, wanasiasa hawaaminiki, watoa elimu hawaaminiki, matabibu na wakunga hawaaminiki, wafanyabiashara hawaaminiki ilimradi ni ubabaishaji kila sekta.
 
Hapa sioni kuwa hawaamini elimu yao bali utaratibu wa kuitoa hiyo elimu. Huyo Musk yuko alipo kwa kupitia elimu ya wote, sasa kaona inachukua muda mwingi kumfikisha hapo, ndio katafuta njia mbadala.
Elimu isiyoaminika ni ya kwetu ambayo mhitimu hakidhi mahitaji ya uelewa wa kazi aliyoisomea.
 
kuna mwandishi mmoja nguli wa habari za makala,ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mmoja hapa nchini enzi za utawala wa kikwete awamu ya pili alikuwa na mtaala wake sambamba na mtaala rasmi kwenye shule yake, ingawa alijaribu kushawishi uingizwe kwenye shule zote wahusika hawakujali
 
mitaala yetu imepitwa na wakati,haimsaidii mhitimu kujimudu bila kuajiriwa,halafu ina ukomo wa kufahamu mambo mapya,sasa hivi mhitimu wa kidato cha nne ni debe tupu,haajiriki kama msomi. Utakuta alisoma masomo yote ya sayansi lakini haruhusiwi hata kufundisha shule ya msingi licha ya kusheheni maarifa mengi.Ni ujasiriamali na ufundi mchundo ndio umekuwa mkombozi mkombozi kwa wahitimu wengi walioshia ngazi za chini za elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…