Hatari kubwa: Elimu ya Tanzania inafundisha watoto kuwa vigeugeu

Hatari kubwa: Elimu ya Tanzania inafundisha watoto kuwa vigeugeu

Jasusi Mbobezi

Senior Member
Joined
May 17, 2020
Posts
194
Reaction score
851
Mfano mmoja ni huu:

Mtoto akiwa darasa la kwanza anaambiwa 1-2= Haiwezekani halafu akifika darasa la sita anaambiwa 1-2= -1 hiki kitu kinaonekana cha kawaida ila ni kosa kubwa sana.

Marekani kuanzia kindergarten watoto wanafundishwa 1-2= -1 na inaenda mpaka chuo kikuu.

Kwa elimu niliyopata usishangae Mimi Jasusi Mbobezi Mwanzo niliunga mkono njia A, sasa ninaunga mkono njia B yaani sieleweki.

Tubadilike jamani.
 
Acha uongo. Nimefundisha American International School. Ulichosema hapa ni uongo. Hicho ulichosema kipo hata kwenye physics. O level mnaambiwa mwanga husafiri katika mstari ulionyooka. Mkifika A level mnaambiwa mwanga uweza kupinda.
 
Nafikiri ni stages Tu Kwa kuwa ubongo bado haujachangamka
 
Anaye kwambia elimu bure yeye anatumia mamilioni kusomesha mwanawe

Wanaokwambia ujiajiri yeye na ukoo wake ni waajiriwa,"jiongeze"za kuambiwa changanya na zako.
 
Acha uongo. Nimefundisha American International School. Ulichosema hapa ni uongo. Hicho ulichosema kipo hata kwenye physics. O level mnaambiwa mwanga husafiri katika mstari ulionyooka. Mkifika A level mnaambiwa mwanga uweza kupinda.
Labda kama umefundisha American International Schools zilizopo hapa nchini ambazo zinajinadi kutumia mitaala ya Marekani. Lakini kama siku moja utaenda America hebu fanya utafiti kwenye hili utagundua hata mitaala inayotumika huku Africa ina mapungufu ndomaana wazungu wenye akili hawawaleti watoto wao kwenye shule za bongo zinazotumia mitaala yao bali huwasomesha kwenye nchi husika.
 
Shida yetu Kama taifa ni lugha ya kufundishia. Bado tunaangaika kuamua ni lugha gani tuitumie katika elimua (KISWAHILI AU KIINGEREZA).

Ukombozi wa kweli upo katika lugha.

Angalia nchi zilizopiga hatua Kama China, Indonesia, Maleshia, Kenya, Afrika ya kusini, Nigeria, Misri, Morocco, Singapore, nk.
 
Back
Top Bottom