Hatari, nyanya moja shilingi 500

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,427
Reaction score
4,944
nyanya moja kwa sasa inauzwa shilingi za kitanzania 500.

muuzaji hapepesi macho wala wamung’unyi maneno.huwezi amini ila bahari ndo hiyo.

sijajuwa bado kama nchi imewekewa vikwazo au serikali iliyopo imefeli kusimamia uchumi wa nchi. miradi mikubwa inayotafuna pesa za walipakodi nayo ujenzi wake kuna suasua. pita pale gold star dar es salaam uone. hakuna kitu mtu wangu kuna manondonondo tu na nyenzo nyenzo kama vile kuna kazi lakini kiuhalisia hakuna kazi inayofanyika.

madege yetu nayo ukipita pale karibu na airport yapo yamepaki tu kama ng’ombe wapo zizini.

magufuli nchi imemshinda?

 
Huu ni msimu wa mvua mkuu, zao la nyanya halihimili mvua kwa hiyo ukuaji wake na uzalishaji ni changamoto hivyo kupelekea bei kuwa juu, sasa hapa serikali inaingiaje, ili nyanya zishuke bei inategemeana na uchache wa mvua.Halafu kuna binadamu wanafikiri kilimo ni rahisi kama kutema mate.
Nb. Lima zako uuze shilingi 10/- nyanya moja.
 
Unajua sijuagi kwanini watu hawataki wakulima wanufaika na kazi za jasho lao?

Mimi ni mwalimu nadhani hatutofautiani sana na hawa wenzetu wakulima
Yaani wanavyokandamizwa wakulima ndivyo na walimu tunavyokanyagiwa na hii awamu.

Mkulima anapelekeshwa hatakiwi kupata faida akipandisha bei ya bidhaa yake hata kwa msimu tu kelele lake na yowe hilo sio la mchezo ukipandisha bei ya mahindi, karubwagira, tembele , nyanya chungu au bamia kila mtu anaona kaonewa kama vile walimu yaani hamna posho ya chakula, wala makazi wala ya wenzi wala uniforms. Kibaya zaidi huku hata ukijiendeleza sijui Masters sijui PhD unaambiwa unajifurahisha haina acknowledge yoyote wala daraja.

Tunaimbiwa wimbo mzuri (waziri mkubwa) kuwa kuna bodi ya mishahara itamaliza tofauti na kibaya zaidi Mkuu kashasema hata yeye mshahara haumtoshi. Sasa kama wa 9mil haumtoshi pamoja na subsidy zote je Sisi wa 350K utatushea wapi minus subsidy?

Wakulima na Sisi walimu nadhani ni wahanga kuntu wa hii awamu!!!
 
Wakati mwingine watanzania tunalalama mno yaani kama watoto wadogo wanadeka kwa mama. Nyanya si muhimu sana katika mlo tafuta mbadala mwingine hio sio staple food.

Kwani huoni mvua kubwa zilizonyesha hapa Kati? Hizo ndio zimesababisha nyanya kufa mashambani. Mwaka huu zimekuwa zaidi ya wastani. Ni janga la asili acha kulalamika serikalini kila wakati haisaidii chochote.

Kingine muda si mrefu nyanya itashuka bei na nyanya zitajazana sana hapo masoko ya dar huku mkulima akiuza kwa 4000 tenga la debe tatu. Ni suala la muda mfupi tu mambo yatarudi kama kawaida.
 
Ukiona hivyo ndiyo ujue uchumi wa kati unaochagizwa na viwanda unakaribia kufikiwa.
 
Hayo ndio maendeleo yenyewe hayo tembea kifua mbele acha kulalamika mpiga dili wewe
 
balimar,
shkamo teacher.

siamini kama kuna mkulima ana maisha mazuri sasa kwa nyanya kuuzwa shilingi 500 kwa kipande. kama yupo nioneshe mmoja.

suala ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei.

elewa kwamba vitu vinaweza kuuzwa bei ya chini na bado wazalishaji na walaji wakanufaika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…