Hatari, nyanya moja shilingi 500

We unadhani kuna umuhimu gani wa kuweka waziri wakilimo, afsa kilimo wa kijiji nk, wizara nzima kazi yao ni nini kama siyo kuhakikisha kuna efficiency and continuous utilization of resources thought a year

Usilete utoto hapa, kusindika hizo nyanya kipindi cha msimu wake ili kipindi cha scarcity hizo nyanya ziwepo stock ni jukumu la serikali,

Kulima nyanya kuna ugumu gani kukiwa and available fund?, watu wanalima nyanya jangwani huko na wanapata supplus ya kuuza hata nje ya nchi,


Tukubaliane hapa kwamba serikali inafeli kufanya mikakati ya muda mrefu, maana kipindi cha msimu wa nyanya watu waliletq nyuzi hapa kuwa mbuzi na ngombe ndio zinakula nyanya huko shambani zisiendelee kuharibika


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kama unga ni ghali nunueni mchele" kwa sauti ya HBashe. "If bred is expensive try a Cake" kwa sauti ya Mke wa Mfalme Luois of XVI (France).... Kama nyanya ni "ghali nunua tomato source" kuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa uchumi...japo kuwa serikali imekuwa ikijinasibu kuwa inaboresha mazingira ya ki uchumi kwa kila Mtanzania ...SIKWELI... Juzijuzi tumeshuhudia mh Rais anasema serikali haiwezi kumuingilia mkulima na kumpangia bei kwa mazao yake...hili ni jambo jema sana tena sana kama ingekuwa hivi....lakini hii kauli haisadifu uhalisia wa mkulima kujipangia bei, wakulima bado wanapangiwa bei...serikali yaweza kuwa ina nia njema lakini ni ukweli kuwa mkulima anayefaidi haya si yule mlengwa wa kule kijijini wa jembe la mkono...hizi kauli zinazidi kuwaneemesha wachuuzi na walanguzi wakubwa pamoja na madalali walioko katikati huku mlaji wa kawaida na mzalishaji wa kwanza wakiendelea kuugulia maumivu..... Serikali ije na majibu ya kupata ufumbuzi wa mfumuko wa bei uliojitokeza hasa miezi ya hivi karibu hasa kwa bidhaa muhiu kwa watu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka mwaka 2016,2017 nyanya zikikosa bei na kumwagwa hovyo.Hivyo sasa kuwa bei juu ni muda wa kufidia hasara walizopata miaka 3 mfululizo.Tuache sok liamue.
 
Babu hakuna mfumuko wa Bei nyanya kipind Cha mvua na kumbuka nyanya haihimili mvua kabisa na zikiwa chache lazima zipande sababu wauzaji huzifuata mbali kumbuka Kuna usafiri,Kodi, na Bei ya kununulia mpaka ifike sokoni

Kuna wanaonunua kwa jumla na reja reja ambao wanaenda kuuza nyanya moja 300-500 vitu vingne Ni akil ndogo tu ya kufikiria

kilicho akilini kitumie
 
Nyanya kupanda bei kidogo tu mnalia lia kwani mmekatazwa kulima ili na nyinyi muuze mia 500?
Nchi hii ina maskini wa fikra na si kipato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha wakulima wauze nyanya1 hata kwa 1000 wanufaike na jasho lao
 
duh bora sisi tunaokula chukuchuku miaka yote
 
Mabeberu wanazidi kubana mbupu za watz wanyonge
 
madege yetu nayo ukipita pale karibu na airport yapo yamepaki tu kama ng’ombe wapo zizini.
Hahaah,kwa nini wasiruhusu tupike nayo selfie ili vizazi vijavyo wajue tuliishi peponi mkuu
 
Watetezi wa serikali kwenye uzi huu wanajidai kutoona sehemu hii:


"sijajuwa bado kama nchi imewekewa vikwazo au serikali iliyopo imefeli kusimamia uchumi wa nchi. miradi mikubwa inayotafuna pesa za walipakodi nayo ujenzi wake kuna suasua. pita pale gold star dar es salaam uone. hakuna kitu mtu wangu kuna manondonondo tu na nyenzo nyenzo kama vile kuna kazi lakini kiuhalisia hakuna kazi inayofanyika."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…