Hatari ya kuongezeka kwa mawazo ya kijamaa, hatamu za kiuchumi kushikiliwa na serikali

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
UPUNGUFU WA SUKARI NCHINI TANZANIA, RAIS WA ARGENTINA ATOA SOMO KWA SERIKALI

Rais Javier Milei wa Argentina atoa hotuba murua na kutoa tahadhari ya Hatari ya kuongezeka kwa mawazo ya kijamaa, hatamu za kiuchumi kushikiliwa na serikali

View: https://m.youtube.com/watch?v=cjONc43KsEo&pp=ygUZSmF2aWVyIE1pbGVpIENQQUMgc3BlZWNoIA%3D%3D Uhuru na Maendeleo ya Watu! (Makofi)! Kwanza kabisa, nashukuru sana kwa mwaliko huu. Kuhusu mkutano wa leo na athari zake, hapo awali nilizungumza huko Davos ambapo nilisisitiza. hatari ambayo nchi za Magharibi (na hata Tanzania) inakabiliana nazo kutokana na kuongezeka kwa mawazo ya kijamaa, nguzo na hatamu za kiuchumi kushikiliwa na serikali. Leo, nitaangazia misingi ya kiufundi ambayo ilisimamia mitazamo ya kisiasa niliyoshiriki katika mkutano huo.

Nitajadili jinsi uchumi wa mamboleo na mtazamo wake juu ya kufeli kwa soko unavyowezesha mawaza ya kiujamaa, hatimaye kukwamisha ukuaji wa uchumi na mapambano dhidi ya umaskini.


Kiini cha suala hili kiko katika mgongano wa kimbinu kati ya modeli ya mawazo ya kinadharia na matukio yanayotokea ulimwengu katika uhalisia.

Kwa ujumla, modeli inaposhindwa kuendana na hali halisi, tunarekebisha au kutupa kielelezo cha modeli. Hata hivyo, katika mfumo wa uchumi mamboleo, kunapokuwa na tofauti, huwa wanalaumu 'ukweli' kwa kusababisha 'kufeli kwa soko.'

Hii inatokana na kukaririshwa somo la uchumi tulilosoma vyuoni kuhusu mizania ya vipengele vya kawaida vya usawa wa ushindani - uwepo bidhaa , upekee wa bidhaa , na kila kitu kuwa sawa yaani utulivu.

Tatizo linatokea kwa uchambuzi wa kawaida kupitia uchambuzi wa fomula ya Pareto. Kwamba Ubora wa formula ya mizania ya Pareto unapendekeza kuwa kuboresha hali ya mtu bila kuzidisha hali ya mwingine ni uboreshaji wa Pareto.

Fursa hizi zinapoisha, tunafikia kiwango bora cha Pareto, na hivyo kusababisha ufafanuzi wa 'kufeli kwa soko' - ushirika usio leta mabadiliko, athari za kutoka nje, bidhaa za umma, tofauti za taarifa , na ile hali inayoitwa Wafungwa kulaumiana kwa sababu ya kutopeana ushirikiano. Fasiri hizi zote huwezesha ushawishi wa uingiliaji kati wa serikali na kuendekeza ajenda za serikali kushika nguzo za kiuchumi na ujamaa


Ili kufafanua hili kwa lugha nyepesi , fikiria enzi za mpito karne ya miaka ya 1800 kutoka kutumia mishumaa hadi balbu za taa ya umeme ili tupate mwanga. Ikiwa serikali husika miaka hiyo wangefuata njia ya kuingilia kati kuokoa viwanda vya uzalishaji mishumaa kufilisika pia ajira kupotea, basi leo hii mwaka 2024 bado tungekuwa tunatumia mishumaa badala ya kufurahia mwanga wa kisasa wa balbu za umeme.

Hivi ndivyo ujamaa unavyoweza kuathiri maisha yetu. Tunahitaji kusonga mbele zaidi ya kiwango bora cha Pareto kinachoamini katika mizania ya usawa, na kukumbatia maendeleo.

Soko liangaliwe kama ni mchakato wa ushirikiano wa kijamii ambapo haki za mali hubadilishwa kwa hiari. Kwa kuwa ubadilishanaji ni wa hiari, dhana ya 'kushindwa kwa soko' / market failrure inakuwa haina maana.

Misingi ya soko ni pamoja na mali ya kibinafsi na uingiliaji mdogo wa serikali. Mfumo wa bei, unaotokana na ubadilishanaji huu, hufanya kazi kama kisambaza habari na utaratibu wa kuratibu.

Mali ya kibinafsi na soko huria hurahisisha hesabu za kiuchumi, kufichua uwezekano wa ujamaa. Ujamaa unakosa mali binafsi na taratibu za soko, hivyo kusababisha uzembe na upotoshaji.

Ushindani, si kwa maana ya kisasa ya ushindani kamili, lakini kama kuingia na kutoka bila malipo, ni muhimu.

Dhana ya mchumi nguli Adam Smith ya mgawanyo wa kazi na ushirikiano wa kijamii inasisitiza kutofaulu kwa mawazo ya ujamaa. Smith alionyesha jinsi kazi maalum huongeza tija kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, bila mahitaji, mgawanyiko wa kazi hauwezi kutekelezwa kikamilifu. Licha ya tofauti zozote za kibinafsi, washiriki wa soko lazima washirikiane, kukuza amani na kudhoofisha ujamaa.

Wafanyabiashara waliofaulu katika mfumo wa kibepari hunufaisha jamii kwa kutoa bidhaa bora kwa bei bora, kuunda nafasi za kazi, na kukuza maendeleo. Wajasiriamali ndio nguzo ya mafanikio.

Sasa, hebu tushughulikie mtanziko wa uchumi mamboleo ndani ya nadharia ya ukuaji wa uchumi. Takwimu za kihistoria zinaonyesha kuwa kutoka enzi ya Ukristo hadi 1800, Pato la Taifa kwa kila mtu libaki bila kukua .

Walakini, kuanzia miaka ya 1800 na kuendelea, iliongezeka zaidi ya mara 15, na idadi ya watu ulimwenguni iliongezeka kutoka milioni 800 hadi bilioni 10. Kipindi hiki pia kilishuhudia kupungua kwa umaskini uliokithiri, kutoka 99% hadi 5%.

Nadharia ya za kiuchumi mamboleo yaani Neoclassical inakosoa ukiritimba, lakini kipindi hiki cha miundo ya ukiritimba kilileta ustawi mkubwa na kupunguza umaskini.

Uchambuzi wa wana uchumi mamboleo una dosari kwa sababu hurahisisha kupita kiasi na kushindwa kuzingatia athari za siku zijazo na uchumi mzima.
Ukiritimba, kulingana na nadharia ya neoclassical, huzalisha kidogo na malipo zaidi.

Walakini, faida ya ukiritimba inaweza kuchochea matumizi, uzalishaji, na ajira katika sekta zingine. Kuokoa faida hizi husababisha uwekezaji na ukuaji.

Hata kama ukiritimba anajilimbikizia mali, hupunguza usambazaji wa pesa, kupunguza bei na kunufaisha idadi ya watu.
Uingiliaji kati wa serikali kwa jina la haki ya kijamii, demokrasia isiyo na kikomo, na kujitafutia umaarufu yaani populism mara nyingi hudhuru uchumi.

Nchi kama vile Argentina, zilizowahi kuwa miongoni mwa nchi tajiri zaidi duniani, zimeanguka kwa kiasi kikubwa kutokana na miongozo/ kanuni nyingi na kuingiliwa na serikali.

Ubepari, kinyume na shutuma za ubinafsi wa kupindukia, sio tu kwamba una tija zaidi bali pia ni wa haki. Soko, kama mchakato wa ugunduzi, hutengeneza utajiri wakati wa uzalishaji. Wale wanaogundua au kuunda thamani mpya wanaimiliki kwa njia halali ...



NeoClassical theory The Pareto Principle is very simple, yet very important. It is named after Italian economist Vilfredo Pareto, who, in 1906, found that 80% of the land in Italy was owned by 20% of the population.

What was most important about Pareto’s finding was that this 80/20 distribution occurs extremely frequently. For example, in general, 20% of your customers represent 80% of your sales. And 20% of your time produces 80% of your results. And so on.
 
22 February 2024

Tanzania kudhibiti wafanyabiashara wa sukari , pia kutoa bei elekezi​



View: https://m.youtube.com/watch?v=k7NvY15w-9Y
BASHE ATOA KAULI NZITO SAKATA la SUKARI - ''WAFANYABIASHARA 28 TUMEWAKAMATA - TUMESHAWABEBA SANA''...

Waziri wa Kilimo Tanzania Hussein Bashe amesema wameazimia kukomesha uwepo wa walanguzi ambao, kwa miaka mingi wametawala soko la sukari. Video.

Serikali ya Tanzania imesema itaifungua biashara ya sukari kwa lengo la kuongeza ushindani na kuondoa wafanyabiashara wachache wenye mazoea ya kuhodhi bidhaa hiyo.

Hatua inakuja wakati serikali ya nchi hiyo inatarajia kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara 84 kwa tuhuma za ulanguzi wa sukari wa bidhaa hiyo ambayo imekuwa adimu nchini Tanzania.

Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Hussein Bashe amesema wameazimia kukomesha uwepo wa watu wa namna hiyo ambao, kwa miaka mingi wametawala soko la Sukari.

"Kuna baadhi ya wauzaji wamekuwa na tabia ya kuficha bidhaa hiyo ili kuongeza bei, atanunua kwa shilingi 2,800 na kuwauzia watu kwa shilingi 4,000 kwa kilo," amesema Bashe, wakati akijibu maswali ya wanahabari katika Ikulu ya Tanzania, mjini Dar es Salaam.

Kulingana na waziri Bashe, wafanyabiashara 84 wameshakamatwa katika operesheni maalumu inayolenga kuwaondoa watu wenye tabia ya kuhodhi bidhaa hiyo.

Katika hatua nyingine, waziri Bashe amesema Tanzania itaendelea kuagiza Sukari kutoka nje ya nchi mpaka mwisho wa mwaka 2024.

Waziri huyo amebainisha kuwa Tanzania ina mpango wa kuagiza zaidi ya ya tani 300,000 kupitia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).

"Kama sio mabadiliko ya tabia nchi, Tanzania isingekuwa inapitia changamoto hii," amesema.

Hata hivyo, waziri Bashe aliwahakikishia Watanzania kuwa hali ya upatikanaji wa sukari itatengemaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Tanzania ina jumla ya viwanda saba vya sukari, vikubwa kati ya hivyo ni Kilombero, ambayo kwa siku inazalisha tani 700 za sukari, hata hivyo kiwango kimeshuka hadi 250, TPC kwa siku tani 450 lakini kwa sasa kimesimamisha uzalishaji kutoka na hitilafu za mashine, huku Kagera Sugar ikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 500 kwa siku, lakini sasa inazalisha wastani wa tani 200 hadi 300. Viwanda vyengine ni Mtibwa na Bagamoyo, ambapo kwa mujibu wa serikali, kutokana na mvua kubwa za el Niño zinazoendelea
 
Rais Javier Milei wa Argentina ni mchumi kitaaluma elimu ya chuo kikuu na mchambuzi wa mifumo ya kiuchumi.

Hotuba yake inabidi ibaki hapa jukwaa la siasa, ili wanasiasa wa Tanzania waachane na elimu waliyokaririshwa chuo kikuu na vyuo vya elimu ya juu kuhusu somo la uchumi.

Wananchi wanatazama uchumi na upungufu wa sukari kama atazamavyo rais Javier Milei na kuuliza maswali mengi ambayo wachumi mawaziri wetu wa Kilimo na Fedha / Uchumi wameshindwa kuyajibu na kuyapatia dawa yasijirudie tena na tena iwe sukari, soko la korosho, soko la mahindi ya wakulima lisilo na vizuizi vya mpaka n.k

Wamebaki kujitafutia umaarufu yaani populism na mara nyingi hudhuru uchumi.
 
January 2024
Mikono yao Mingi ya Udhibiti wa Tasnia ya Sukari katika Ujamaa

View: https://m.youtube.com/watch?v=4V8nfLzWDBo&pp=ygUPUHJvZmVzYSBiZW5nZXNp
Bodi ya Sukari ni taasisi ya umma iliyoanzishwa na serikali mnamo mwaka 2001 majukumu yake makubwa ni udhibiti wa tasnia ya sukari kulinda wadau ambao ni wazalishaji ambao pia waagizaji , walaji, mabenki kwa ajili ya mitaji na wakulima wadogo asema profesa Kenneth Michael Kitundu Bengesi.

Sikiliza mahojiano marefu ya tasnia hii moja ya sukari

Prof. Kenneth Bengesi afafanua kuhusu changamoto ya upatikanaji wa sukari nchini
Profesa aja na nadharia, takwimu pia habari za ndani na kujibu maswali kibao ya waandishi wa habari ambayo yanafanana na ya wananchi. Kuwa kwanini mbali ya taarifa za mamlaka za hali ya hewa nchini TMA, mikutano ya Bodi ya Sukari na wadau wa sekta hiyo bado serikali imeshindwa kuweka mazingira ya uwepo wa sukari nyingi ili bei pia iwe himilivu huku kukiwa hakuna upungufu ....


TOKA MAKTABA
2022 25 October

PROF. KENNETH BENGESI - KWA MUJIBU WA ILANI YA CCM, UPUNGUFU WA SUKARI KUWA HISTORIA 2025



View: https://m.youtube.com/watch?v=-vJPSeZJKzsUanzishwaji wa viwanda vipya vya kuzalisha sukari na kupanua uzalishaji kwa viwanda vilivyopo utawezesha nchi kuzalisha tani 756,000 ifikapo mwaka 2025.

Na hivyo kuondokana na upungufu wa sukari unaoilazimu Serikali kutumia zaidi ya Bilioni 300 kila mwaka. Miongoni mwa viwanda vinavyotarajiwa kumaliza tatizo la upungufu wa sukari nchini ni kiwanda cha Bagamoyo Sugar kinachomilikiwa na kampuni za Said Salim Bakhresa.
 
Yesu alikuwa mjamaa na mtume Muhammad alikuwa mjamaa. Mawazo ya kijamaa hayajawahi, na hayawezi kuwa hatari.

Shetani anatumia nguvu sana kuwaaminisha hivyo.
 
Kwenye Sukari lengo ni kulinda Viwanda vya Ndani hata kama Viwanda hivyo havitoshelezi.
 
Kwenye Sukari lengo ni kulinda Viwanda vya Ndani hata kama Viwanda hivyo havitoshelezi.

Ndiyo hatari ya ujamaa kwa serikali kubeba viwanda hivyo 7 vya ndani huku mchumi rais Javier Milei anasema, mbeleko hiyo inaficha mapungufu siyo tu ya viwanda bali na sera za nchi.

Rais Javier Milei anataka mapungufu hayo yafanyiwe kazi na viwanda badala ya kufichwa. Mfano viwanda hivyo vingekuwa na ufanisi mkubwa vingezalisha sukari tani milioni 1.2 na kukidhi mahitaji ya tani 600,000 kwa mwaka ya nchi huku akiba ghalani ikiwepo tani 600,000 inayoweza kukabiliana na mvua za msimu wa el Niño na isipokuwepo El Niño sukari ya ziada kuuzwa nje.

Ujamaa huu wa serikali na viwanda 7 dhaifu ndiyo tatizo la sukari nchini na linatiwa ulemavu kwa kutoa bei elekezi kwa sukari inayozalishwa viwanda vya ndani.

Rais Milei anatetea hoja yake kuwa uzalishaji wa ufanisi viwandani na bei isiyo elekezi anayokubali kutoa mnunuzi kwa hiyari ndiyo mzania mzuri na hakikisho la uwepo wa sukari bila upungufu huku pia viwanda vya ndani vikizidi kupanuka na kuzalisha kwa wingi.

Badala ya serikali kutoa vibali kwa viwanda vya uzalishaji sukari nchini viagize sukari iliyoshindwa kuzalisha kutoka nje huo ni ujamaa wa hatari ambao serikali inafanya kwa sasa katika sekta ya sukari.
 

Uhaba wa sukari, Serikali yatoa vibali kwa wenye Viwanda vya Sukari Nchini kuagiza nje kutoka nje​


Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari nchini, Profesa Kenneth Bengesi amesema kuwa Serikali imetoa vibali kwa viwanda vya sukari kuagiza sukari tani 50,000 kutoka nje ya nchi ili kukabiliana na uhaba wa bidhaa hiyo ambapo itaanza kuwasili mwezi huu.

Kwa sasa Sukari imekuwa adimu nchini na imesababisha kupanda bei na kufikia kati ya TSh 3,200 mpaka TSh 4,000 kutoka TSh 2,500 hadi Tsh 3,200.
Upungufu wa sukari umetokana na upungufu wa bidhaa hiyo kwenye maghala kulikosababishwa na viwanda kusimamisha uzalishaji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Profesa Kenneth M K. Bengesi amesema baada ya viwanda kusimama uzalishaji, sukari iliyokuwa inatumika ni iliyozalishwa mwezi Mei 2023 na hivyo kusimama kwa uzalishaji kulimaanisha sukari iliyokuwepo kwenye maghala kupungua kwa kiasi kikubwa hali iliyofanya wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia mwanya huo kupandisha bei.

Naye waziri Hussein Bashe
alisema wenye viwanda saba vya uzalishaji wa sukari ambavyo vinalindwa na serikali ndio maana wamekuwa wakiwaambia kuwa ni lazima waheshimi nafasi wanayopewa na serikali.

Alibainisha kuwa hali ya upungufu wa sukari nchi ulishawahi kutokea Mwaka 2018 hadi 2019 na serikali ilichukua hatua hizo hizo ili kukabiliana na changamoto hiyo.
 
Serikali ya Ujamaa inayoendeshwa n wafanya biashara
 
Tatizo si ujamaa, tatizo ni serikali kuendeshwa na wafanyabiashara.

Sera za siasa za ujamaa ambapo wachache wanafanya maamuzi wakidai kwa ajili ya wanyonge wengi.

Wakati biashara na wafanyabiashara na wale waliopo ktk soko kwa hiyari yao wenyewe ni wengi kuliko watoa maamuzi waliopo katika serikali ya kijamaa.
 
Sera za siasa za ujamaa ambapo wachache wanafanya maamuzi wakidai kwa ajili ya wanyonge wengi.

Wakati biashara na wafanyabiashara na wale waliopo ktk soko kwa hiyari yao wenyewe ni wengi kuliko watoa maamuzi waliopo katika serikali ya kijamaa.
Serikali kuyalinda hayo makampuni ya wafanyabiashara wa sukari wasiolipa hata kodi stahiki ndio ujamaa?!
 
Serikali kuyalinda hayo makampuni ya wafanyabiashara wa sukari wasiolipa hata kodi stahiki ndio ujamaa?!

Ndiyo ujamaa wa CCM kukumbatia petite bourgeoisie / mabepari (mabilionea) uchwara wa CCM.

Hawa wenye viwanda vya kuzalisha sukari Tanzania na hapo hapo wanapewa vibali vya kuagiza sukari nje ni wafanyabiashara uchwara wakubwa, wamegeuka kuwa machinga badala ya kuzalisha bidhaa ya sukari hivyo ni mabepari uchwara waliotengenezwa na CCM ...

TOKA MAKTABA:

Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ... - Wizara ya Kilimo
"Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli maelekezo yako ya kutengeneza mabilionea kupitia kilimo yatawezekana kupitia viwanda ...
 
Shida ni mabepari kuwa wahuni na kufanya watu wengine wote ni mambwa.

Uonevu umedhidi dunianina hakuna mtetezi zaidi ya watu kutuambia ubepari ndio ulivyo.
 
Mambo ya pareto efficient and optimal hayo.Wachumi wenzangu wataelewa.

But ukweli ni kwamba Ujamaa Huwa ni upumbavu tuu ambao Huwa unatafuta suluhisho la Zima moto bila kujali athari zake mda mrefu ujao.

Na mfumo wa kijamaa Kwa sehemu kubwa unanufaisha Wanasiasa na kuharibu welfare ya jamii Kwa sehemu kubwa lakini in short run Huwa unafariji maskini ndio sababu umejengwa kwenye msingi wa propaganda na vitisho.

Leo hii ukiona hao wanayodai.kuandamnaa maisha magumu hawaelewi wanasimamia sera zipi za Uchumi ingawa wanapoenda kwenye maandamano wanadhani labda watakuwa wanapata vitu Bure bila kujiuliza vitatoka wapi hivyo vya Bure,wanakimbia ukweli kwamba bila kwenda Kuzalisha maandamano Yao na wanachodai hawatakaa wapate sana sana watatumiwa na Wanasiasa matapeli Ili kushika hatamu.Inakuwa kama mambo ya makanisani.
 
Yaani mtu timamu ana msikiliza Milei kuna tatizo kwenye ubongo sio bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…