- Thread starter
- #21
24 February 2024
Mwanza, Tanzania
CPA AMOS MAKALLA KATIKA KIKAO KIZITO NA WAFANYABISHARA WA SUKARI MKOANI MWANZA
View: https://m.youtube.com/watch?v=m2KFLB1Rfxk
Mkuu wa mkoa CPA Amos Makalla asikiliza hali ngumu ya sukari kutoka kwa wasafirishaji, wagavi na wenye maghala.
Amos Makalla serikali imetoa kibali na mkoa wa Mwanza umepojea tani 255 ingawa bado kuna foleni kubwa kwa SHAH muuzaji maarufu wa mjini Mwanza ...
CPA Amos Makalla asema bei elekezi ya Serikali Jumla ni shs 2650 hadi 2800 na rejareja ni shs. 2800 hadi Shs. 3000
Awahimiza Wakuu wa Wilaya na Maafisa Biashara kushirikiana kufuatilia bei sahihi. Aahidi kufuatilia bei ya Sukari wakati wa ziara yake Majimboni kuanzia Machi 2024 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Makalla leo Februari 26, 2024 wakati akiwa na kikao kizito kilichojumuisha wakuu wa wilaya, wafanyabiashara na wasambazaji wa sukari mkoani humo na kutangaza rasmi ujio wa tani 254.5 wa bidhaa hiyo na kusisitiza uzingatiaji wa bei elekezi ya Serikali.
Akizungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa, CPA Makalla amesema kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali bei ya Jumla itakuwa Tshs 2650 hadi 2800 na Rejareja ni Tshs 2800 hadi 3000 na kusisitiza bei hiyo itaendelea hadi viwanda vya sukari nchini vitakapo rejea katika uzalishaji wao wa kawaida.
CPA Makalla akaongeza kwa kusema "Ndugu zangu nimewaita hapa wote tunafahamu upungufu wa sukari uliojitokeza nchini kwetu, Serikali imetoa tangazo namba 40 b ya amri ya bei elekezi ya sukari naomba sana tuzingatie hilo ili kuwaondolea usumbufu wananchi wetu", amesisitiza CPA Makalla wakati akizungumza na wadau hao wa sukari.
Aidha, amewataka Wakuu wa Wilaya na Maafisa biashara kushirikiana kufuatilia usahihi wa bei ya sukari kwa muda wote ambao bidhaa hiyo itakuwa inauzwa dukani."Kuanzia Machi 4, 2024 nitaanza ziara ya kusikiliza kero za wananchi Majimboni na kipaumbele cha kwanza nitawauliza wananchi sukari wananunua kwa bei gani nikisikia tofauti nitajua viongozi hamkutimiza wajibu wenu."
"Tunashukuru kwa uamuzi huu wa Serikali wa kutoa vibali kwa wafanyabiashara kuagiza kutoka nje, hii inatupa unafuu sisi wafanyabiashara kuepuka malalamiko kutoka kwa walaji," Joyce Maduhu, msambazaji wa sukari.
Hivi karibuni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alitoa maelekezo kwa Wakuu wote wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia bei elekezi ya Sukari baada ya bidhaa hiyo nyeti kupanda bei sana kutokana na upatikanaji wake kuwa mdogo na mahitaji kuwa makubwa
Source : MWANZA RS TV

RC MAKALLA: MWANZA TUMEPOKEA SUKARI TANI 255