PostGE2025 Hatari ya kushitakiwa ICC: Waliogiza raia wauawe ovyo ovyo, watarudia kosa hilo Desemba 9 ?

PostGE2025 Hatari ya kushitakiwa ICC: Waliogiza raia wauawe ovyo ovyo, watarudia kosa hilo Desemba 9 ?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Hili ndio swali ambalo binafsi najiuliza hasa ikitokea raia wanaandama kwa wingi na kwa amani huku media za kimataifa zikiwa zinafuatilia kwa karibu (zinakusanya ushahidi) kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia picha za satellite .

Mtazamo wangu:

Kwasababu limeshafanyika kosa na kuna juhudi za kutaka watuhumiwa wafikishwe kwenye mahakama ya ICC, kuna uwezekano mkubwa wenye kutoa maagizo safari hii wakaea wazito na pengine kuacha askari waungane na raia kwenye maandamano.

Mbali na tishio la kushitakiwa. ICC, vyombo vya dola katika mataifa yaliyokumbwa na maandamano huangqlia public opinion ikoje na wakiona kiongozi hakubaliki, basi hujitenga nae dakika za mwisho kwa maana ya kumgeuka na kumtaka aondoke madarakani.

Njia pekee ya kuokoa mtawala anaepingwa na wananchi ni kuhakikisha maandamano hayafanyika kabisa kwa maana ya kuyazuia yssitokee au kwa kutangaza hali ya hatari.

Je, watafanya hivyo?

Kama ndio, kwa muda gani?

Kiuchumi, tutabaki salama iwapo curfew itakuwa ni kwa muda usijulikana?
 
ndiyo, wataua tena wakipewa nafasi, these people are psychopaths, power kwao ni kila kitu na watafanya kila waliwezalo hata kama ni kuchoma nchi yote kama wakipewa nafasi watafanya, Biblia imeongelea haya mambo yote, existence of evil.

punchline, mjueni adueni yenu, mnadili na psychopaths, kama waliweza ku shoot indiscriminately namna ile bila ya huruma yoyote na wala kujali risasi ilimpata nani na yupi walishavuka mipaka yote ya ubinadamu hata wakoloni hawakufanya hivyo, kuzima uprising walikuwa (wakoloni) wanashoot waliokuwa na silaha au askari wa jadi waliokuwa na silaha za jadi na siyo watoto wadogo, vijana, walemavu au yoyote yule anayeonekna kama anakwenda dukani au kumpeleka mtoto mdogo hospitali hakuna tofauti wote bullet na ujue sababu za wao kufanya vile ni kuleta hofu na uoga kwa watu kwa kuuwa wengi.

tunadili na evil, na knowledge of evil ni muhimu moving forward ...
 
Nahisi ni muhimu kilichotokea kikatokea tena ili watu wapate kujifunza zaidi.

ICC haiwezi kufanyakazi kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa kwa njia fulani fulani, hivyo sio mwarobaini

Vile vile ushirika wa mataifa fulani fulani ni njia ya matumaini na kikwazo kwa ICC na kura ya turufu pale UN.
 
Hivi kwa mfano ;
watu wakatoka na wasifanye vurugu! Wakandamana kwa amani na polisi wakawalinda!
Hayo maandamano yatakua na destination?
-Je ikifika saa 12 waandamanaji watarejea majumbani au watalala hapo mpaka siku watayosikilizwa kwa uvumilivu hata ikawa wiki2?
- ama ndio wataaanza vurugu mpya
 
Kuna kisa kimojq kilitokea siku chache zilizopita pale Brazil ktk mkutano mkubwa wa viongozi wa kidunia

Watu wengi walipoteza maisha ktk maandamano yale ya amani.

Maandamano yalikuwa ya amani lakini watu waliuliwa pale pale na hakukuwa na kuzimwa kwa mtandao. Dunia iliona na ilikaa kimya na hakuna tamko lolote la maana.
 
Wahalifu watauwawa kila siku siyo hiyo tarehe tu ukitaka hata leo toka ukaharibu mali na kuiba uone kama utabaki
 
Kuna kisa kimojq kilitokea siku chache zilizopita pale Brazil ktk mkutano mkubwa wa viongozi wa kidunia

Watu wengi walipoteza maisha ktk maandamano yale ya amani.

Maandamano yalikuwa ya amani lakini watu waliuliwa pale pale na hakukuwa na kuzimwa kwa mtandao. Dunia iliona na ilikaa kimya na hakuna tamko lolote la maana.
kwa hiyo unamaanisha na huku watafanya hivyo hivyo!? Uzuri wanaozika ndugu wamo wana CCM, Waislamu! na wapo ndugu wa waliopo Serikalini!

Nchi hasara sana hii kwa kweli Mungu arande woote waliotusababisha shida hii
 
Sijui kama wataepuka kushitakiwa ICC wakirudia hilo kosa
Kwamba sasa hivi ICC haiwezi kuwashtaki mpaka warudie kosa?

Na kwanini huwa tunadhani ICC ua wazungu wanajali sana tukiumia, ukweli hawajali tena wakati mwingine wanachochea kusiwe na utulivu ili wavune vya kutosha, mifano ipo.
 
Mhh! Mi ningekuwa samuya ningekuwa nimeshajiuzulu zamani
 
kwa hiyo unamaanisha na huku watafanya hivyo hivyo!? Uzuri wanaozika ndugu wamo wana CCM, Waislamu! na wapo ndugu wa waliopo Serikalini!

Nchi hasara sana hii kwa kweli Mungu arande woote waliotusababisha shida hii
Kila mtu atawajibika kwa makosa yake bila kujali upande, rangi, dini, umri, kimo, chama nk.

Tutaendelea kuwazika. Ni jukumu letu kuwastili marehemu bila kujali ni mtoto, mkubwa, dini yake, chama chake nk
 
Hata wakirudia jambo la msingi hakuna wa kurudi nyuma!
Ni vizuri zaidi, huku vijijini tutaendelea kutenga maeneo makubwa zaidi kwa ajili ya kupanda miili ya watu na sio mbegu kipindi hiki cha kilimo

Walizikwa babu zetu maelfu kwa maelfu na bado watawala waliendelea mbele bila kujali ukatili walioufanya mpaka kesho.
 
Kuna kisa kimojq kilitokea siku chache zilizopita pale Brazil ktk mkutano mkubwa wa viongozi wa kidunia

Watu wengi walipoteza maisha ktk maandamano yale ya amani.

Maandamano yalikuwa ya amani lakini watu waliuliwa pale pale na hakukuwa na kuzimwa kwa mtandao. Dunia iliona na ilikaa kimya na hakuna tamko lolote la maana.
Serekali ya dunia huwa ina maslahi yake na ukionyesha kutishia maslahi yao wanafanya chochote na wanakaa kimya. Hizi kesi za nyani ngumu kumpelekea ngedere labda wawe hawana maslahi nae
 
Kwamba sasa hivi ICC haiwezi kuwashtaki mpaka warudie kosa?

Na kwanini huwa tunadhani ICC ua wazungu wanajali sana tukiumia, ukweli hawajali tena wakati mwingine wanachochea kusiwe na utulivu ili wavune vya kutosha, mifano ipo.
Bongo watu wanaangamia kwa kukosa maarifa na utafiti😅😅😅🤣🤣
Kwa haya yanayoendelea nmegundua maarifa ni tunu na elimu haijamsaidia mtu.
 
Bongo watu wanaangamia kwa kukosa maarifa na utafiti😅😅😅🤣🤣
Kwa haya yanayoendelea nmegundua maarifa ni tunu na elimu haijamsaidia mtu.
Uko sahihi, mantiki inawekwa pembeni, hisia zinaongoza akili, matokeo yake ni kulia na kulalamika kwenye mambo ambayo yako wazi.
 
Back
Top Bottom