Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Kwa Saddam Hussein watu wa dunia ya tatu walinukuu hata misahafu wakidai safari hii Marekani kaingia choo cha kike na kwamba vita ambavyo vingetokea ni mother of all battles. Wako askari wa Saddam waliojuliakana kama Republican Guards ambao ilidaiwa wangewaonesha cha mtema kuni wanajeshi wa Marekani na kwamba jangwa lingegeuka jehanamu na kutiririka damu!
Saddam Hussein enzi zake akitamba!
Wako walioenda mbali zaidi na kutabiri mwisho wa dunia wakinukuu aya kwenye misahafu iliyotabiri kutokea mvaa kilemba wa mashariki ya Kati ambaye angeifuta Marekani kwenye uso wa dunia. Bila shaka vijana ambao hivi sasa wanamshabikia huyo mnyoa kiduku wa NK walikuwa bado kuzaliwa. Kwa kufupisha hadithi ndefu ni kwamba operation desert storm ilipotangazwa dunia ilisimama.
Saddam Hussein na kilemba.
Ghafla anga lote la Iraq likafunikwa kwa wingu jeusi la mawimbi ya redio na Warusi waliotabiriwa kumsaidia Sadam wakakunja mikia na kumuacha Saddam akicharazwa kama mtoto mdogo. Republican Guards wake wakasambaratika wakitafuta pa kujificha wasipaone. Marekani, kwa moyo wa huruma akasema imetosha, akamkanya na kumuonya asirudie na hivo kumuacha Saddam akikusanya vyake.
Miaka michache baadaye Saddam kwa ama utundu au ujinga akasahau akaanza tena chokochoko na safari hii Mmarekani akaapa kutomuonea tena huruma. Masikini Saddam, baada ya kukosa pa kukimbilia akaishia shimo la panya kujisetiri kuepuka vipondo. Lakini hata huko alitafutwa na siku anatolewa shimoni macho yalikuwa hayaoni baada ya kukaa gizani miaka yote hiyo.
Saddam Hussein akitolewa shimoni alikojificha!
Endeleeni kukidanganya hicho kitoto cha NK! Historia hujirudia...nyie vita muisikie tu ila mkae mkijua kwamba Marekani wako mazoezini miaka yote toka vita vikuu vya dunia vya pili.