YEHOVA
JF-Expert Member
- Sep 23, 2023
- 223
- 307
Mzee anaukabila sana ndio maana TISS hawamtaki kabisaZitto hata Mimi nakubaliana na wewe Kimei amedoda sana aisee,
Tumepoteza hiyo potential
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee anaukabila sana ndio maana TISS hawamtaki kabisaZitto hata Mimi nakubaliana na wewe Kimei amedoda sana aisee,
Tumepoteza hiyo potential
===
Historia imeandikwa katika Masoko ya Mitaji Afrika Mashariki leo baada ya Hati fungani ya NMB Jamii kukusanya Tsh Bilioni 400 ikiwa ni zaidi ya mara tatu ya lengo lililokusudiwa ambapo ni Tsh Bilioni 212.9 kwa fungu la shilingi za kitanzania na dola za kimarekani milioni 73 kwa fungu la dola.
Matokeo haya yametangazwa rasmi wakati wa hafla ya kuiorodhesha Hati Fungani ya NMB Jamii katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) mapema leo ambapo fedha zote zilizopatikana kupitia Hati Fungani ya Jamii zitaelekezwa katika kutoa mikopo nafuu kwenye miradi endelevu ikiwemo miradi ya nishati mbadala, miradi ya kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira, miradi ya maji, miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, miradi ya wanawake, vijana, elimu, afya, nyumba nafuu na mingine inayoendana na hiyo.
NMB Jamii Bond ilizinduliwa na kuanza kuuzwa Septemba 25 hadi Oktoba 27 mwaka huu ambapo Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna akizungumza leo amesema NMB Jamii Bond ilikuwa imegawanyika katika mafungu mawili, fungu la kwanza likihusisha shilingi za kitanzania na fungu la pili la dola za kimarekani ambako kote wamevuka lengo la makusanyo kwa kupata shilingi bilioni 212.9 kutoka bilioni 100 za lengo na upande wa dola wakikusanya milioni 73 badala ya milioni 15 walizolenga.
“Kwa mantiki hiyo, thamani ya jumla ya fedha zilizopatikana kutokana na NMB Jamii Bond ni Sh. Bilioni 400, ambazo ni mara tatu zaidi ya lengo tulilokuwa nalo” amebainisha Ruth Zaipuna huku akiwahakikishia Wateja zaidi ya 5,600 walionunua Hati Fungani hizo kuwa pesa zao ziko mikono salama.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa hafla hiyo aliipongeza NMB kwa kuweka rekodi ya bilioni 400 za mauzo ya Hati Fungani hiyo “Hati Fungani ni fursa muhimu kwa jamii kunufaika kwa njia mbili za kuweka akiba lakini pia kufanya uwekezaji wenye faida kubwa, bond ni mkopo ambao Taasisi ya fedha inakopa kwa Wananchi, NMB ingeweza kwenda kukopa BoT au Benki za nje lakini ikachagua kukopa kwa Wananchi kupitia mdhamana wao ambaye ni CMSA na inarejesha kwa riba kubwa ya asilimia 9.5”
Nunua Sasa Jamii Bond kuanzia TZS 500,000 upate mpaka 9.5%
Umesahau siasa ni si hasaMtampoteza sasa, why kila mtu aki perform lazima aingie siasa? Kimei is underperforming licha ya kushine CRDB..... huyu abaki huku huku ikiwezekana apelekwe BOT au CMSA sio political post.
Si hasi au si hasa?Umesahau siasa ni si hasa
Si hasa means sio uhalisiaSi hasi au si hasa?
Mkuu mambo yanaendaje? Vipi ushajiwekea bond zako tayari?Si hasa means sio uhalisia
CjaelewaMkuu mambo yanaendaje? Vipi ushajiwekea bond zako tayari?
Kimei angekua waziri was fedha ndio tungeiona potential yake practically!!Zitto hata Mimi nakubaliana na wewe Kimei amedoda sana aisee,
Tumepoteza hiyo potential
Nadhani awamu ya pili ya Uongozi wake anaweza kuwa waziriKimei angekua waziri was fedha ndio tungeiona potential yake practically!!
Nakubaliana na weweHuyu Mama angepewa tu na CRDB, NBC pamoja na TCB aziongoze maana naona wale Viongozi wanzungusha tu sketi
Huyu Mama ni balaaBinafsi namkubali sana Bi Ruth Zaipuna,
Huyu Mama ni wa mipango sana,
Hii program anayokuja nayo italinufaisha sana Taifa hili,
Nadhani kama Taifa lazima tuvilee hivi vipaji vinavyochipukia namna hii,
Sio mbaya na NBC wakaiga hili linalofanywa na mtoto wake