Hatia 4 - Dizasta vina ni best story teller tangu hiphop ya bongo ianze mpaka sasa

Hatia 4 - Dizasta vina ni best story teller tangu hiphop ya bongo ianze mpaka sasa

Ah sikua na zali sikuziamini ndumba, sikua na mali za kufuja.../

Nilijitahidi kuuza mitumba kufuga mipunga, ili siku nimpe gari nimpe nyumba.../

Nilishindwa niliishia kumpa chai, chipsi mayai na vocha, nywele za kimasai na mkoba.../

Pesa za magauni majuba na viatu vya kuzuga, ilimpa muda ila bado haikutosha..../

kwani nilipomwambia nampenda hakujibu, akaweka moyo wangu maumivu.../

Na mtima wangu akauweka solemba, nikaapia kuwa sitakuja kupenda forever.../

Ah nilimoa upendo nilimpa sifa, niliweka mitego ya faida..haikua shwari/

Nikabadili mwenendo wa maisha, slniliweka malengo sikutimiza...hakunikubali/

Alikua na ndoto kubwa kushinda mimi, alikua na misimamo kuipita dini.../

aliniambia ameomba nije kuokota utajiri, amengoja sana na sasa amechoka kusubiri.../
 
"john alifahamu hali ya jane, kuwa jane alizaliwa kwenye familia maskini na aliuchukia mno umaskini.

Alifahamu umaskini ulivyochukua uhai wa mama yake kipenzi aliyefariki jwa kukosa matibabu.

Alifahamu nadhiri aliyoiweka jane ya kwamba hatokubali tena kuishi kwenye maisha ya kimaskini, nadhiri iliyomweka john njia panda
 
Ah sikuwa na hali ya kuikosha roho yake, nilimuacha aende aufuate moyo wake.../

Alipata bwana wa kizungu magharibi, alimuahidi kuishi maisha ya ndoto zake.../

Nilipata uchungu niliishia kuhamaki nilitaka nijiue, nilitaka nimzuie abaki nikakumbuka ukioenda ua haulikati unaliacha likue.../

Duka langu nilifunga biashara niliacha zote, uchumi uliyumba kwa maana nilianza pombe.../

Niliumwa bado kidogo moyo uzime, nilimfanya ndoto yangu kumbe naye ana ndoto nyingine.../

Alisema anakwenda jiji la miami, hakuna alichowaza zaidi ya kuishi kifahari.../

Kamtumia picha na mchizi kazikubali, na yupo tayari kumipia gharama za safari.../

Aliondoka na kipande kimoja cha mwili, nilikonda nilipata ugonjwa wa akili.../

Haikuwahi kupita hata sekunde nisilie, nilitamani mpaka ardhi ipasuke niingie.../
 
Kuna movie ya Kiafrika imefanya vizuri Cannes.Inaitwa "Farewell Amor". Ya Ekwa Msangi.

Nilikuwa naiangalia siku moja kabla Dizasta hajatoa huu wimbo.

Movie ina maudhui yanafanana kidogo na wimbo, ingawa tofauti.

Dizasta akipata team nzuri na budget, script ya kutokana na huu wimbo inaweza kutoa movie nzuri zaidi ya "Farewell Amor".


Ngoja nitafute hiyo movie
 
Back
Top Bottom