Hatifungani ya Samia Kianzio Tsh 500000: Wale Mliotaka Kuwekeza Kwenye Hati Fungani (Bond) Hii Hapa Samia Infrastructure Bond Kianzio Tsh 500,000 Tu

Hatifungani ya Samia Kianzio Tsh 500000: Wale Mliotaka Kuwekeza Kwenye Hati Fungani (Bond) Hii Hapa Samia Infrastructure Bond Kianzio Tsh 500,000 Tu

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Wale Mliotaka Kuwekeza Kwenye Hati Fungani (Bond) Hii Hapa Samia Infrastructure Bond Kianzio Tsh 500,000 Tu

Kwa kuanza, unaweza kuwekeza kuanzia TZS 500,000 kwenye Samia Infrastructure Bond kwa muda wa miaka 5. Hii ni fursa maalum ya kufadhili miradi ya ujenzi wa miundombinu nchini, hususan barabara za vijijini na mijini kupitia TARURA. Bondi hii inalipa riba ya 12% kwa mwaka, inayolipwa kila miezi mitatu (mara 4 kwa mwaka) bila makato.

Kwa mfano, ukiwekeza TZS 1,000,000, utapata TZS 30,000 kila miezi mitatu, jumla ya TZS 120,000 kwa mwaka.

Jinsi ya Kuwekeza

1. Kwa Wateja wa CRDB Bank
Fungua app ya Simbanking, chagua Huduma > Samia Bond > Wekeza Sasa na fuata maelekezo.

2. Kwa Wateja wa Benki Zingine
Tembelea tawi lolote la Benki ya CRDB, chukua na ujaze fomu ya uwekezaji. Pia unaweza kupakua fomu hiyo kupitia tovuti ya CRDB, ujaze kwa umakini na kuwasilisha kwenye tawi lolote.

Kwa kuanza na TZS 500,000 tu, unapata nafasi ya kuwekeza kwenye maendeleo ya taifa huku ukijipatia faida nzuri na salama. Usikose fursa hii!
 
Biashara ya Bond inawafaa watu wenye majukumu mengi kiasi cha kukosa muda wa kushughulika na fursa mbali mbali mtaani ili kukuza kipato.
Yaani niwekeze 1M ili nipate 10K kwa mwezi. Dah!
 
Baada rais kuondoka madarakani Samia infrastructure raisi ajae akiifuta usalama wa pesa utakuaje
 
Ndio mambo wanayoyapenda hayo ma-Bank.

Hao watanzania wa kawaida wa kununua Bond na kuona tija wapo wapi.

Hapo wanazungusha hela za serikali, watatumia hela za mashirika ya serikali ambazo zipo kwenye savings. Riba labda asilimia 5%-7%. Halafu wao hela hela hizo wanaenda ikopesha serikali kwa riba ya 15%.

CRDB wakiikopesha serikali billion 120 (hela zao wenyewe ambazo taasisi zake zinaweka) kwa riba 15%.

Maana yake nini, ukitoa interest wanayopokea serikali kwenye saving labda 7%, kwakuwa wanakopeshwa hela hela hizo na kuwalipa CRDB 15%; in other words serikali inailipa CRDB 8% kuweka hela bank.

Upuuzi huu Magufuli ndio alikuwa hataki, akataka hela zote za serikali ziende hazina. Mafisadi sasa ohoo anaua uchumi.

Sasa hivi wamepata mtu wa kumng’ong’a hela za serikali anayoongoza yeye mwenyewe ndio anakopeshewa na kumpamba kwa kuziita Samia Bond.

In Magufuli’s voice “ndugu zangu tumechezewa sana, hii nchi sio maskini”.

Ni watu wa hovyo tu ndio hawakumuelewa Magufuli.

Mambo yaMerici kuwa ya hovyo kipindi cha JK afadhali, the worst is yet to come; best believe.
 
Back
Top Bottom