Manji atimkia Nairobi
27 Nov 2008
By Mwandishi Wetu, Jijini
Mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu aliripotiwa kuwa yu taaban na akakimbizwa Nairobi, Kenya kwa matibabu, eti hali yake imekuwa mbaya tena na inadaiwa tayari keshasafirishwa fasta fasta kupelekwa huko Kenya.
Taarifa ambazo zimetua mezani mwa Alasiri asubuhi ya leo, zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikimbiziwa Nairobi jana ikiwa ni masaa machache tu baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Aga Khan ya Jijini.
Taarifa zaidi zimedai kuwa awali, alifikishwa hospitalini hapo mishale ya kati ya saa 7:00 na 8:00.
Chanzo chetu kimedai kuwa baada ya kufikishwa hospitalini hapo, mfanyabiashara huyo alikimbiziwa moja kwa moja chumba cha dharura, yaani \'emergency room`, ambako huko aliendelea kuhudumiwa kwa muda wote.
Hata hivyo, chanzo hicho hakikueleza mfanyabiashara huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo gani la kiafya na pia, ni muda gani alitolewa na kukimbiziwa Jijini Nairobi.
Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, Manji aliwahi kuripotiwa kuwa aliugua na kulazwa katika hospitali hiyo ya Aga Khan ambako inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na presha ya kupanda.
Pia ilidaiwa kuwa wakati alipolazwa katika mwezi huo wa Septemba, Manji alikuwa akisumbuliwa na malaria iliyompanda kichwani na kumfanya azungumze mambo yasiyoeleweka, kiasi cha kuwafanya ndugu zake wamfunge kamba kwa hofu kuwa pengine angeweza hata kujirusha toka kwenye ghorofa ya wodi aliyokuwa amelazwa.
Baada ya kutibiwa hospitalini hapo na kisha kuruhusiwa, inadaiwa alizidiwa tena na hivyo ndugu zake kulazimika kumrejesha hospitalini ambako alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, ICU kabla ya baadaye kupelekwa katika hospitali nyingine ya Aga Khan iliyopo Nairobi nchini Kenya.
Wakati huo huo, baada ya kufikishwa mahakamani kwa mawaziri wa zamani wa awamu ya tatu ambao ni Basil Mramba na Daniel Yona, inadaiwa kuwa hofu kubwa imetawala miongoni mwa baadhi ya vigogo wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.
Chanzo chetu cha kuaminika kutoka Serikalini kimedai kuwa baadhi ya vigogo wamesoma alama za nyakati na kuona kuwa upepo unaweza kuwaendea vibaya na hivyo kuanza kuhaha huku na huko, kwa nia ya kuhakikisha kuwa nao hawafikishwi kortini kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo zile za kutumia madaraka yao vibaya.
``Kuna kesi nyingine tatu ziko mbioni kuanza na hatimaye kuwafikisha kortini vigogo wengine wakati wowote ule kuanzia sasa,`` kimedai chanzo hicho.
Mramba na Yona walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi na kusomewa mashtaka kadhaa, likiwemo lile la kutumia madaraka yao vibaya na kuliingizia taifa hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 11.
Mawaziri hao wa fedha wa zamani katika vipindi tofauti vya Serikali ya Rais Mkapa, walishindwa kutimiza masharti waliyopewa ili wapate dhamana na hivyo wakajikuta wakiswekwa katika mahabusu ya Gereza la Keko.
* SOURCE: Alasiri
Naona JF ni more credible kuliko hii. Naomba msome tu kuona kilichoandikwa na mwandishi huyu na tuendelee kufuatilia ukweli. Lakini nafurahi sana watu walituibia na kutudhalilisha na kuwadhalilisha baba zetu sasa kuna dalili za kuwafikisha kwenye mkono wa haki. Kama mliyosema wana JF wengine kama Manji alitaka kufuata nidhamu ya Japan that is well and good, as long as amejiona guilty basi sisi tuchukue hela zetu tu na zitumike kuwasaidia waibiwa.