Huo uimara ulikuwa enzi hizo kaka, ukitaka kuamini hizo gari si lolote si chochote nunua mpya ya kisasa utumie katika mazingira yetu ya Tanzania uone hio teknolojia unayosifia kama haitakutoa nishai.
Chukua gari unazoita za uhakika Landrover mpya latest technology kazitie off-road ziloane na maji ya madimbwi na matope ya wilayani huko halafu uone kama mna gari mle. Utabadili sensor baada ya sensor mpaka akili ikukae sawa na yet bei ya vipuri sio rafiki ni million baada ya million.
Enzi za carburetor ilikuwa rahisi kutengeneza gari yako mwenyewe bila hata kumshirikisha fundi sana. Tatizo likiwa kubwa ni kubadili plug, fuel pump, oil filter, kumwaga oil, brakes,springs na bush. Ziada ni labda radiator inavuja ama kuziba pancha na kubadili matairi yakiisha.
Na ndio kipindi ambacho kulikuwa na gari imara hamna mfano ila kwa sasa ambapo kila kitu ni umeme kwenye gari mfumo umekuwa complex na sio reliable kabisa hasa kwa hizo makes za ulaya. Usidanganye watu mzee baba.
Huwezi kusema gari ni imara kama utatumia karibia au zaidi 50% ya bei ulionunulia kwa maintainance ndani ya miaka michache ya matumizi. Hizo gari uhakika wake ni wa mashaka, labda utoke nalo masaki-posta miaka yote utayolitumia which is never the sole purpose of an off-road vehicle.
Hujiulizi kwanini baadhi ya wizara wamezi ditch na kuhamia kwenye ma Land cruiser hardtop na LX. Hizi ndio gari pekee ambazo hazijawa na mabadiliko makubwa ya kupelekea complexity katika maintainance. Engine ni zile zile na mfumo ni ule ule miaka yote hamna umeme mwingi. Mabadiliko ni kwenye shape ya body tu