- Source #1
- View Source #1
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dr. Emmanuel Nchimbi, amefanya ziara ya kushtukiza na ya faragha usiku wa manane katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumjulia hali na kumpa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Ziara hii imefanyika katikati ya siku za mwisho za eda ya Rais Samia kufuatia msiba wa mume wake, huku ikiwa na lengo la kutoa faraja ya kibinadamu pamoja na kuondoa taharuki na maswali mengi miongoni mwa wananchi baada ya ukimya wa Dr. Nchimbi wa takribani mwezi mmoja tangu kuibuka kwa uvumi wa kujiuzulu kwake.
Ili kulinda faragha yake na kuepuka vyombo vya habari, Dr. Nchimbi aliwasili Ikulu katika mazingira ya giza nene bila mpango wa kupigwa picha rasmi, hatua iliyowalazimu wasaidizi wa Rais kumuamsha kiongozi huyo kutoka usingizini.
Hata hivyo, pamoja na jitihada zote za kufanya kando ya ulingo wa hadhara, taarifa na picha za mkutano huo ziliibuka na kusambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na wanaharakati wa mtandaoni, zikimwonyesha akiwa na afya njema na kukomesha uvumi uliokuwa ukisambaa.

- Tunachokijua
- Kumekuwa na picha ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa ikimuonesha Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Nchimbi akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakiwa pamoja Ikulu, kufuatia kifo cha mumewe Hafidh Ameir.
Picha hiyo imeambatana na yanadai: "HATIMAE JANA USIKU DR.NCHIMBI AMEONEKANA HADHARANI GHAFRA AKIWA MZIMA WA AFYA ALIPOOENDA KUMPA RAISI SAMIA POLE YA MSIBA PALE IKULU,MLOSEMA HAWA NI MAADUI MTAFICHA WAPI SURA ZENU".
Uhalisia
Ufuatiliaji uliofanyika kwa kutumia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa Taarifa hii si ya kweli Picha iliyotumika imehaririwa kutoka kwenye moja ya picha halisi ambapo Rais Samia alikuwa akipokea salamu za pole alipokuwa katika Ikulu ndogo Zanzibar.
Hakuna taarifa yoyote rasmi kupitia Tovuti Rasmi ya Ikulu au vyombo vya habari vya ndani ama vya nje vinavyoaminika ambavyo vimechapisha kuwepo kwa mkutano au ziara ya Dkt. Emmanuel Nchimbi Ikulu kumpa pole Rais Samia Suluhu Hassan.
Hadi sasa kumekuwepo na maswali mengi ni wapi alipo kiongozi huyo mstaafu kutokana na ukimya wake toka alipochapisha taarifa yake ya kumuandikia Rais barua yake ya kujiuzulu.