Hatimae Flora Mbasha awa Flora Kusweka

Naomba Mnaojua misingi ya Ndoa hasa za Kikristo mnijibu yafuatayo,
Hivi kila Ndoa inayofungwa kanisani na kunukuu viapo Kwa kuvitamka Kwa mdomo huwa kweli zote ni halali na anakuwa kaunganisha MUNGU?
hivi mtu tapeli anaelenga maslahi Wakati maslahi si msingi wa Ndoa nae kukarili viapo na Kutamka anakuwa kaunganishwa na mwenzake Mwenye nia ya dhati na inapaswa Aina hii tuseme kaunganisha MUNGU?,
Iwapo mwanandoa mmoja hakuwa na Nia toka awali ya kuishi milele ktk Ndoa Lkn akakarili kitapeli viapo na kukubali kiuongo ili tu atimize malengo na hii tutasema kaunganisha MUNGU,
Km ni Mpaka kifo kitenganishe Kwa nini mnanukuu kifungu cha uzinzi kinachohalarisha talaka?inamaana uzinzi ndo kifo,
Inakuaje Kwa akina dada na kaka wanaofunga Ndoa Kwa kufuata Mali, na hawa wanapaswa kuhesabiwa km wanandoa ambao Mungu kaunganisha au Mali na tamaa zao zimeunganisha?
Kwa hayo maswali Yangu yanayo akisi kinachofanyika ktk ufungaji wa Ndoa je mnauhakika gani kuwa kila inayoitwa Ndoa huwa kweli imeunganishwa na MUNGU?
Je ni sahihi Ndoa ambayo ilikuwa na utapeli wa misingi na lengo la Ndoa ikivunjika tunapaswa Kusema alichounganisha MUNGU?
Mnajuaje Sasa km ni Ndoa ipi mmoja alimtapeli mwenzake ili iwape usahihi wa kutumia fungu la alichounganisha MUNGU binadamu asitenganishe maana Siri ya dhamira ya MTU kufunga Ndoa anayo muhusika?
Mnaonaje tukisema MUNGU ndo anajua uhalali wa kila Ndoa maana zipo zinazofungwa kibatili Toka mwanzo?
Na hii ya Mbasha mnauhakika gani kuwa ilikuwa si batili since day one au ilikuwa batili since day one?
Nikimdanganya MTU kuwa nipo tayari kuishi nae milele Kwa shida na raha Wakati najua Moyoni sipo tayari na sintadumu nae nimelenga kitu je Ndoa hii nayo imeunganishwa na Mungu?
Mambo ni mengi Sana
 
Umeuliza swali la msingi mkuu naamini wakakapokujibu itanisaidia na mm kupata majibu
 
umetudanganya live
sema hupendi kubadili jina
siyo kubadili jina kumepitwa na wakati.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kumepitwa na wakati aisee,huoni Flora anavyotupa shida kujua ubin wake?
Korora/Mbasha au Kusweka?
Imagine bibie Dida angekuwa anabadilisha ubin kila akiolewa tungekuwa tumesha msahau kwani angetupotea kabisa!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kumepitwa na wakati aisee,huoni Flora anavyotupa shida kujua ubin wake?
Korora/Mbasha au Kusweka?
Imagine bibie Dida angekuwa anabadilisha ubin kila akiolewa tungekuwa tumesha msahau kwani angetupotea kabisa!
ila kwa iman ya waislam nadhani wao si lazima kubadikisha jina

ila isikupe shida, akiachika si unajua kabsa si jina lake, endelea kutumia jina lingne, na ujue vile utaolewa unamwambia mumeo eti sibadili kwa kuwa twaeza peanwa talaka[emoji23] [emoji23] , lazima akushangae asee, utamwakeza vzuri
 
KWANI HUYU KUSEKWA NDO KAMUOA FLORA AU FLORA NDO KAMDANGANYA HUYO "MINOR" NA KUMUOA ! KWANI HUYU KUSEKWA NI KUSEKWA YUPI JAMANI ANA ROHO NGUMU HIVI! HII NDOA IMEFUNGWA KWENYE MADHABAHU YA KISHETANI NA SIO YA MUNGU HATA KAMA MADHABAHU HIYO IPO NDANI YA KANISA LA KILOKOLE.NI YA KISHETANI KWA SABABU EMANUEL MBASHA BADO YUPO HAI.HIYO SPIRIT ILIYOMTENGANISHA FLORA NA MBASHA BADO IPO NA SUALA TU LA MUDA,ITAIVUNJA TENA HII NDOA YA SASA HIVI.BAADA YA MUDA MFUPI UJAO, HII SPIRIT YA KISHETANI ITAMFANYA HUYU DOGO KUSEKWA AJITAMBUE.AKISHAJITAMBUA TU ATAONA DAH ! KUMBE NIMEPIGA CHINI HIVII ! DOGO HAPO ATAANZA KUCHEPUKA MAANA ATAONA KUMBE FLORA HAKUWA SIZE YAKE HASA AKILINGANISHA AGE, NA HISTORIA YA HUYO FLORA....HAPO NDO HIYO UNCLEAN SPIRIT ITAIBUA UGOMVI MKUBWA KATIKA NDOA HII MPYA KULIKO ILE YA KWAKE NA MBASHA.
 
Sitakaa nifanye huo upuuzi wa kubadili jina la ubin wangu! Ndoa zenyewe ni za kukaa mguu ndani mguu nje.
Mbali na hapo nchi yenyewe haieleweki unaweza shangaa unatumbuliwa bure eti watumia cheti feki.
 
Hivi ninyi mnaobwabwaja humu wangapi Mko kwenye ndoa? Na mmedumu kwa muda gani? Biblia ni Isigeuke kuwa mzigo, kwa habari ya uzinzi na uasherati ni ruhusa kudai au kutoa talaka sasa ninyi mnazijua changamoto zilizokuwa ktk hiyo ndoa hadi wakakubaliana kupeana talaka? Mambo mengine muachage ujuaji
 
Sitakaa nifanye huo upuuzi wa kubadili jina la ubin wangu! Ndoa zenyewe ni za kukaa mguu ndani mguu nje.
Mbali na hapo nchi yenyewe haieleweki unaweza shangaa unatumbuliwa bure eti watumia cheti feki.
aaaah! huwa hawabadili vyeti bhana [emoji23] [emoji23]

unabadili katika ile social status stuu, mi mwenyewe nikioa mke wangu hawezi badili jina la kwenye vyeti vyake au kazini ( though mke wangu atakuwa ana cheti cha la saba tu, akizid saana cha form four, so haito leta shda) but kwenye ishu za kijamii tu ndio unabadili ni heshima kwa mumeo na kwa jamii pia, ndio hata unakna kina michelle ni michelle Obama,

sema pia unachonga sana kwakuwa hujui mumeo atakuwa nan, mwenzio hillary alikuwa na kiburi hivo hivo, mumewe alipo ukwaa Urais akabadili fasta[emoji23], na wewe unaeza sema ooh sibadili, ukaolewa na successful person of coz u will like to associate you name with his big nem
 
Ndoa ya kikristo inavunjika kwa sababu mbili
Uasherati
Kifo
Sasa kama mbasha alibaka, unataka nini tena!
lakini ni option ya kifo tuuu, ndio huruhusu ndoa ya pili.
ila masuala ya talaka yanataka mlo talikiana mkae hvo hvo single.
 
Wapo wanaobadili hadi vyeti,mfn Mch.Getruda Lwakatare.

Kwa issue ya u first lady nitabadili hadi vyeti [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Wapo wanaobadili hadi vyeti,mfn Mch.Getruda Lwakatare.

Kwa issue ya u first lady nitabadili hadi vyeti [emoji12] [emoji12] [emoji12]
hahahah
usibadili vyeti kwa kuwa haukufaulu na mimi, thats your achievement. hilo halitakiwi au ile kuanza kuwasumbua watu kazini ooh sasa mniiite Thad Iceman, kuwa kuwa nshaolewa, hiyo haijakaa poa unless wao wametaka wakuite hivo.

hahahaha, ndio wanawake wengi husema hawatabidili kwakuwa tu siye wanaume hatuja achieve viti impressive, ila watu kuwa mama Diwani tu wana tupa shida [emoji23], sembuse akiwa Rais hapo najua utabadili fasta tu
 
Mbona hayumo humu.Au unampa hongera flora gani?Halafu mbona umekuja kama umemezeshwa ujumbe.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kitakachobadilisha ubin wangu ni u first lady tu basi....huo uheshimiwa wa ubunge na blah blah zingine,never!

Btw best unalalaga saa ngapi? Maana kila nikipitaga huku nakukutaga hadi mida ya wanga [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Mbona kila siku huko majuu wasanii wanaolewa na kuachana. Mnataka sema uwa hawatumii vitabu hivi hivi vya dini? Halafu hata hapa bongo kuna mzee miss Tanzania kwani mke wake hakuwepo. Hacheni dada asitiliwe ni aibu kumkuta dada yako anabadiri wanaume. Tujipime hata sisi tunaokosoa hatutoki nje ya ndoa? Maana siku hizi nimexperience kua wake za watu wengi uchukuliwa na vijana haswa makazini kisa ukaribu tu. Tujisahihishe wenyewe kabla ya kumkosoa flora. Je kwa umri angeishi bila mume si angekua anafanya mambo ya aibu kumbuka nae ni binadamu. Mambo ya ndoa yana siri nyingi tukubali tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…