Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Hapo naomba unifafanulie kidogo mkuu, maana tumesha saini hukumu, japo baada ya 45 days itakaziwa rasmi. Je una maanisha kuna uwezekano mdai akakata rufaa kupinga matakwa yake mwenyewe? Kwamba alitaka taraka na sasa hataki??

Kwa Sababu alibaki anaweza tengeneza mazingira Kaka then mkarudi kwenye usuluhishi, trust me, either way Bro, nakupongeza, you have nothing to lose! Usikubali kesi, wala mazungumzo, na Kama akisema kabadili mawazo, ondoka kaa kimya tena hivyo hivyo!

Nakutia moyo Kaka, Umefanya jambo sahihi sana la kukukomboa na drama za huyo Shemeji yetu wa hovyo, at this stage you have nothing, I repeat again nothing to lose!
 
Ni kabila gani huyo wife wako?
 
Moja kati ya uzi wenye mengi ya kujifunza , tunakushukuru sana mleta mada kwa kutushirikisha.

Kwanza kabisa ni neno la faraja kwako , pole.
Pili neno la pongezi kwako, hongera sana.

Ukisoma maoni ya wengi kwenye uzi huu toka maoni ya kwanza hadi sasa lawama nyingi zinaelekezwa kwa mwanamke na kuonyesha ile maana ya maisha ya pamoja kati ya mwanamke na mwanaume haipo tena.

Ukweli hio maana au ule umuhimi haupo tena na si kwa sababu ya mwanamke pekee hadi sisi wanaume.

Binafsi naamini nature imemfanya mwanaume kuwa kama kiongozi kwenye familia au mahusiano tunayoweza kuyaita ndoa.

Inapotokea hayo mahusiano yanakuwa isivyo kawaida yule aliye kiongozi kuna sehemu ameshindwa kusimama katika nafasi yake.

Si zungumzii mume tu bali hata baba .
Kuna namna imefanywa mwanamke hakupaswa kutoka mikono mwa mwanaume kwa karibu kipindi chake chote, ata toka kwa baba atakuwa kwsa mume.

Sasa mwanamke anapo kosea sambamba na kumlaumu lakini tujiulize nasi kama waanaaume tumeweza kusimama katika nafasi yetu.



Maoni ya wengi kwenye uzi huu yamekubaliana na kauli iliyopo sasa ya kukataa ndoa, wengi walio toa maoni haikosi robo walio kwenye ndoa,

Na kama kuna yoyote aliye kwenye familia ama ndoa ambaye yupo na watoto, nadhani wanafahamu fika mtoto atakavyo kuwa mwaathika wa kwanza endapo kutakuwa na mgogoro .

Kuwa hio inapofika wakati wa mgogoro kama sababu hazikidhi haja heri kuvumilia kwa ajili ya nusura ya watoto...


Nadhani pia kuwepo na namna sauti ya mwanaume ipaaazwe serikali na watunga sera na watu wa dini waone namna ya kubadilisaha hizo sheria zinazo husu mambo ya ndoa na mahusiano.

Maisha ya mwanaume ni magumu sana , tokea siku ile anaitwa mwanaume ni mtu asie hitajika na dunia, anaye kandamizwa kwa kila namna na ambaye hatakiwi kuonewa huruma hadi siku ile atakapo rudi kwenye ardhi.

Embu watusaidie hao watu maana dunia imetuelemea mno, embu wafanye tu inavyo wezekana mwanaume nae asikilizwe.


Pia wanaume wenzangu kwenye kuijenga familia na ustawi wake , tufikirie kuwa na mji wa pili usiohusiana kabisa na familia,hii inaweza kusaidi inapotokea hali kama hii, au huko uzeeni watoto na mama yao watakavyo kosa umuhimu wako uwe na sehemu ya kwenda kuvutia faraja.
 
Pale anapoanza kuonekana mfalme ndio hapa Sasa.
 
Je huyo yf wako alichangia katika kuijenga Nyumba ?

Au umeamua kumnufaisha
Siwezi deny mchango wake kwenye ujenzi, lakini ni kwa sehemu ndogo sana, na nina vithibitisho vya kibenki kuhusu kila shilling 5 alioingiza bank, hivyo nimeamua kumnufaisha kwakua sikutaka hili shauri lipite jana liitwe tena aiku nyingine ndio maana nikaamua hivyo
 
Hongera brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…