Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ya nini bana!Kuna msimamo mmoja wa kisheria ulitolewa kwenye moja ya kesi maarufu unasema ''sio tu haki itendeke, bali ionekane ikitendeka'' sasa kwenye kesi ya jamaa hayo hayajafanyika, kama siku moja Hakimu Mfawidhi akikutana na hilo jalada na uhakika atalifanyia marejeo
Mkuu ahsante sana.Mkuu Fanton Mahal kwanza pole na habari za kesi (kesi zinakula sana muda wa wadaawa) ila Mkuu nikuhakikishie jambo moja hapo hakuna mlichokifanya wala kukikwepa kwenye swala la muda. Nitakuambia kwasababu gani nasema hivyo.
Kwanza kabisa kesi zote za madai ya hamri ya talaka ni sharti la lazima zisikilizwe ushahidi hii ni ili Mahakama ijiridhishe kupitia ushahidi uliotolewa kuwa kweli hiyo ndoa imevunjika kiasi cha kushindikana kurekebishwa.
Nimesikitika sana juu ya mwenendo uliochukuliwa na Mh. Hakimu husika maana ni amefanya kituko cha aibu sana.
Tukiachana na hili la amri ya talaka embu tuangalie hapo kwenye chumo la pamoja yaani mgawanyo wa mali na mali zenyewe.
Kwanza kama imeenda hivi ulivyosimulia hapa ni dhahiri na wazi kuwa mkeo ameshindwa kuthibitisha kwanza uwepo wa hizo mali zilizotokana na ndoa, kwanini nasema hivyo ni kwasababu hizo mali ambazo bado mkapewa mgao wa 60%kwa 40% bado hata hazijatajwa hapo Mahakamani. Sasa mimi na wewe na wana JF wote tujiulize mmegawana mali gani na ipi hiyo ambayo imetajwa Mahakamani?
Tuache hili la mali na mgawanyo wake embu tuangalie hilo lingine la kuhusu watoto ambao nao mmesema wakae na mama yao, tujiulize swali tena ni watoto wapi hao?, ni nani na nani kwa majina yao?, je walitajwa hapo Mahakamani na kutambuliwa inavyopaswa kuwa?.
Hii ni aibu nyingine kwa mhimili wa Mahakama, na hapa haujatoa rushwa (sababu hujataja swala hilo) ila Mh. Hakimu kwa uzembe wa kukosa weledi amekinzana na taratibu zote na sheria zote zinazosimamia mashauri ya migogoro ya ndoa.
Nina uhakikakama utaitaja hiyo Mahakama basi hilo jalada litaitwa na Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya maana hii ni aibu na imeshakuwa mazoea sasa.
Hata kwa kuokoa muda wenu basi Mahakama ingepokea ushahidina utetezi siku hii hii moja kuliko kukanyagataratibu hivi zilivyokanyagwa. Ninaelewa kusudio lako la kuokoa muda na gharama lakini hii wiki na wewe umejifunza utaratibu usio sahihi wa namna kesi za talaka zinavyoenda.
Kesho au keshokutwa utamshauri mtu au kumpa uzoefu wako huu na akikutana na Mh. Hakimu anayejua nini kinatakiwa kufanyika ataanza kuhisi au kufikiri kuwa Hakimu husika anaweka mazingira magumu ili adai rushwa, mwisho wa yoteni kukosa imani na Mahakama na mfumo wake wote.
Hili linasikitisha sana.
Naona umeamua umtafutie kabisa mke.Wakati anaendelea na tiba mnakua marafiki.

Nishamaliza kazi Fanton Mahal ushindwe wewe tu.Naona umeamua umtafutie kabisa mke.
Mi ni pasua kichwa asieeeh acha tu niendelee kujikuna mgongo ukutani!
![]()
Bora yameisha...Ila kesi za talaka ni Kama kesi za mirathi haziishagi,huo ni mwanzo Tu..kila la kheri
ahahahahahhahahahha!Nishamaliza kazi Fanton Mahal ushindwe wewe tu.
Ahahahahahah..huyu mdogo angu ,jeuri sana huyuNaona umeamua umtafutie kabisa mke.
Mi ni pasua kichwa asieeeh acha tu niendelee kujikuna mgongo ukutani!
![]()
Nakupigia pasi, unahitaji mtu mzima aliyevuka milima na mabonde ndio mtadumu.Ahahahahahah..huyu mdogo angu ,jeuri sana huyu
All women are devils only your mother mighty be good to you, but she is still a devil to your father.Mungu akutunze, vita bado ni Kali. MWANAMKE ni shetani, furaha yake wewe uangamie na kufutika kabisa.
Na miaka 50 ijayo AI ndio itakuja na mfumo mpya wa kazi bila binadam ucjaliSikusoma Uzi wa kwanza ila niseme tu umekutana na vita!
Muktadha wa madaraka uliosema ni matokeo ya woman empowerment hata hivyo Hilo ni tone tu baada ya miaka 50 kutoka Sasa wanaume watakuwa kwenye ujenzi na kuchimba mitaro plus labda u driver
Hili limeumiza wanawake wengi sana. As soon as mwanaume akijua kimada anayetembea naye ameachwa, basi anaanza kumkwepa. Ukiona mke wako anakuletea ghafla jeuri mbaya, haambiliki basi ujue keshapata mtu. Watu wengi wanaona ni kama fahari kutembea na mke wa mtu plus gharama zinakuwa ndogo.Kibaya zaidi akiachika na mchepuko anamuacha kwani mchepuko anaogopa atapewa majukumu kamili ya ulezi
ahahahaaahaha nakuona Aziz KiNakupigia pasi, unahitaji mtu mzima aliyevuka milima na mabonde ndio mtadumu.
Daaah pole mno kaka 😔😔😔😔😔😔Wakuu heshma kwenu.
Habari za jioni.
Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu 👇👇👇👇
Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali
Wakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu. Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana. Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya...www.jamiiforums.com
"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.
Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
Hakika wanawake wametaradadi everywhere, tukiendelea kwa mwendo huu, wanaume twafaaa
- nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
- leo hii mahakamani, hakimu alikua mwanamke.
😁😁😁😁😁.
Anyway,.
Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.
Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"
Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto
Akauliza "unasemaje?"
Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"
Akauliza "umekubaliana na haya yote?"
Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"
Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.
Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.
Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.
Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.
1. Talaka.
Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.
2. Mgawanyo wa mali.
Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.
3. Matunzo ya watoto
Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.
4. Kuishi na watoto.
Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.
Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.
Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"
Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"
Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.
Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.
Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.
PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.
Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.
Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.
Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!
Ikaisha hivyo.
Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.
ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani
SHUKRANI WAKUU.
Usiku mwema
Ushauri mzuriii mkuuPicha lilipoanza ulionyesha ni jamaa Lia Lia + kulalamika .
Demu utombewe, ukute na picha za utupu, alafu wee ndio ulielie.
Anyway , X Mkeo alijua utazungusha suala la Talaka, Sasa haamini ndo Ivo Kawa mtalikiwa.
Mchepuko wake hawez kumuoa sababu keshazaa watoto wengi, Engine imechoka , na sababu kubwa kabisa ya kutomuoa ni kwamba kashuhudia demu anavunja ndoa yake mwenyewe .
Mwisho, Hongera , kuanza Upya Si ujinga.
Muda mfupi ujao, jiandae Ndugu zake na viongozi wa Dini kuanza kukubembeleza.